Ajali imetokea eneo la Mzambarauni (Nje kidogo ya Mji wa Morogoro). Inadaiwa kuwa waendesha Bodaboda waliojaribu kuchota mafuta wameteketea ktk moto huo
Mpaka sasa chanzo cha Lori hilo kupinduka na hatimaye kushika bado haijafahamika
Update: 1205hrs
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Rita Lyamuya amesema wamepokea miili 60 na majeruhi 60:
"Tunavyoongea sasa hivi tumeshapokea majeruhi 60, bado tunaendelea kupokea. Kati ya hao walio ndani ya ward wanaume ni 58 na wanawake ni wawili…na pia tumepokea miili 60."
Hali ilivyokuwa kabla ya moto kulipuka
Update: 1400hrs
Polisi Morogoro imesema idadi ya watu waliokufa imefikia 62 na majeruhi 72.
Majeruhi 39 wamekimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili.
View attachment 1177837
======
Morogoro. “Inasikitisha”. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Agosti 10, 2019 ambapo Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia miili iliyoungua ikiwa imelazwa pembeni ya barabara ya Dar es Salaam-Morogoro wengi wakiwa ni madereva bodaboda na mamalishe wanaofanya shughuli zao hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi.
Ajali hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.
Baadhi ya mashuhuda wamelieleza Mwananchi kuwa baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kuchota mafuta hayo.
Wamesema mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alikuwa akivuta sigara, kwamba ndio chanzo cha mlipuko huo.
======
UPDATES: 11 August 2019
Morogoro/Dar. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameungana na viongozi wengine wa vyama na Serikali mkoani Morogoro kwenye msiba wa kitaifa baada ya kutokea ajali ya moto iliyoua Watanzania 68 hadi leo Jumapili Agosti 11, 2019 saa 3 asubuhi.
Kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema idadi hiyo imeongezeka kutoka vifo 64 vilivyoripotiwa hadi jana saa 10 jioni hadi vifo 68.
Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika kijiji cha Itigi, Msamvu mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.
Picha za video zinaonyesha lori hilo likiwa limepinduka barabarani na mafuta yakichuruzika kuelekea pembeni mwa barabara ya Morogoro- Dar es Salaam ambako watu waliokuwa na madumu ya ujazo mbalimbali walikuwa wakichota mafuta kabla ya moto kuwaka.
Mbali na Majaliwa, viongozi wengine waliomiminika mkoani humo ni Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Sera, Bunge,Ajira, Kazi,Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama; Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe; mganga mkuu wa Serikali ya Tanzania, Profesa Mohamed Kambi.
UPDATES: 1120hrs
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema kati ya majeruhi 46 walioletwa hospitali hiyo wawili wamefariki dunia.
UPDATES:1130hrs
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa anaunda tume itakayoanza kufanya kazi leo Agosti 11 kubaini kama kuna mamlaka serikalini zilishindwa kuwajibika mara baada ya lori la mafuta kupata ajali na hatimae kusababisha mlipuko uliogharimu maisha ya watu zaidi ya 60.
UPDATES: 14 AUG 2019
Idadi ya watu ambao wamefariki kutokana na mkasa wa ajali ya mlipuko wa lori la mafuta mjini Morogoro imeongezeka hadi 82
UPDATES: 2130hrs
Majeruhi wengine watatu ajali ya lori la mafuta Morogoro, waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wafariki dunia. Waliofariki hadi sasa wamefika 85
UPDATE: 15 AUG 2019
Majeruhi wengine 7 kati ya 32 waliosafirishwa kutoka Morogoro na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi kufariki dunia. Idadi ya vifo yafikia 89
UPDATES:0900HRS 17 AUG 2019
Idadi ya waliokufa kutokana na ajali ya moto iliyotokea Morogoro Agosti, 10 imefikia 93 baada ya majeruhi wengine wanne kufariki dunia Hospitali ya Taifa Muhimbili
UPDATES: 1800HRS 18 AUG 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI MOROGORO YAFIKIA 95
- Ni baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kufariki jana usiku
- Wagonjwa 20 wa ajali hiyo waliobaki katika hospitali hiyo wamelazwa katika chumba cha uangaliazi maalum
UPDATES: 1140HRS 19 AUG 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YAFIKIA 97
Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kuwaka moto Morogoro imeongezeka na kufikia 97 baada ya majeruhi wengine wawili kufariki leo.
UPDATES:2200HRS 20 AUG
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YAFIKIA 99
Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali yalori la mafuta yaongezeka na kufikia 99
UPDATES:0940HRS 21 AUG 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YAFIKIA 100
Vifo vilivyotokana na ajali ya moto baada ya lori la mafuta kulipuka imeongezeka na kufikia 100
UPDATE: 1200HRS AUG 23 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YAFIKIA 101
Ni baada ya majeruhi mmoja kufariki dunia alfajiri ya leo Ijumaa Agosti 23, na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 101
UPDATE: SEPTEMBER 1, 2019
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO MOROGORO YAFIKIA 104
Ni baada ya majeruhi 2 kati ya 13 waliokuwa wamelazwa ktk Hospitali ya Taifa Muhimbili, kufariki