Uchaguzi 2020 Morogoro: Devotha Minja amewasilisha fomu bila picha kitendo kinachomnyima sifa ya kuwa Mgombea

Uchaguzi 2020 Morogoro: Devotha Minja amewasilisha fomu bila picha kitendo kinachomnyima sifa ya kuwa Mgombea

Eti dosari siku zote ni kwa wapinzani tu ccm hawafanyi makosa..!! Hakuna nchi inayoweza kuendelea huku ikidhulumu wananchi wake.
 
Hili sio tatizo la Chadema bali ni tatizo la tume. Watu tumebarikiwa kuwa na akili kuliko nyani lakini wao tume wanafanya mambo ya kijinga kuliko hata nyani wenyewe!
Mbona mlishaambiwa mjaze form na mawakili sasa mna shindwa nini?
Mna wasomi wengi ila kazi hawana?
Hizo pesa za ruzuku zinfanya kazi gani?
 
Mpunga Mpunga Mpunga......halafu alisikika KAMANDA mmoja aliye pale "machinjioni" Njendengwa,TUNAONEWAAAAA.....
 
Kusahau picha ni tatizo la tume?
Mantiki yangu ni kuwa kurudisha fomu kusiwe na mitego ya kijinga. Makosa madogo kama kutokuwa na picha siyo ya kufanya mtu asigombee. Tume inatakiwa kufanya kazi kisomi kwa kutumia busara na siyo kwa mitego ya kijinga kabisa. (hapa nimejibu nuki-assume ni kweli alisahau picha kwani ''makosa'' mengi ya wapinzani ni kutengenezwa).
 
Mbona mlishaambiwa mjaze form na mawakili sasa mna shindwa nini?
Mna wasomi wengi ila kazi hawana?
Hizo pesa za ruzuku zinfanya kazi gani?
Kwa taarifa yako mimi sishiki kwenye uchaguzi, siyo kwa kupiga kura wala kupigiwa kura. Natoa amoni yangu yatakayonya tume isionekane ina watu idiots. Vizazi vijavyo vitashangaa sana tume ilikuwa inaongozwa na mtu aliyefikia kwenye level ya ujaji kufanya kazi kwa njia za kitoto namna hii.
 
Hamna mahali paliposema kuwa picha ibandikwe kwenye fomu. Mara nyingi unapotakiwa kubandika picha kwenye fomu kunakuwa na kiboksi cha kuonyesha mahali pa kuibandika picha hiyo. Kwa hali hii picha zinaweza kuwasilishwa peke yake au hata kubandikwa nyuma ya fomu.

Amandla...
Bush Lawyer
 
..sasa si wampe nafasi awape hiyo picha?

..wasimamizi wanatakiwa wawezesha wananchi kugombea, na siyo kuwa kikwazo cha wananchi kugombea nafasi.
Mtu kakaa na fomu wiki nzima. Leo mnamuambia msimamizi wa uchaguzi ampe muda. Sheria ndo inavyosema hivyo?
 
Unajua watu wengi hawajui sababu ya vigezo vya kugombea ni lazima ujue kusoma na kuandika..SASA usipojaza fomu vizuri Kwa kufata maelezo yaliyoandikwa Kwa Kiswahili tafsiri yake inakua kwamba hujui kusoma au kuandika au vyote Kwa pamoja.

Sio kweli, unaweza kufanya kosa hata kama unajua kusoma na kuandika
 
Pamoja na Sheria na kanuni kufuatwa ili kutimiza matakwa fulani, kuna mambo ambayo katika hali ya kawaida hayapaswi kutumika kama kigezo cha kumuengua mgombea.

Makosa madogo madogo ya uandishi au kukosekana kwa picha vinatakiwa vipewe nafasi ya kurekebisha wakati mchakato ukiendelea.

Huu upuuzi ndiyo unaojenga hata tabia chafu za kuteka au kunyang'anya form.

Kama hakuna picha, unaambiwa ulete picha.

Fomu zaweza kujazwa hata kwa mtandao.

Maelezo ya kwenye fomu yanalenga kumtambulisha mgombea ili akapigiwe kura.

Lengo uchaguzi ni kupata viongozi kupitia sanduku la kura. Hayo mengine ni kuweka nafasi za nia ovu zinazonyima haki na kuzalisha ufisadi na udhalimu wa aina zote.
 
Ujinga mtupu, hiyo picha inawezekana wameitoa hao wasimamizi wa CCM wanamtafutia mgombea wa Chadema sababu ya kumuondoa kwa hila tu, wasimamizi wa uchaguzi hawaaminiki nchi hii, wana upendeleo wa wazi kwa wagombea wa CCM.
 
Huo no
Wakati tunalaumu Tume ya Uchaguzi kuna makosa ambayo yanaepukika kama hili la Devota Minja ni makosa ya Kitoto yanayofanywa na aliyekua Mbunge.

CHADEMA mchunguzeni huyu kuna viashiria vya Rushwa iliyopelekea kujaza Form hovyo pasipo kuambatanisha viambatanisho muhimu kama Picha.

Unaenda Kugombea Nafasi kubwa kama hiyo lakini Form yako hata kuikagua unashindwa?

Picha za Form zimeambatanishwa hapa chini kwa marejeo.

View attachment 1547771View attachment 1547772
Uzembe hayuko makini,passport size unaenda nazo wanabandika wao,kwenye form hapo no 4,pameandikwa vizuri tuu
 
Sio kweli, unaweza kufanya kosa hata kama unajua kusoma na kuandika
Na hapo ndipo wanapofail wengi..huwezi kumpereka MTU Bungeni akatunge Sheria alafu anakosea kusoma na kuandika..SASA akiletewa miswada mabundle ya papers si ndo itakua balaa... mbunge anaweza akawa hajui kujieleza au kujenga hoja but kutokujua kusoma na kuandika Kwa umakini ni sharti muhimu sana kwani huko Bungeni KAZI zao ni sensitive Sana na wakikosea tuu impact ni kubwa Sana.
 
Back
Top Bottom