Morogoro: Dereva bodaboda auawa, atobolewa macho

Morogoro: Dereva bodaboda auawa, atobolewa macho

Nilijua tu lazima watu watahusianisha na mambo ya mapenzi yaan akili zetu wa bongo zinawaza mapenzi tu, mtu akijirusha ghorofani mapenzi, mtu akijinyonga mapenzi, mtu akijipiga risasi mapenzi , mtu akiuliwa mapenzi
yaan kila kitu huwa tunahitimisha kwa jibu la mapenzi bila kuwa na taarifa kamili

Hakuna anaewaza labda katobolewa macho akiwa anajaribiwa kuporwa pikipik au labda mambo mengine
Watu ni mapenzi tu wanawaza ..ubatili mtupu
 
Kuna stori sijui ka umewahi kuzisikia kuwa kile kiini cha jicho kuwa kinatunza picha ya mtu aliyemuona kwa mara ya mwisho?

Wauaji pengine walikuwa na mindset hiyo wakaogopa ikitokea polisi wanafanya upelelezi halafu wakafika hatua ya kuangalia jicho liliona nini mara ya mwisho si wataweza kuwa exposed

Nadhani ndio sababu ya kumtoboa macho
Hizi story za vijiweni tu kama zile za kusema ndege ikigusa mchanga inalipuka.

Wewe jicho linatunzaje image ya mwanadamu limekuwa kamera.
 
Kamsome Willy Kuhne kuhusu optograms

Halafu kuna rekodi ya mwaka 1857 iliyoripotiwa nchini London kuonesha kufanikiwa kupata image ya muuaji kupitia retina ya jicho.

Pia kuna mwana physiologist anaitwa Franz Boll huyu ndio aliyegundua biochemical mechanism inayofanya hicho kitu kiwezekane.

Pia nakubaliana na wewe kuwa vipo vyanzo ambavyo vimepinga haya madai
Hii ingekuwa ni kweli basi zile open cases nyingi za huko USA za mauwaji zingekuwa solved
 
Hizi story za vijiweni tu kama zile za kusema ndege ikigusa mchanga inalipuka.

Wewe jicho linatunzaje image ya mwanadamu limekuwa kamera.
Umejisumbua kidogo kusoma hizo details nilizokuwekea?
 
Umejisumbua kidogo kusoma hizo details nilizokuwekea?
Yeah nimesoma. But if ingekuwa ni effective method then fuatilia zile cases za Serial killers huko USA uone namna askari wanahangika upelelezi uone kama wanaongelea swala la macho kutumika kama kitendea kazi.
 
Mi mwenyewe nimefikiria hivyo ila nilichowaza pengine ni njia moja ngumu sana ambayo inaweza kukupa majibu tofauti

Kwasababu kuna process zimeelezewa kuwa unaenda mpaka kwenye ubongo ambapo taarifa zote za jicho zinapotafsiriwa.

Yani optogram ni very paradox and confusing
 
Dereva wa Bodaboda, Oscar Samuel (36) Mkazi wa Mtaa wa Kilongo B Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro ameuawa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kutobolewa macho na Watu wasiojulikana.

Akiongea na @ayotv_ Mdogo wa marehemu, Huruma Samweli amesema May 31,2023 Oscar alimuaga Mkewe anaelekea shambani eneo la CCT Forest Manispaa ya Morogoro na hakurejea tena hadi Juni mosi mwaka huu walipokuta mwili wake umetelekezwa msituni ukiwa na majeraha huku macho yametobolewa na pikipiki haipo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilongo B Paul Laurence amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kwa sasa wanaanza msako kuwatafuta Vijana wote ambao wanakaa vijiweni na kuvuta bangi ili waweze kuchukuliwa hatua kwani huenda ikawa sababu ya matukio kama hayo kutokea katika Mtaa wake.

Chanzo: Millard Ayo
Mwenyekiti wa mtaa hajielewi.
 
Huyo jamaa(R.I.P) sio bodaboda kwa maana ya kusafirisha abiria ila anamiliki pikipiki na biashara yake kuu ni kuuza maji na mkaa pia. Pikipiki iliyoibiwa huku wanaita mcharaka yaani imeisha.
Plus huyo mwenyekiti ni ndezi anataka akamate wavuta bangi na tukio halijatokea mtaani kwake.!
 
Wee uko hapo karibu na eneo la tukio??
 
Kamsome Willy Kuhne kuhusu optograms

Halafu kuna rekodi ya mwaka 1857 iliyoripotiwa nchini London kuonesha kufanikiwa kupata image ya muuaji kupitia retina ya jicho.

Pia kuna mwana physiologist anaitwa Franz Boll huyu ndio aliyegundua biochemical mechanism inayofanya hicho kitu kiwezekane.

Pia nakubaliana na wewe kuwa vipo vyanzo ambavyo vimepinga haya madai
Bila kwenda kusoma hizo rejea zako, hili ni jambo nililo na uhakika nalo: HALIPO. Kuna jitihada kubwa zilifanywa na huyo mjerumani Will Kunhe lakini hakufanikiwa na mpaka sasa hatujafanikiwa. Kuna forensic methods nyingine nyingi tu za kisasa zinatumika na zinaoneka zikitumika in real time na ushahidi wake kupelekwa mahakamani na watuhumiwa kutiwa hatiani. Nitajie hata kesi moja ambayo hii njia imeshatumika na mahakama ikamtia hatiani mhalifu!
 
Back
Top Bottom