Inasikitisha,lazima wagonge 100.
Kutokana na hao waliobaki hali zao ni mbaya.kwanini lazima mia
Pole sana kwa droo jana.Kutokana na hao waliobaki hali zao ni mbaya.
Ndo mpira,ila siyo mbaya ukizingatia season iliyopita hawa jamaa walitufunga.Pole sana kwa droo jana.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji109][emoji123]Mawazo mazuri wizara husika walifanyie kazi....
Bado ninaamini hospital za Moro na Tumbi zingekuwa vizuri tungeweza kuokoa roho nyingi si kwenye ajali hii tu ya moto bali kwenye ajali zinazotokea kila siku kwenye hii barabaraIla Mshana ukiungua kwanzia asilimia 60 kupona ni nadra matarijio ni kidogo sasa hawa wameungua asilimia 70 mpaka 80 ukiangalia hapo kupona ni sawa na uongo kuwa kweli hatuwezi kulaumu serikali why wamekufa hili hali kwa asilimia hizo ni ngumu kupona cha msingi kama ulivyo sema hospital ya tumbi iangaliwe kwa jicho la huruma
POLITIK maybe or most likely...!!!Yasipofanyiwa haya kazi ni nini kiyafanyiwa kazi?
Moderator on duty... Tafadhali punguza kukurupuka... Soma maudhui uyaelewe kabla hujaamua kuchukua maamuziNi habari za kusikitisha na kukatisha tamaa sana... Majeruhi 47 wa ajali ya moto Moro wamebakia 15 tuu... Wengine wote 32 wamefariki dunia
Tuweke siasa kando na kuhoji kwa weledi... Kipaumbele chetu kwenye afya kina walakini mkubwa... Barabara ya Morogoro inajulikana kwa matukio yake ya ajali lakini hospital kubwa iliyoko Tumbi wilayani Kibaha inapumulia mashine
Ni kama vile hatujajiandaa kwa majanga makubwa makubwa.... Kitengo cha dharura pale Tumbi kinatisha, kinasikitisha, kinakatisha tamaa, kiko hoi huku vitendea kazi vikiwa duni kabisa na kwa sehemu kubwa kikihudumiwa na wanafunzi wa udaktari na unesi
Tuna hospital la maana sana pale Mloganzila... Lililosheni kila aina ya vifaa.. Linavutia kwakweli... Ni msaada wa watu wa jamhuri ya Korea... Ukifika pale kidogo unaweza kupata moyo wa kupona... Lakini napo tatizo linabaki pale pale... Wataalam! Sehemu kubwa ni wanafunzi wa udaktari... Lakini mbaya zaidi ni uongozi
Pamoja na kuwa Tumbi ni hospital ya rufaa kama ilivyo Mloganzila ambayo ni auxiliary ya Muhimbili... Lakini majeruhi wote 47 walipitishwa wima... Wakazipita hospital zote hizi mbili zilizo karibu na eneo la ajali wakaenda kulundikwa wote Muhimbili iliyo busy kupita maelezo
Cha kushangaza zaidi siku ya pili baada ya ajali majeruhi wengine waliokuwa Hospital ya Moro wakahamishiwa Muhimbili kwa tukio maalum lililoandaliwa... Wakasafirishwa kwa helicopter na kupokewa jangwani
Kwa umuhimu huu wa barabara ya Morogoro, uwingi wa watu na magari... Kumbuka sehemu kubwa ya nchi kwa upande wa kaskazini hii ndio barabara pekee ya kutoka na kuingia mpaka nchi nyingi za jirani na zaidi... Hospitali hizi tatu Mloganzila, Tumbi na Morogoro zilipaswa zipewe kipaumbele na kufanywa kama hospital mkakati za kanda maalum
Nina hakika hili likifanyika tutaokoa vifo vingi sana
Inasikitisha sana waziri anafika hospitali kubwa kama Tumbi na msafara wa ma V8 ambayo thamani yake ni zaidi ya billion moja. Anaenda kutembelea hospitali iliyo mahututi kwenye kitengo cha dharura, mochwari isiyo na uwezo wa kubeba miili 20, hospitali isiyo na dawa na vifaa tiba vya kutosha nknk... Anafika hapo anapiga blah blah anarekodiwa na makamera kisha anasepa
Tunapojenga libarabara kubwa la njia nane linaloishia Kibaha basi tusiisahau na hospitali hii muhimu sana ya Tumbi ili kupunguza mrundikano Muhimbili
Mkuu badili tittle na uutupie tena, mode wanazingua sometymeModerator on duty... Tafadhali punguza kukurupuka... Soma maudhui uyaelewe kabla hujaamua kuchukua maamuzi
Nina hakika ungesoma hiki nilichoandika usingechukua uamuzi wa kuunganisha huu uzi... Wewe umesoma heading tu ukaona inafaa kuunganishwa huku... Mnaiangusha JF
Mkuu naunga mkono hoja.Ni habari za kusikitisha na kukatisha tamaa sana... Majeruhi 47 wa ajali ya moto Moro wamebakia 15 tuu... Wengine wote 32 wamefariki dunia
Tuweke siasa kando na kuhoji kwa weledi... Kipaumbele chetu kwenye afya kina walakini mkubwa... Barabara ya Morogoro inajulikana kwa matukio yake ya ajali lakini hospital kubwa iliyoko Tumbi wilayani Kibaha inapumulia mashine
Ni kama vile hatujajiandaa kwa majanga makubwa makubwa.... Kitengo cha dharura pale Tumbi kinatisha, kinasikitisha, kinakatisha tamaa, kiko hoi huku vitendea kazi vikiwa duni kabisa na kwa sehemu kubwa kikihudumiwa na wanafunzi wa udaktari na unesi
Tuna hospital la maana sana pale Mloganzila... Lililosheni kila aina ya vifaa.. Linavutia kwakweli... Ni msaada wa watu wa jamhuri ya Korea... Ukifika pale kidogo unaweza kupata moyo wa kupona... Lakini napo tatizo linabaki pale pale... Wataalam! Sehemu kubwa ni wanafunzi wa udaktari... Lakini mbaya zaidi ni uongozi
Pamoja na kuwa Tumbi ni hospital ya rufaa kama ilivyo Mloganzila ambayo ni auxiliary ya Muhimbili... Lakini majeruhi wote 47 walipitishwa wima... Wakazipita hospital zote hizi mbili zilizo karibu na eneo la ajali wakaenda kulundikwa wote Muhimbili iliyo busy kupita maelezo
Cha kushangaza zaidi siku ya pili baada ya ajali majeruhi wengine waliokuwa Hospital ya Moro wakahamishiwa Muhimbili kwa tukio maalum lililoandaliwa... Wakasafirishwa kwa helicopter na kupokewa jangwani
Kwa umuhimu huu wa barabara ya Morogoro, uwingi wa watu na magari... Kumbuka sehemu kubwa ya nchi kwa upande wa kaskazini hii ndio barabara pekee ya kutoka na kuingia mpaka nchi nyingi za jirani na zaidi... Hospitali hizi tatu Mloganzila, Tumbi na Morogoro zilipaswa zipewe kipaumbele na kufanywa kama hospital mkakati za kanda maalum
Nina hakika hili likifanyika tutaokoa vifo vingi sana
Inasikitisha sana waziri anafika hospitali kubwa kama Tumbi na msafara wa ma V8 ambayo thamani yake ni zaidi ya billion moja. Anaenda kutembelea hospitali iliyo mahututi kwenye kitengo cha dharura, mochwari isiyo na uwezo wa kubeba miili 20, hospitali isiyo na dawa na vifaa tiba vya kutosha nknk... Anafika hapo anapiga blah blah anarekodiwa na makamera kisha anasepa
Tunapojenga libarabara kubwa la njia nane linaloishia Kibaha basi tusiisahau na hospitali hii muhimu sana ya Tumbi ili kupunguza mrundikano Muhimbili
Ajali imetokea eneo la Mzambarauni (Nje kidogo ya Mji wa Morogoro). Inadaiwa kuwa waendesha Bodaboda waliojaribu kuchota mafuta wameteketea ktk moto huo
> Mpaka sasa chanzo cha Lori hilo kupinduka na hatimaye kushika bado haijafahamika
Update: 1205hrs
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Rita Lyamuya amesema wamepokea miili 60 na majeruhi 60:
"Tunavyoongea sasa hivi tumeshapokea majeruhi 60, bado tunaendelea kupokea. Kati ya hao walio ndani ya ward wanaume ni 58 na wanawake ni wawili…na pia tumepokea miili 60."
Hali ilivyokuwa kabla ya moto kulipuka
Update: 1400hrs
Polisi Morogoro imesema idadi ya watu waliokufa imefikia 62 na majeruhi 72.
Majeruhi 39 wamekimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili.
View attachment 1177837
======
Morogoro. “Inasikitisha”. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Agosti 10, 2019 ambapo Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia miili iliyoungua ikiwa imelazwa pembeni ya barabara ya Dar es Salaam-Morogoro wengi wakiwa ni madereva bodaboda na mamalishe wanaofanya shughuli zao hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi.
Ajali hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.
Baadhi ya mashuhuda wamelieleza Mwananchi kuwa baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kuchota mafuta hayo.
Wamesema mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alikuwa akivuta sigara, kwamba ndio chanzo cha mlipuko huo.
======
UPDATES: 11 August 2019
Morogoro/Dar. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameungana na viongozi wengine wa vyama na Serikali mkoani Morogoro kwenye msiba wa kitaifa baada ya kutokea ajali ya moto iliyoua Watanzania 68 hadi leo Jumapili Agosti 11, 2019 saa 3 asubuhi.
Kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema idadi hiyo imeongezeka kutoka vifo 64 vilivyoripotiwa hadi jana saa 10 jioni hadi vifo 68.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika kijiji cha Itigi, Msamvu mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.
Picha za video zinaonyesha lori hilo likiwa limepinduka barabarani na mafuta yakichuruzika kuelekea pembeni mwa barabara ya Morogoro- Dar es Salaam ambako watu waliokuwa na madumu ya ujazo mbalimbali walikuwa wakichota mafuta kabla ya moto kuwaka.
Mbali na Majaliwa, viongozi wengine waliomiminika mkoani humo ni Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Sera, Bunge,Ajira, Kazi,Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama; Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe; mganga mkuu wa Serikali ya Tanzania, Profesa Mohamed Kambi.
UPDATES: 1120hrs
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema kati ya majeruhi 46 walioletwa hospitali hiyo wawili wamefariki dunia.
UPDATES:1130hrs
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa anaunda tume itakayoanza kufanya kazi leo Agosti 11 kubaini kama kuna mamlaka serikalini zilishindwa kuwajibika mara baada ya lori la mafuta kupata ajali na hatimae kusababisha mlipuko uliogharimu maisha ya watu zaidi ya 60.
UPDATES: 14 AUG 2019
Idadi ya watu ambao wamefariki kutokana na mkasa wa ajali ya mlipuko wa lori la mafuta mjini Morogoro imeongezeka hadi 82
UPDATES: 2130hrs
Majeruhi wengine watatu ajali ya lori la mafuta Morogoro, waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wafariki dunia. Waliofariki hadi sasa wamefika 85
UPDATE: 15 AUG 2019
Majeruhi wengine 7 kati ya 32 waliosafirishwa kutoka Morogoro na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi kufariki dunia. Idadi ya vifo yafikia 89
UPDATES:0900HRS 17 AUG 2019
Idadi ya waliokufa kutokana na ajali ya moto iliyotokea Morogoro Agosti, 10 imefikia 93 baada ya majeruhi wengine wanne kufariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili
UPDATES: 1800HRS 18 AUG 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI MOROGORO YAFIKIA 95
- Ni baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufariki jana usiku
- Wagonjwa 20 wa ajali hiyo waliobaki katika hospitali hiyo wamelazwa katika chumba cha uangaliazi maalum
UPDATES: 1140HRS 19 AUG 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YAFIKIA 97
Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kuwaka moto Morogoro imeongezeka na kufikia 97 baada ya majeruhi wengine wawili kufariki leo.
UPDATES:2200HRS 20 AUG
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YAFIKIA 99
Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali yalori la mafuta yaongezeka na kufikia 99
UPDATES:0940HRS 21 AUG 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YAFIKIA 100
Vifo vilivyotokana na ajali ya moto baada ya lori la mafuta kulipuka imeongezeka na kufikia 100