Morogoro Kusini, Wilaya masikini kuliko zote Tanzania

Morogoro Kusini, Wilaya masikini kuliko zote Tanzania

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
Wilaya hii makao makuu yake yapo moro mjini kwa kuwa watendaji wengi wa wilaya hii wanakwepa maisha ya dhiki yasiyo stahili kuishi binadamu ndani ya wilaya.

ELIMU:
-Wilaya ya Morogoro hakuna hata shule moja ya Advance level (kidato cha tano na sita).
-Shule za msingi zilizopo ni duni chakavu tena zilizochoka.
-Hakuna walimu wa kutosha. Kuna shule kama shile ya msingi kitengu, lumba chini na lumba juu kuna mwalimu mmoja mmoja kila shule.
Mbunge ni wa ccm.

AFYA:

Wilaya hii hakuna hospital yenye hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Kuna kituo cha afya cha tawa eti ndo wanataka kuifanya hospital ya wilaya. Kiukweli haina hadhi, kama ingekuwa Dar hii ingekuwa zahanati.
Mbunge ni wa ccm.

BARABARA:
Unaweza ukafikiri kama nafanya uchochezi au masihara ila ukweli ni kwamba HAKUNA HATA MITA MOJA ya kipande cha lami. Barabara huku kwetu ni za vumbi zilizojaa makorongo zinazohatarisha safari.
Mbunge ni wa ccm.

UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.

Lakini pamoja na yote hayo wananchi wameridhika na ccm huwaambii kitu juu ya CCM yao.
Huku mgombea akishapitishwa na CCM basi yeye ndiye mshindi kwa asilimia 90. Haijawahi pata kiongozi wa upinzani ingawa mwaka 2005 - 2010 tulikuwa na diwani mmoja tu wa chadema kata ya kibungo juu.

Wananchi tumeamua kujisemea wenyewebkwa kuwa masikini wachache na wajinga wachache wanatuumiza sisi kwa kuendelea kuichagua ccm.
 
Kamanda ni kweli mi mwenyewe nipo huku kikazi shule ya sekondari kibungo juu. Watu wa huku huwaambii kitu kwa ccm.
Upo sehemu gani kamanda Tawa tutafutane kaka

Npo matombo kamanda ndipo familia yangu ilipo japo mimi nafanya kazi eneo lingine. Kila wikiend nipo huku. Njoo hapa matombo kaka tuongee vizuri kama utapata nafasi
 
Mkuu, poleni sana. Hiyo ndiyo hali halisi ya CCM

Hivi hiyo wilaya iko pande zipi hapo Morogoro?

Na kuhusu kujisemea wenyewe, inaelekea mpo wachache sana mnaojisemea wenyewe. Inaelekea walio wengi wameridhika na maisha hayo, vinginevyo wasingeing'ang'ania CCM kila mwaka.

Wakipata akili watafikiri.
 
Hivi lami ya Matombo imebanduliwa?
 
Hivi lami ya Matombo imebanduliwa?

Matombo hakujawahi kuwekwa lami. Kama hujui maeneo ya watu acha kuropoka. We kaa kwenu huko singida ambako mkidanganywa na molamu na kuambiwa lami mnakubali.
 
msitegee elimu ikafika hapo mtapoteza mtaji wa kura za ccm! Hyo wilaya ni aina mpwapwa usitegemee kabisa huduma za Jamii!
 
Mkuu, poleni sana. Hiyo ndiyo hali halisi ya CCM

Hivi hiyo wilaya iko pande zipi hapo Morogoro?

Na kuhusu kujisemea wenyewe, inaelekea mpo wachache sana mnaojisemea wenyewe. Inaelekea walio wengi wameridhika na maisha hayo, vinginevyo wasingeing'ang'ania CCM kila mwaka.

Wakipata akili watafikiri.

Sisi waluguru ni watu wa ajabu sana, huwa hatuelewi na ni wavivu kufikiri
 
Miaka yote huwa wanaweka molam msitu wa kibungo ili mbunge na kikwete akiwa anaenda kwa mganga wake kolelo wasitekwe lakini hakuna hata changalawe iliyowahi kuwekwa huku.

Achana nae mjinga huyu sijui kala maharagwe ya wapi huyu.
 
Npo matombo kamanda ndipo familia yangu ilipo japo mimi nafanya kazi eneo lingine. Kila wikiend nipo huku. Njoo hapa matombo kaka tuongee vizuri kama utapata nafasi

hiyo sehemu mbona waliita hivyo?
 
Kama kashindwa Lowasaa sisi ni nani kaka?

nililojifunza morogoro, ni kuwa uwajibikaji haupo, ile hali ya kuwa na wivu wa maendeleo haipo, ninayadhuhudia hayo kwenye sekta fulani ninayowajibika kama mtumishi wa umma, ushindani wa kuleta mafanikio katika jasmii haupo, ni jasmii pekee inayosubiri kusema asante kwa wanachopewa na wahisani,
 
Kaka yawezekana ya huko morogoro kusini ni 9 kumi nenda wilaya ya Ileje mkoani mbeya kamanda. Yaani nadhani ni mojawapo ya wilaya fukara kabisa hapa nchini.

Kule huwaambii chochote kuhusu ccm yaani 2010 kulikua na diwani mmoja tu wa CHADEMA kata ya chitete Hali kadhalika hata mwaka huu ni mmoja tu toka kata hiyo hiyo. Kuna vijiji ukitaka kwenda toka mbeya mjini unatumia cku 2 kutokana na miundo mbinu mibovu.

Mfano ni kule ikinga na vijiji kama bwenda. Umeme ndo usiseme kati ya vijiji zaidi ya 80 vyenye umeme si zaidi ya vitano. Vijiji kama Itale, shuba, katengere, bufura, Ilanga nk ccm imeota mizizi lakini umasikini ni wa kutisha. Wilaya nzima sidhani kama Kuna hata mwenye PhD kule. Ccm kutoka madarakani kule ni ndoto za rinacha
 
Matombo hakujawahi kuwekwa lami. Kama hujui maeneo ya watu acha kuropoka. We kaa kwenu huko singida ambako mkidanganywa na molamu na kuambiwa lami mnakubali.


Nafikiri anaongelea molam ya kibungo na chamanyani sijui...

hivi dutumi...mvuha...kisaki ipo jimbo hilo au tofauti?
 
Kaka yawezekana ya huko morogoro kusini ni 9 kumi nenda wilaya ya Ileje mkoani mbeya kamanda. Yaani nadhani ni mojawapo ya wilaya fukara kabisa hapa nchini. Kule huwaambii chochote kuhusu ccm yaani 2010 kulikua na diwani mmoja tu wa CHADEMA kata ya chitete Hali kadhalika hata mwaka huu ni mmoja tu toka kata hiyo hiyo. Kuna vijiji ukitaka kwenda toka mbeya mjini unatumia cku 2 kutokana na miundo mbinu mibovu. Mfano ni kule ikinga na vijiji kama bwenda. Umeme ndo usiseme kati ya vijiji zaidi ya 80 vyenye umeme si zaidi ya vitano. Vijiji kama Itale, shuba, katengere, bufura, Ilanga nk ccm imeota mizizi lakini umasikini ni wa kutisha. Wilaya nzima sidhani kama Kuna hata mwenye PhD kule. Ccm kutoka madarakani kule ni ndoto za rinacha

ohooo,mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa watanzania hasa wa vijijini,jeshi la polisi,na NEC,lakini ukiondoa hivi viwili vya mwisho nafikiri itakuwa afadhali.ila sidhani
 
TAWA

Ninapajua huko Matombo....kule kuna umaskini wakutisha ndugu zanguni.

Maeneo ya milawilila,kisemu,Tawa,kibangile ni shida za kufa mtu. Hawajawahi kuona hata km 1 ya Lami. Miaka ya 2000 kulikuwa na mbunge Hamza Mwenegoha,alikuwa akigawa mipira tu kwa vijana lakini hajihusishi na maendeleo ya watu wa Morogoro kusini.

Mbunge akiwapa mipira ya buku nane nane kamaliza kazi.

Nakumbuka alikuwa akidhamini ligi ndogo ndogo tu kwa kila miaka mitano tu....kulikuwa na timu km mtamba stars na n.k zikishiriki ligi zake.

Ukiwa mwenyeji wa Morogoro kusini basi jinyonge tu maana mpaka mje kufanana na sehemu kama Marangu Mashariki ni miaka 100 ijayo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom