Hili nimelisikia mwanzo toka kwako; ingawa nami nilikuwa sina shaka juu ya kugawanyika ndani ya CCM.
Kikwete na sehemu kubwa ya hao niliwabakisha kwenye kundi la GENGE, linalomwendesha Samia; likiwa na lengo la kumbakisha Samia madarakani kwa njia yoyote ile. Bado nasita sana kumwondoa Kikwete kwenye GENGE hilo.
Kundi la pili ni lile ambalo ni "mateka" ndani ya chama chao, kundi ambalo limenyamazishwa kwa kulinda maslahi yao binafsi. Wengi ndani ya kundi hilo ni hao uliowataja, akina Majaliwa, Nchimbi, Lukuvi, Kalamaganda Kabuti na wengi wengine wa aina hiyo.
Hilo kundi la tatu la "Sukuma Gang" bado silipi umuhimu wowote katika muundo uliopo sasa. Lakini naweza nikawa nimepitiwa na hali ilivyo saiti kwenyewe sasa hivi.