Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukitaka kujua umasikini upo Tanzania sogelea eneo hiloNilikuwa kibungo kitongoji cha Mwalazi kwenye mgodi wa Wasrilanka asee waluguru wa kule na elimu bado sana. Yani kuanzia wazazi hadi walimu na wanafunzi wao wanaenda mto ruvu kuchimba dhahabu, vinyumba kama mabanda ya bata, wao na pombe.
Mabadiliko yanakuja
Heko kamanda kwa kuliona hili. Yaani uliyoyaona Morogoro kusini ni afadhali kwa kulinganisha na Bukoba Vijijini. CV ya Morogoro kusini ndo hiyo hiyo kwa Bukoba vijijini jimbo lenye kata 29 na ccm imekuwepo tangu enzi mpaka leo. Hakuna hospitali, shule ndo hivyo tena, barabara kama ulivyosema kwa morogoro. Ofisi zake ziko manispaa ya Bukoba. ila kilichoko huko ni gereza la Rwamulumba na ccm. Adios
Shida ya sisi watanzania ni kujifanya kujua kila kitu. Hali iliyopo huku ni kama kila kaya na si kata kulipia shilingi 1000 kwa huduma ya mto au kijito kilichopo kwa kampuni hiyo tajwa hapo wakati utunzaji wenyewe unafanywa na wananchi wenyewe kwa hiyo hilo ni dili la kupiga hela za wanyonge. Usikurupuke kutukana watu pasi kujua mantiki ya jambo ubabe kamletee mkeo na watoto wako hii jf home of great thinkers bwe.ge we.
mkuu soma alichoandika mleta mada hapa chini halau angalia nilichojibu then jipime kati yangu na wewe nani BWE'GE.
(UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.)
mkuu soma alichoandika mleta mada hapa chini halau angalia nilichojibu then jipime kati yangu na wewe nani BWE'GE.
(UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.)
Na bumbuli kwa makamba mkuuTakwimu za NEC zinaonesha hilo pia ndio jimbo pekee lililoharibu kura NYINGI kuliko majimbo yote Tanzania.
Kwa kuongezea tu ni kwamba jimbo liliharibu kura chache kushinda yote ni kilindi Tanga.
Nasikia eti ndo atakuwa PM huyo mbunge wa huku kwetuMbunge wa huku ni Prosper Joseph Mbena. Ana kazi kubwa sana
Kaka yawezekana ya huko morogoro kusini ni 9 kumi nenda wilaya ya Ileje mkoani mbeya kamanda. Yaani nadhani ni mojawapo ya wilaya fukara kabisa hapa nchini.
Kule huwaambii chochote kuhusu ccm yaani 2010 kulikua na diwani mmoja tu wa CHADEMA kata ya chitete Hali kadhalika hata mwaka huu ni mmoja tu toka kata hiyo hiyo. Kuna vijiji ukitaka kwenda toka mbeya mjini unatumia cku 2 kutokana na miundo mbinu mibovu.
Mfano ni kule ikinga na vijiji kama bwenda. Umeme ndo usiseme kati ya vijiji zaidi ya 80 vyenye umeme si zaidi ya vitano. Vijiji kama Itale, shuba, katengere, bufura, Ilanga nk ccm imeota mizizi lakini umasikini ni wa kutisha. Wilaya nzima sidhani kama Kuna hata mwenye PhD kule. Ccm kutoka madarakani kule ni ndoto za rinacha
Nmefanya kazi kituo cha afya mvuha, kisha dutumi. Ingawa kwa sasa nimehama wilaya hii kikazi ingawa bado naishi huku na familia yangu. Huku hali ni mbaya sana janani
Mkuyuni kwetu, daaah ile barabara inakera Sana yani