Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
tumekwisha kusikia kilio chenu , ukombozi uko njiani .Ipo karibu kivipi kaka!? Unakujua sehemu yenyewe au unasikia tu. Haya, karibuni mtupe faraja.
very sad we have to prayKwa mbunge huyo huyo wa ccm!? Kulikuwa na mbunge mmoja wa ccm alishapita alikuwa anaitwa Hamza Mwenegoha alishawahi kuwa naibu waziri wa ujenzi kwa miaka saba lakini jimbo lake wala wilaya nzima hakuna lami.
Huyu mbunge wa sasa.alikuwa katibu wa rais alifanya nini wakati anaitumikia Ikulu ya Tanzania kabla hajawa mbunge
Ccm mbere kwa mbereWilaya hii makao makuu yake yapo moro mjini kwa kuwa watendaji wengi wa wilaya hii wanakwepa maisha ya dhiki yasiyo stahili kuishi binadamu ndani ya wilaya.
ELIMU:
-Wilaya ya Morogoro hakuna hata shule moja ya Advance level (kidato cha tano na sita).
-Shule za msingi zilizopo ni duni chakavu tena zilizochoka.
-Hakuna walimu wa kutosha. Kuna shule kama shile ya msingi kitengu, lumba chini na lumba juu kuna mwalimu mmoja mmoja kila shule.
Mbunge ni wa ccm.
AFYA:
Wilaya hii hakuna hospital yenye hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Kuna kituo cha afya cha tawa eti ndo wanataka kuifanya hospital ya wilaya. Kiukweli haina hadhi, kama ingekuwa Dar hii ingekuwa zahanati.
Mbunge ni wa ccm.
BARABARA:
Unaweza ukafikiri kama nafanya uchochezi au masihara ila ukweli ni kwamba HAKUNA HATA MITA MOJA ya kipande cha lami. Barabara huku kwetu ni za vumbi zilizojaa makorongo zinazohatarisha safari.
Mbunge ni wa ccm.
UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.
Lakini pamoja na yote hayo wananchi wameridhika na ccm huwaambii kitu juu ya CCM yao.
Huku mgombea akishapitishwa na CCM basi yeye ndiye mshindi kwa asilimia 90. Haijawahi pata kiongozi wa upinzani ingawa mwaka 2005 - 2010 tulikuwa na diwani mmoja tu wa chadema kata ya kibungo juu.
Wananchi tumeamua kujisemea wenyewebkwa kuwa masikini wachache na wajinga wachache wanatuumiza sisi kwa kuendelea kuichagua ccm.
Wabunge woote wa ccm wana sifa hiziTAWA
Ninapajua huko Matombo....kule kuna umaskini wakutisha ndugu zanguni.
Maeneo ya milawilila,kisemu,Tawa,kibangile ni shida za kufa mtu. Hawajawahi kuona hata km 1 ya Lami. Miaka ya 2000 kulikuwa na mbunge Hamza Mwenegoha,alikuwa akigawa mipira tu kwa vijana lakini hajihusishi na maendeleo ya watu wa Morogoro kusini.
Mbunge akiwapa mipira ya buku nane nane kamaliza kazi.
Nakumbuka alikuwa akidhamini ligi ndogo ndogo tu kwa kila miaka mitano tu....kulikuwa na timu km mtamba stars na n.k zikishiriki ligi zake.
Ukiwa mwenyeji wa Morogoro kusini basi jinyonge tu maana mpaka mje kufanana na sehemu kama Marangu Mashariki ni miaka 100 ijayo
🤣🤣🤣ohooo,mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa watanzania hasa wa vijijini,jeshi la polisi,na NEC,lakini ukiondoa hivi viwili vya mwisho nafikiri itakuwa afadhali.ila sidhani
DuuhKamanda ni kweli mi mwenyewe nipo huku kikazi shule ya sekondari kibungo juu. Watu wa huku huwaambii kitu kwa ccm.
Upo sehemu gani kamanda Tawa tutafutane kaka
🤣🤣🤣duuhKaka yawezekana ya huko morogoro kusini ni 9 kumi nenda wilaya ya Ileje mkoani mbeya kamanda. Yaani nadhani ni mojawapo ya wilaya fukara kabisa hapa nchini.
Npo matombo kamanda ndipo familia yangu ilipo japo mimi nafanya kazi eneo lingine. Kila wikiend nipo huku. Njoo hapa matombo kaka tuongee vizuri kama utapata nafasi
Kuwa makiniNpo matombo kamanda ndipo familia yangu ilipo japo mimi nafanya kazi eneo lingine. Kila wikiend nipo huku. Njoo hapa matombo kaka tuongee vizuri kama utapata nafasi