Kuna yule binti Shyrose Mahande Mabula 21 mwanafunzi wa Mzumbe, Mbeya. Alitekwa siku kadhaa zilizopita inadaiwa na majambazi. wakadai pesa ransom, Baba yake akalipa lakini bado wakamuua.
Juzi tunaambiwa polisi wameua watu watatu wanadai walikiri kumteka Shyrose.
Baadaye tunaambiwa wale watatu waliouliwa walitumwa kumteka Mdude na viongozi wa polisi mbeya. Polisi wakaamua kuwaua walipotishia kutoa siri sababu hawakulipwa kama walivyokubaliana.
Story yote imejaa ukakasi, polisi kutumia majambazi kumteka mtu?
Baba yake Shyrose ni Daktari mbobevu, tajiri, lakini ni mwanasiasa pia. Uchunguzi wa kina haujafanyika.
Hii kesi ni kama imefungwa. Tunaelekea pabaya sana.