Morogoro Kusini, Wilaya masikini kuliko zote Tanzania

Morogoro Kusini, Wilaya masikini kuliko zote Tanzania

Sipati picha ya Wilaya mpya ya Malinyi huko Ulanga Magharibi.Hali ni tete kuliko hii Morogoro Kusini mnayoizungumzia.Mbaya zaidi CCM ni kama imeota mizizi maana asilimia kubwa ya Wananchi wa huko hawaoni kama CCM ndio kikwazo cha maendeleo yao.
 
Nakubaliana na wewe ndugu, barabara zenu ni mbaya sana. Nimefika Mvuha mara ya kwanza mwaka huu, kwa kweli malalamiko yako ni genuine kabisa. Kesho pia naenda kijiji cha Kongwa, kule karibu na mbuga ya Selous, huko tunapita kwenye miti tu ili kufika kijijini, kwa sababu hakuna barabaya ya gari ya kueleweka ili kufika kijijini Kongwa. Kuna mradi nautekeleza kule, wa kuwapekelea umeme watu wa kijiji cha Kongwa. Ilituwia vigumu sana kupeleka mitambo wakati wa mvua, kwa kuwa njia hazipitiki kirahisi kabisa. Poleni sana

Kongwa ipo kata ya mvuha imepakana na kata ya selembala. Karibu moro (v) tusemayo yapo hatutanii
 
Sipati picha ya Wilaya mpya ya Malinyi huko Ulanga Magharibi.Hali ni tete kuliko hii Morogoro Kusini mnayoizungumzia.Mbaya zaidi CCM ni kama imeota mizizi maana asilimia kubwa ya Wananchi wa huko hawaoni kama CCM ndio kikwazo cha maendeleo yao.

Hahaaa. Nilitembelea Malinyi mwanzoni mwa mwaka huu yaani ni shida. Barabara ni mbovu na matukio ya utekaji wa magari kwenye pori la Nambiga yalikuwa yameshamili. Ni eneo ambalo limeongozwa na kiongozi mzito wa serikali ndugu Ngasongwa kwa muda mrefu. Sasa hivi yupo ndugu Haji Mponda kwa awamu ya pili sasa. Ni eneo muhimu sana kwa uzalishaji wa mpunga na kwasasa kunafanyika tafiti za mafuta na gesi kwenye Bonde hilo lakini bado ni eneo lenye miundombinu mibovu kabisa.
 
Wakuu hiyo ndo hali ilioko ngome zote za mafisiem, Naomba anaeweza kuielezea hali ya wilaya za mkoa wa dodoma anisaidie, nmesoma chuo flani pale kwakweli ule mkoa unanuka umaskini kutokea pande zote Kus, Kaskaz, Mashar na Magharibi. Mungu awafunulie nuru kwakweli Wagogo wanatia huruma!
 
Pole kwa watanzania wote. Ila vp kwa maeneo ya Iringa?
Hali ikoje...hiyo ya Ileje kuna rafiki yangu aliacha kazi ya serikali baada ya kukaa mwezi mmoja tu kule...
Walioenda Tandahimba , Simiyu wanakubali mazingira ni poa.
 
Mkuu afadhali ileje hata lami ipo, huku hakuna hata hatua moja ya lami
 
Kuna Wakati nilipita huko nikifanya utafit kwenye elimu shule za msingi,nikafika mziha mngazi mpaka lumba chin na juu-vp yule mama wanamuita bibi bado yupo? nilisikia habari zake ilikuwa 2009 nilipopita huko !
 
tatizo utaliona liko wapi tatizo liko kwetu sisi waTZ hatujitambui uwelewa mbo tulio wengi tunajua kwamba umaskini na shida zetu ni mipango ya Mungu kwamba haisababishwi na watu
 
Kongwa ipo kata ya mvuha imepakana na kata ya selembala. Karibu moro (v) tusemayo yapo hatutanii

Ni kweli Mkuu. Nimetoka huko leo, nilienda Mara moja. Nimerudi Moro mjini, niliingilia njia ya mikese mizani hadI mbuyuni.
 
Hahaaa. Nilitembelea Malinyi mwanzoni mwa mwaka huu yaani ni shida. Barabara ni mbovu na matukio ya utekaji wa magari kwenye pori la Nambiga yalikuwa yameshamili. Ni eneo ambalo limeongozwa na kiongozi mzito wa serikali ndugu Ngasongwa kwa muda mrefu. Sasa hivi yupo ndugu Haji Mponda kwa awamu ya pili sasa. Ni eneo muhimu sana kwa uzalishaji wa mpunga na kwasasa kunafanyika tafiti za mafuta na gesi kwenye Bonde hilo lakini bado ni eneo lenye miundombinu mibovu kabisa.

Nilikua huko wiki jana, hali ni mbaya. Nilikua kikazi kijiji cha Biro, kwa akina Dr. Juma Ngasongwa na Joti muigizaji. Sina la kusema
 
Mbona bora hata Moro huku kwetu songea na maeneo mengine tuna shida zaidi ya hizo. Kuna kta kama ya Mkongo watu wanachota maji tena machafu lakin wao ccm kwao ndo baba na mama yao wanasema wao wanachotaka in amani uliwauliza je wanaridhika na Hatari ya maji wanayokunywa wanasema wanchukizwa mno ila wao wameshazoea kwa kweli ni hatri sana.
 
tunaweza laumu mpka kesho ila wenzetu wamefanywa asset.. ndo hao wanaojaza kura za wagombea wao.. huoni ni sehemu nyingi za mijini kuna upinzani. by the way dodoma kuna lami tatu. mkoa mzima lami ya kwenda iringa. kwenda moro na kwenda singida. na zile za pale dodoma mjini. Asante
 
Hiyo chorus yako "mbunge wa ccm" nimekipenda inaonesha ww mshairi mzuri sana.
 
Wilaya hii makao makuu yake yapo moro mjini kwa kuwa watendaji wengi wa wilaya hii wanakwepa maisha ya dhiki yasiyo stahili kuishi binadamu ndani ya wilaya.

ELIMU:
-Wilaya ya Morogoro hakuna hata shule moja ya Advance level (kidato cha tano na sita).
-Shule za msingi zilizopo ni duni chakavu tena zilizochoka.
-Hakuna walimu wa kutosha. Kuna shule kama shile ya msingi kitengu, lumba chini na lumba juu kuna mwalimu mmoja mmoja kila shule.
Mbunge ni wa ccm.

AFYA:

Wilaya hii hakuna hospital yenye hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Kuna kituo cha afya cha tawa eti ndo wanataka kuifanya hospital ya wilaya. Kiukweli haina hadhi, kama ingekuwa Dar hii ingekuwa zahanati.
Mbunge ni wa ccm.

BARABARA:
Unaweza ukafikiri kama nafanya uchochezi au masihara ila ukweli ni kwamba HAKUNA HATA MITA MOJA ya kipande cha lami. Barabara huku kwetu ni za vumbi zilizojaa makorongo zinazohatarisha safari.
Mbunge ni wa ccm.

UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.

Lakini pamoja na yote hayo wananchi wameridhika na ccm huwaambii kitu juu ya CCM yao.
Huku mgombea akishapitishwa na CCM basi yeye ndiye mshindi kwa asilimia 90. Haijawahi pata kiongozi wa upinzani ingawa mwaka 2005 - 2010 tulikuwa na diwani mmoja tu wa chadema kata ya kibungo juu.

Wananchi tumeamua kujisemea wenyewebkwa kuwa masikini wachache na wajinga wachache wanatuumiza sisi kwa kuendelea kuichagua ccm.
Hiyo chorus yako ya "mbunge wa ccm" mi hoi.
 
Back
Top Bottom