Morogoro: Polisi wazuia Msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika

Nasbukuru sana kwa jibu muruwa.

CHADEMA na vyama pinzani wanaona sawa hizi moves za ukandamizwaji wa demokrasia nchini

Ni bora wakaenda mahakamani hata kama watashindwa basi iwe walijaribu
 
Inaonekana kuna maigizo ya makusudi Samia huwa anawafanyia Chadema, ni kama vile akikaa nao wanasikilizana kama yupo tayari kukubaliana nao.

Lakini akitoka hapo anawaambia wasaidizi wake kamatieni hapo hapo, lakini ajabu wengine wanamtetea anapotezwa na wasaidizi wake, kama vile yeye ndie yupo chini ya hao wasaidizi.

Kwenye hiyo video Mnyika anaonekana kuongea na polisi kirafiki, na polisi nae anamjibu kirafiki, kama vile wanaelekea kupata suluhisho, kumbe wapi, hii tabia ya hovyo inazidi kuendelea tu.
 
Kuna polisi hapo kavaa kiraia anayeongoza magari anaitwa samson au maarufu babu makoti huyo ni occid ambaye yupo juu ya rpc, rco na ocd wake hapo Morogoro si ajabu hii kaamua yeye wala hajatumwa na kiongozi wake yeyote!

Huyo kakaa kituoni hapo zaidi ya miaka 10 keshabadilishiwa rpc wawili na ocd watatu ila yeye haamishiwi mwanzo walisema ni ndugu wa siro anamlinda wengine wakasema anatumia sana uganga na sasa sijui watasema lipi maana huyu jamaa ukiingia 18 zake umekwisha anaua watuhumiwa kwa kipigo kuliko izirael hata wiki iliyopita maiti 3 zimetolewa sero wanadai ni kazi ya mikono yake!

Cha kushangaza hq ya polisi wanafahamu tuhuma zamakoti huyo lakini hawachukui hatua yoyote dhidi yake!
 
Watu wanamiliki karibu kila kitu ila Bado Wana hofu kweli ukiwa na hatia hukai kwa amani😎
#Mabavu kwa asie na akili
 
Kuna watu wanatamani hii nchi amani itoweke. Kwanini watu wazuiwe kufanya kazi zao za kisiasa?
Hao watakuwa ni CCM wenyewe. Wanazuia mikutano halali ili kuchokoza Chadema kwa matarajio kuwa watafanya fujo ili wasema chadema ndo wasiotaka amani. Amani nintunda la haki. Haki isipokuwapo na amani haitakuwapo. CCM watende haki tu; wajitahidi tu hata kama si necha yao.
 
CCM kwishaa! Kwishaaa! Kwisha kabisaa!

Huko Kilimanjaro ccm hawaelewani, Geita na Shinyanga tafrani tupu.

Kwahiyo wakisikia harufu ya chadema tu wanatetemeka.

Mwachieni John Mnyika haraka Sana.
Kwani kakamatwa!
 

Kwanini CHADEMA wasijitoe kwenye hayo mazungumzo ya kinafiki. Mwenzako anakushughulikia huku anakuambia kaa Chini tuzungumze.
 
Ila kipindi cha JK hayo mambo ya vibali haikuepo, huyu mwendazake ndo alianzisha huu ushenzi, katika multiparty democrancy vibali hivyo vilisha tolewa na katiba tayari kwenye kipengere cha "freedom of political expression"
Kuna kitu flan jpm alikipanda , kinatakiwa kiondoke maana kitaleta ugomvi mkubwa mbeleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…