Morogoro: Kuna sehemu kunajengwa msikiti mkubwa unaopakana ukuta na kanisa, Je hii imekaaje?

Afadhali zote ni nyumba za Ibada, cha msingi kuheshimiana na kuvumiliana bila makwazo. Ingekuwa ni BAR ama nyumba za starehe zimepakana na nyumba za Ibada hapo ingeweza kuleta sintofahamu kidogo.

Pia Watanzania tutambue changamoto ya Uhaba wa ardhi kwa siku zijazo. Itafikia wakati Jengo la ghorofa juu kuna hotels au bar, chini kanisa na floor ya mwanzo ni msikiti
 
Dar es Salaam, eneo linaitwa Darajani, Barabara ya Nyerere mkono wa kushoto kabla ya kufika petroli station kwenye kona ya Chang'ombe, kuna kanisa na msikiti wamepakana, hakuna mgogoro wowote kila mtu na hamsini zake. Kwenye kile kikanisa ndipo deal lilichongwa Reginald Mengi akaanza kuitwa Dk Reginald Mengi. Hii dunia iko poua sana, wanadamu ndio wenye shida!
 
Hakuna shida kwa maana ratiba zao za ibada haziingiliani.
Ni kama darajani oilcom mali asili msikiti na kanisa vimepakana.Na Hakuna mikwaruzano yeyeto lugha ya kiswahili imetuunganisha
 
Uhaba wa ardhi tza haupo hata miaka 500 ijayo
 
Achana nao.Mbona kule Yerusalemu kuna lile Hekalu lililojengwa na Mfalme Sulemani, nasikia linatumika na Wakristo na Waislamu pia, yaani upande mmoja Wakristo na upande mwingine ni Waislamu.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Lile kanisa la kisabato haina shida wasabato wamesali hapo kitambo na waisalam wanaswali pia hapo hapo hamna shida.
 
Kuna msikiti upo mjinì kati kati wanapaita masika unajengwa kwenye hifadhi ya bala bala
 
Nipo naishi mitaa hii hii karibu, ipo shida naiona siku za usoni! Msikiti umepakana na kanisa......
Watakubaliana tu kupeana muda hawa muda huu hawa muda huu alimradi maisha yaendelee,kasheshe siku upande mmoja upange speakers nje ili kuhubiri au upande mwengine ufanye kitu ili waumini wake wasogee kuabudu ndo watajua hawajui.
 
Nje ya mada tafadhali hebu fanya kufafanua sentensi ya pili kutoka mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…