Civilize
Kwanza nikusaihihishe. Kwa Kenya mfumo wao unaruhusu chama chochote kushika madaraka. KANU, NARC, PNU, JUBILEE, na Sasa UDA. Sisi huku tumefungwa akili kwamba ni CCM tu mpaka milele.
Civilized kitu gani? Tanzania vyama vya upinzani vimepigwa marufuku kufanya siasa tangu 2015 mpaka leo. Yani miaka Saba, umewahi kusikia Kuna fujo au machafuko. Vyama vya upinzania vimetulia mpaka mkaanza kuvitukana kwamba vinalamba asali, unataka civilization ya namna gani?.
Mmeharibu uchaguzi wa 2020 Kuna machafuko yeyeote yalitokea?. Mmeua watu Pemba akiwemo Mbunge Bakari, umesikia machafuko au fujo yeyote?.
Mmeingia CHADEMA mkawarubuni wabunge wa viti maalum na kuwakingia kifua umeona chadema wanafanya fujo au kulichoma bunge Kama Burkina faso?
Civilization gani unayoiongelea? Mmekaa miaka mitano wenyewe mnafanya siasa , ilipofika 2020 mkaona maji marefu mkaamua kuharibu mchakato wa uchaguzi mpaka kuzima internet.
Siasa za Tanzania ni ovyo kwa sababu ya CCM ndio uncivilized. Wanaona wao ndio wenye hati miliki na Tanzania na kuwaona wengine Kama wakimbizi na sio raia wa Tanzania.