Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Sasa mkataba wa mwaka,uliona wapi unalipa miezi mitatu mitatu? Hama kwenye nyumba ya watu.
Hujui kama mkataba na malipo ni vitu viwili tofauti? Mkataba unaweza kusema malipo yatakuwa yanafanyika kwa miezi 3 mitatu ndani ya mwaka mmoja. Baada ya mwaka mpangaji atalazimika kuingia mkataba mpya na mmiliki kulingana na makubaliano mapya.
 
Angekuwa Salum au Asha kafanya hivyo, tungeipata Waislam wote humu JF na Tanzania nzima.

Lakini kwa kuwa kafanya kondoo mwenzao wa kilimanjaro, wote kimyaa.

Mbona kila kitu unahusisha na dini yako? Una shida gani? Mbona tunaishi vizuri tu kila mtu? Wewe unaishi Tanzania gani iliyojaa unafiki kiasi hicho?

Kuna wakati tunaugua magonjwa ya kuchagua wenyewe. Sio magonjwa halisia. Hili la dini, linakusumbua na halitabadilisha chochote ndani ya ulimwengu huu.

Ottoman, pamoja na kutwaa Constantinope, na zile crusade za uislamu na ukristu, zilishindwa kumaliza dini moja zaidi ya nyingine. Abdul Nasser, pamoja na nia yake ya kuifuta Israel na kuwapa support Fedayeen. Hata Hamas na Hezbollah watashindwa. Ndio maana Qatar amejitoa kusuluhisha juzi juzi.

Vita za kidini ni vita za hovyo kabisa maana hazina waungaji mkono wa kweli zaidi ya wababaishaji wanaojificha kwenye dini.
 
Wakuu, huu ni Uungwana kweli?

Huko Marogoro mwenye nyumba kamfungia ndani saa 27 mpangaji kisa amekiuka notisi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmiliki wa nyumba Plot namba 149 BLOCK ‘A’ Kihonda Kilimanjaro, Dk. Lusako Mwakiruma ilioyopo Mtaa wa Kilimanjaro Manispaa ya Morogoro, amemfungia ndani mpangaji wake kwa saa 27 kisha kumtolea vitu vyake nje, kwa madai kuwa mpangaji huyo, Paschal Paulo alishindwa kupokea notisi ya kumtaka ahame kwenye nyumba hiyo ndani ya mwezi mmoja.
kiungwana kabisa unaambiwa uhame kwenye nyumba ya mtu, ila wewe unajifanya mjuaji kaidi na jeuri zaidi ya mwenye haki,

na kwamba wewe ni hodari zaid ya mwenye nyumba right ?

nami nasema afungiwe tu maana hakuna namna nyingine sasa 🐒
 
Hiyo dini itakufanya chizi. Kwa siku usipotukana mkristo au asiye wa dini yako hupati amani. Kwa hiyo kila anayekosea makosa yake hupimwa kwa dini yake. Nenda magereza kahesabu waliofungwa na dini zao halafu ulete huo ushabiki wako humu. Wewe huwezi kumpangisha asiye wa dini yako.
Kuna mfia dini mmoja ndgu yake FaizaFoxy alikataa kuuza kiwanja chake kilicho karibu na barabara, sio kua kwasababu hana shida na pesa ila anaetaka kununua ni mkristo na yeye hapokei pesa toka kwa mtu wa dini tofauti yake.
 
Wakuu, huu ni Uungwana kweli?

Huko Marogoro mwenye nyumba kamfungia ndani saa 27 mpangaji kisa amekiuka notisi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmiliki wa nyumba Plot namba 149 BLOCK ‘A’ Kihonda Kilimanjaro, Dk. Lusako Mwakiruma ilioyopo Mtaa wa Kilimanjaro Manispaa ya Morogoro, amemfungia ndani mpangaji wake kwa saa 27 kisha kumtolea vitu vyake nje, kwa madai kuwa mpangaji huyo, Paschal Paulo alishindwa kupokea notisi ya kumtaka ahame kwenye nyumba hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Ukizichanga vizuri na case ya kidnaping jamaa inakula kwake, watu wanakuwaga na ubabe wq kipumbavu sana! Very basic law procedures
 
Kiustaarabu, mwenye nyumba akikwambia hama kwenye nyumba yake, basi mdai kodi ya miezi iliyobaki, kama kodi imeisha basi sepa tu, usitake sana mambo ya notice.

Ila kisheria mwenye nyumba ana makosa
Lazima mwenye nyumba akupe muda wa kujipanga na kutafuta nyumba nyingine(notice), tusiendekeze ujinga wa wenye nyumba kuendesha nyumba zao kiswahili swahili.
 
inaonesha uungwana ulimshinda mpangaji ndio maana mwenye nyumba naye akaweka ustaarabu pembeni, tukiwa wapangaji tukae vizuri na wenye nyumba wetu ili papanp changamoto tusitirike, ukileta ubabe na si kwako ndo madhara haya.
Nyumba za kupanga sasa zianze kusajiliwa rasmi na wenye nyumba walipe kodi ya mapato kwa serikali.
 
Back
Top Bottom