Morogoro: Kijana Rogers Ludovick adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana

Morogoro: Kijana Rogers Ludovick adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Kupitia ukurasa wake Instagram Maria ameandika kuwa kijana Rogers Yohana Ludovick ametekwa Oktoba 7, 2025 katika eneo la Dumila, Kilosa mkoani Morogoro.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa saba mchana baada ya gari jeupe aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T324 ELK kufika ofisini kwake.

Watu wanne walikuwa ndani ya gari hilo ambapo watatu walishuka, kumchukua na kuondoka naye kuelekea kusikojulikana. Hadi sasa haijafahamika alipopelekwa

maria.png

IMG_8047.jpeg

IMG_8046.jpeg
 
Kitu watu hawaelewi ni kwa jinsi gani CCM hiko involved na haya mambo ya utekaji.

Yes! Yule bwana Mafwele na kundi lake ni watekaji wakubwa lakini wao wanafanya hivo kwa watu wenye platform kubwa i.e Polepole n.k.

Kwa vijana wa chini hawa wanachukuliwa na vikosi kazi vya CCM. Haijalishi unampinga mama dully au lah! Ikitokea chawa wa CCM amekushuku na kukuripoti kwa kikosi kazi basi wewe ni haki yao.

Unfortunately, hawa machawa watoa taarifa wamo hadi humu mitandaoni wamejaa tele. Kazi yao ni kupeleka majina ya “critics”. Takribani mikoa yote wapo na wamewapa jina kabisa, wanawaita “Drones”.

Safari ni ndefu sana.
 
Kwa hali ilivyo sasa hivi ni kama utekaji umehalalishwa na serikali na kufanywa kitu cha kawaida. Hawajali hata kuchunguza, ulisikia kauli ya Murilo juzi, anachukulia kama utani.

Hii ni hatari sana kwa kila raia. Jambazi, mshindani wa kibiashara, mtu yoyote yule anaweza kumteka mtu mwingine akijisikia watu wakadhani ni polisi wasitoe msaada wowote.

Sababu style ya kuteka ya serikali na majambazi ni moja.
 
Alikuwa mwanasiasa au ana umaarufu gani? Sipendi utekaji na ninalaani watekaji, je wengine wasiofahamika nao wakitekwa nani ataripoti humu, mfano member wa humu tusiyemjua akitekwa kuna wa kuripoti habari za kutekwa kwake au ndio itakuwa kimya?
 
Kuna yule binti Shyrose Mahande Mabula 21 mwanafunzi wa Mzumbe, Mbeya. Alitekwa siku kadhaa zilizopita inadaiwa na majambazi. wakadai pesa ransom, Baba yake akalipa lakini bado wakamuua.

Juzi tunaambiwa polisi wameua watu watatu wanadai walikiri kumteka Shyrose.

Baadaye tunaambiwa wale watatu waliouliwa walitumwa kumteka Mdude na viongozi wa polisi mbeya. Polisi wakaamua kuwaua walipotishia kutoa siri sababu hawakulipwa kama walivyokubaliana.

Story yote imejaa ukakasi, polisi kutumia majambazi kumteka mtu?
Baba yake Shyrose ni Daktari mbobevu, tajiri, lakini ni mwanasiasa pia. Uchunguzi wa kina haujafanyika.

Hii kesi ni kama imefungwa. Tunaelekea pabaya sana.
 
Alikuwa mwanasiasa au ana umaarufu gani? Sipendi utekaji na ninalaani watekaji, je wengine wasiofahamika nao wakitekwa nani ataripoti humu, mfano member wa humu tusiyemjua akitekwa kuna wa kuripoti habari za kutekwa kwake au ndio itakuwa kimya?
Naambiwa alihoji elimu ya kiongozi wa Afughanstan kupitia page ya wachokonozi
 
Back
Top Bottom