Morogoro: Polisi wazuia Msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika

Morogoro: Polisi wazuia Msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika

Umeongea maneno mengi nje ya muktadha?. Hivi Katibu Mkuu wa Chadema Hana haki ya kuwa na msafara?. Ila wa CCM ndio ana haki ya kusafiri na msafara. Naona somo la Magufuli halijakaa vizuri.

wa w
Chama tawala kazi yake kusimamia ilani ya chama kinasimamia Serikali misafara inakuwa ya viongozi wa chama na Serikali kwenda kuangalia wametelekezaje ilani ya chama baada ya uchaguzi

Msafara kama wewe sio chama tawala unahitaji.kibali,hata wa kukusanyika tu.Mbona kitu kidogo akina Kakobe tu au Gwajima nk wakienda Airport na misafara huomba vibali polisi

Ndio maana hata ukitaka kufanya send off au harusi au kitchen party lazima upate kubali.
 
Nasbukuru sana kwa jibu muruwa.

CHADEMA na vyama pinzani wanaona sawa hizi moves za ukandamizwaji wa demokrasia nchini

Ni bora wakaenda mahakamani hata kama watashindwa basi iwe walijaribu

Mahakama sio sehemu ya majaribio. Utakuwa uchizi kufungua kesi ukijua hautatendewa haki, hizo pesa na muda uliopoteza utafidiwa na Nani?. Ebu jifunzeni kwenye kesi ya Lema, Lissu ya kufukuzwa ubunge na kesi ya Sasa ya akina Halima Mdee.
 
Mahakama zipo Kenya sio huku nchi ya tozo. Mahakama za Tanzania zipo hostile kwa CHADEMA. Kuna hukumu nyingi zimetolewa baadaye zimeangushwa mahakama ya Afrika Mashariki. Inamaanisha mahakama kuu na mahakama ya Rufaa zilipitisha. Bado mahakama zetu sio za haki, bali zinaongozwa na CCM.

Sasa hivi Kuna kesi ya akina Halima Mdee ambao mahakama inawakingia kifua mpaka 2025. Kwenda mahakamani Tanzania Ni ujinga na kujichoresha. Ndio maana CHADEMA wanalili katiba mpya.
Huwezi kulinganisha utendaji wa vyama vya upinzani vya Nchi zingine za Afrika Mashariki kama vya Uganda,Kenya,Rwanda,Burundi na Congo

Vyama vyao vya upinzani nchini zao viko civilized

Vyama vya upinzani vingi Tanzania haviko civilised hasa Chadema ni chama cha wahuni Hawako focused na hawana agenda na Hawako civilized

Wanapenda sana provocations kuliko politics
 
Chama tawala kazi yake kusimamia ilani ya chama kinasimamia Serikali misafara inakuwa ya viongozi wa chama na Serikali kwenda kuangalia wametelekezaje ilani ya chama baada ya uchaguzi

Msafara kama wewe sio chama tawala unahitaji.kibali,hata wa kukusanyika tu.Mbona kitu kidogo akina Kakobe tu au Gwajima nk wakienda Airport na misafara huomba vibali polisi

Ndio maana hata ukitaka kufanya send off au harusi au kitchen party lazima upate kubali.

Tatizo mnalazimsha mfumo wa chama kimoja. Yani chama na serikali viwe pamoja. Kwenye mfumo wa vyama chama kikiunda serkali , serikali ndio inaongoza maendeleo. Viongozi wa chama wanaendelea kujenga chama na sio kusimamia maendeleo hiyo ni kazi ya serikali na wataalamu. Ndio maana tunataka katiba mpya sio huu ujinga.
 
Civilize
Huwezi kulinganisha utendaji wa vyama vya upinzani vya Nchi zingine za Afrika Mashariki kama vya Uganda,Kenya,Rwanda,Burundi na Congo

Vyama vyao vya upinzani nchini zao viko civilized

Vyama vya upinzani vingi Tanzania haviko civilised hasa Chadema ni chama cha wahuni Hawako focused na hawana agenda na Hawako civilized

Wanapenda sana provocations kuliko politics

Kwanza nikusaihihishe. Kwa Kenya mfumo wao unaruhusu chama chochote kushika madaraka. KANU, NARC, PNU, JUBILEE, na Sasa UDA. Sisi huku tumefungwa akili kwamba ni CCM tu mpaka milele.

Civilized kitu gani? Tanzania vyama vya upinzani vimepigwa marufuku kufanya siasa tangu 2015 mpaka leo. Yani miaka Saba, umewahi kusikia Kuna fujo au machafuko. Vyama vya upinzania vimetulia mpaka mkaanza kuvitukana kwamba vinalamba asali, unataka civilization ya namna gani?.

Mmeharibu uchaguzi wa 2020 Kuna machafuko yeyeote yalitokea?. Mmeua watu Pemba akiwemo Mbunge Bakari, umesikia machafuko au fujo yeyote?.

Mmeingia CHADEMA mkawarubuni wabunge wa viti maalum na kuwakingia kifua umeona chadema wanafanya fujo au kulichoma bunge Kama Burkina faso?

Civilization gani unayoiongelea? Mmekaa miaka mitano wenyewe mnafanya siasa , ilipofika 2020 mkaona maji marefu mkaamua kuharibu mchakato wa uchaguzi mpaka kuzima internet.

Siasa za Tanzania ni ovyo kwa sababu ya CCM ndio uncivilized. Wanaona wao ndio wenye hati miliki na Tanzania na kuwaona wengine Kama wakimbizi na sio raia wa Tanzania.
 
Misafara ya harusi inakubaliwa ila chadema ziara ya katibu Mkuu msafara unakataliwa.
 
Nilidhani u policcm uliisha na Mwendazake kumbe u chawa wa kipumbavu kuliko wa Mwijaku bado upo na ni policcm ile ile
 
Inaonekana kuna maigizo ya makusudi Samia huwa anawafanyia Chadema, ni kama vile akikaa nao wanasikilizana kama yupo tayari kukubaliana nao, lakini akitoka hapo anawaambia wasaidizi wake kamatieni hapo hapo, ajabu wengine wanamtetea anapotezwa na wasaidizi wake, kama vile yeye ndie yupo chini ya hao wasaidizi.

Mnyika anaonekana kuongea na polisi kirafiki, na polisi nae anamjibu kirafiki, kama vile wanaelekea kupata suluhisho, kumbe wapi, hii tabia ya hovyo inazidi kuendelea tu.
Samia ana uchu wa madaraka kuliko Magufuli japo hana sifa
 
Lakini ni lazima kitoke kabila mbili tu. Imekuwa hivyo tangu uhuru.

Hayo makabila mawili yamepatikana kutokana na nguvu ya ufuasi wa wapiga kura. Kenya wanaangalia zaidi kaunti.

Rais wa kwaza alitokea kiambu, Rais wa pili alitokea Baringo, Rais wa tatu alitokea Nyeri , Rais wa nne alitokea KIAMBU na Rais wa Tano katokea Uasin Ngishu.
 
Katika Muendelezo wa kutumiwa na ccm kisiasa , Jeshi la Polisi limetumwa tena leo kuzuia Msafara kabambe wa Katibu Mkuu wa Chadema , aliyeingia kwa kishindo mkoani humo kwa ajili ya vikao vya ndani vya chama chake ( CHADEMA DIGITAL )

Taarifa zaidi kuhusu Mtiti uliotokea zitakujia hivi punde .....

Heee! Hebu tuambie hicho kishindo kilikuwaje? Kama tetemeko la ardhi?
 
Back
Top Bottom