Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Fanya hivyo ndugu...
 
Je huyo bank teller sanasana atatozwa fidia isiyozidi ml 10, na Prof ndio atampa azilipe, mchezo umekwisha. Na uadui ndio itazidi kuwa mkubwa baina ya Matilda na Prof.
 
Siku hizi zinavunjwa tu nyingi na sababu sio za msingi kivile.
 
Tatizo sisi wanawake tunajazwa upepo na tunaingia kingi. Prof ataandikwa kwenye magazeti baada ya wiki wabongo wameshasahau. Unabaki uhasama wa Matilda na Prof na wanafamilia pande mbili.
 
Sheria ya ndoa ina mikanganyiko mingi. Kuanzia uhalali na uharamu wa ndoa za utotoni hadi kuishi pamoja mwanamke na mwanamume kwa kipindi fulani kutambulika kuwa ni wanandoa.
Ndio maana kimekuwa kilio kikubwa kwa mashirika kuomba irekebishwe maana ina vichaka vingi vya kujificha
 
Kwanini mlalamikaji asanuke baada ya chitaaki chikaki kutoka?
 
Thamani ya mwanaume haishuki boss?
Haishuki mkuu,mwanaume unaweza kuachana leo baada ya wiki ukaoa binti mbichi hata kama una miaka 50,sasa we fikiria jinsi gani ilivyokazi kwa mwanamke aliyezalishwa kuolewa tena hata kama ana mtoto mmoja.
 
Kama alifunga ndoa Chachi na hakupeleka taarifa serikalini, serikali haiwezi kuwa na taarifa ya hiyo ndoa, ukienda kanisani unaikuta Ila serikalini huikuti
Lazima baada ya kufunga kwa wakala uisajili ndoa yako serikalini upate cheti cha ndoa...Kile cha wakala si cheti cha ndoa ni uthibitisho ndoa imefungwa....
 
Lazima baada ya kufunga kwa wakala uisajili ndoa yako serikalini upate cheti cha ndoa...Kile cha wakala si cheti cha ndoa ni uthibitisho ndoa imefungwa....
Sidhani kama unatakiwa kusajili, talaka ndio unasajili. Mbona cha kwangu nilipewa siku ya ndoa na kimeandikwa certificate of Marriage. Mawakala ndio wanatakiwa wapeleke taarifa huko Rita
 
Sidhani kama unatakiwa kusajili, talaka ndio unasajili. Mbona cha kwangu nilipewa siku ya ndoa na kimeandikwa certificate of Marriage. Mawakala ndio wanatakiwa wapeleke taarifa huko Rita
Nilijua haya baada ya kile cha wakala kukataliwa nje ya nchi, wakaniambia hicho siyo cheti halali cha ndoa ...Ndipo ikabidi niende kuomba cheti halali serikalini, kina fanana sana na kile cha uthibitisho wa ndoa......Watanzania wengi hawafahamu hilo...Ila nadhani mahakama inakubali uthibitisho huo wa wakala wa serikali kuwa ni ndoa hata bila cheti...Mimi siyo mwanasheria nimetumia uzoefu tu.
 
Ok, mbona hao mawakala hawawaelimishi wanaowafungisha ndoa? Kazi kweli
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Ila mimama ya nyumbani inakuwaga jau sana, lenyewe likishapika michicha yake na ugali linashinda na makanga ukichanganya na visirani na ubishi wa kiha basi burudani
 
Men, by nature, are polygamous ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…