G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Mwenyekiti wa timu ya kampeni ya Mgombea ubunge wa Morogoro mjini kwa tiketi ya CHADEMA na dereva wa mgombea Ubunge wa Morogoro mjini Bi Devotha Minja wamekamatwa na Polisi muda huu huku mgombea huyo akisakwa baada ya kuwatoroka polisi.
Inadaiwa gari yake pia imekamatwa na ilikuwa ni katika harakati za kumteka ili asirejeshe fomu ya ugombea leo.
Aidha sababu za waliokamatwa bado hazijawekwa wazi.
Maelezo haya ni kwa mujibu wa yeye Devotha Minja ambaye yupo mafichoni.
-----
Jeshi la Morogoro mjini, wamezingira ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Morogoro mjini, lengo likiwa nikumsubiri Devotha Minja wamkamate kabla ya kurudisha fomu, baada ya kupigwa simu na OCD akimtaka aripoti kituoni asubuhi hii.