Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Hapa ninapandisha somo kuhusu SHERIA YA NDOA na taratibu zake, ni zuri sana litafaa sana hasa kwa kuzingatia comment zilizo katika uzi huu, nimeona ni vyema tupate uelewa wa sheria ya ndoa na sisi wenyewe tuwe na uamuzi wa kisheria tunapokutana na changamoto za kindoa.
Fanya hivyo ndugu...
 
The Law of Marriage Act 1971 (72)
72. Right to damages for adultery
(1) A husband or wife may baring a suit for damages against any person with
whom his or her spouse has committed adultery:
Provided that no such proceeding shall lie–
(a) where the aggrieved party has consented to or connived at the adultery;
(b) where damages in respect of the alleged adultery have been claimed in a
petition for divorce.
(2) A suit brought under this section shall be dismissed if the defendant satisfied
the court that he or she did not know and could not, by the exercise of reasonable
diligence, have known that the person with whom he or she committed the act of
adultery was married.
Je huyo bank teller sanasana atatozwa fidia isiyozidi ml 10, na Prof ndio atampa azilipe, mchezo umekwisha. Na uadui ndio itazidi kuwa mkubwa baina ya Matilda na Prof.
 
1. Kuacha (divorce) kisheria INARUHUSIWA ila zipo taratibu na lazima uwe na sababu (nazijua 3) katika hizo KUKOSESHWA AMANI haipo.
2. Kabla hujafunga ndoa jipime kama upo tayari na consequences za ndoa/divorce usioe kwa kufuata mkumbo/wazazi/marafiki.
Siku hizi zinavunjwa tu nyingi na sababu sio za msingi kivile.
 
Ndio maana nakwambia hii ni kesi mfu lengo ni kumchafulia Jina bwana Prof aonekane yeye ni mzinzi na ijulikane na watu kila kona ya nchi kwamba kuna Prof amefumwa na mkewe hilo ndio lengo la bibi Matrida hayo mengine hayamfikishi popote maana kesi haina mashiko uzani wa million 100 na scenario ya kesi haviendani,
Tatizo sisi wanawake tunajazwa upepo na tunaingia kingi. Prof ataandikwa kwenye magazeti baada ya wiki wabongo wameshasahau. Unabaki uhasama wa Matilda na Prof na wanafamilia pande mbili.
 
Sheria ya ndoa ina mikanganyiko mingi. Kuanzia uhalali na uharamu wa ndoa za utotoni hadi kuishi pamoja mwanamke na mwanamume kwa kipindi fulani kutambulika kuwa ni wanandoa.
Ndio maana kimekuwa kilio kikubwa kwa mashirika kuomba irekebishwe maana ina vichaka vingi vya kujificha
 
Profesa wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, Christopher Kasanga na mwenzake Linael Makundi mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Mandela mkoani hapo wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro kwa shitaka la madai ya Ugoni dhidi ya malalamikaji Matrida Sigaret.

Akizungumza nje ya Mahakama hiyo jana, wakili wa mlalamikaji Emmanuel Chengulo alisema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 16, 2022 na ilitajwa kwa mara ya kwanza Januari 23, 2023 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Lukumai.

Aidha, wakili Chengulo amesema katika shitaka hilo Matrida Sigaleti anawashitaki Profesa Kasanga ambaye ni mume wake wa ndoa na Linael kwa kesi ya Ugoni dhidi yao.

"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.

Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.

Kwa upande wa washitakiwa ambaye ni Profesa Kasanga na Linael Makundi wanatetewa wa wakili Asifiwe Alinanuswe ambaye alipatakiwa kuzungumzia shitaka hilo alisema hajapewa maelekezo ya kuzungumzia kesi hiyo kutoka kwa mteja wake.

"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine, wateja wangu hawajanipa maelekezo ya kuzungumza nanyi," alisema.

Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
Kwanini mlalamikaji asanuke baada ya chitaaki chikaki kutoka?
 
Thamani ya mwanaume haishuki boss?
Haishuki mkuu,mwanaume unaweza kuachana leo baada ya wiki ukaoa binti mbichi hata kama una miaka 50,sasa we fikiria jinsi gani ilivyokazi kwa mwanamke aliyezalishwa kuolewa tena hata kama ana mtoto mmoja.
 
Kama alifunga ndoa Chachi na hakupeleka taarifa serikalini, serikali haiwezi kuwa na taarifa ya hiyo ndoa, ukienda kanisani unaikuta Ila serikalini huikuti
Lazima baada ya kufunga kwa wakala uisajili ndoa yako serikalini upate cheti cha ndoa...Kile cha wakala si cheti cha ndoa ni uthibitisho ndoa imefungwa....
 
Lazima baada ya kufunga kwa wakala uisajili ndoa yako serikalini upate cheti cha ndoa...Kile cha wakala si cheti cha ndoa ni uthibitisho ndoa imefungwa....
Sidhani kama unatakiwa kusajili, talaka ndio unasajili. Mbona cha kwangu nilipewa siku ya ndoa na kimeandikwa certificate of Marriage. Mawakala ndio wanatakiwa wapeleke taarifa huko Rita
 
Sidhani kama unatakiwa kusajili, talaka ndio unasajili. Mbona cha kwangu nilipewa siku ya ndoa na kimeandikwa certificate of Marriage. Mawakala ndio wanatakiwa wapeleke taarifa huko Rita
Nilijua haya baada ya kile cha wakala kukataliwa nje ya nchi, wakaniambia hicho siyo cheti halali cha ndoa ...Ndipo ikabidi niende kuomba cheti halali serikalini, kina fanana sana na kile cha uthibitisho wa ndoa......Watanzania wengi hawafahamu hilo...Ila nadhani mahakama inakubali uthibitisho huo wa wakala wa serikali kuwa ni ndoa hata bila cheti...Mimi siyo mwanasheria nimetumia uzoefu tu.
 
Ok, mbona hao mawakala hawawaelimishi wanaowafungisha ndoa? Kazi kweli
 
Nani anataka mtu kang'ang'ana kuoga na magadi na mawese.....Prof akasema usintanie kavuta katoto keupe peee....kishundu hiihaa....kanatereza kwa kuoga na shower gel......

Wanawake jamani msibweteke mkiolewa, bado ninyi ni maua mpendeze bila mwisho, msiaachie house maid kutupikia, kutupikia...... huku nje tunakumbana na mengi....mwishowe ndo inakuwa hivi!!!
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Ila mimama ya nyumbani inakuwaga jau sana, lenyewe likishapika michicha yake na ugali linashinda na makanga ukichanganya na visirani na ubishi wa kiha basi burudani
 
Profesa wa Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, Christopher Kasanga na mwenzake Linael Makundi mfanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Mandela mkoani hapo wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro kwa shitaka la madai ya Ugoni dhidi ya mlalamikaji Matrida Sigaret.

Akizungumza nje ya Mahakama hiyo jana, wakili wa mlalamikaji Emmanuel Chengulo alisema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 16, 2022 na ilitajwa kwa mara ya kwanza Januari 23, 2023 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Lukumai.

Aidha, wakili Chengulo amesema katika shitaka hilo Matrida Sigaleti anawashitaki Profesa Kasanga ambaye ni mume wake wa ndoa na Linael kwa kesi ya Ugoni dhidi yao.

"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.

Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.

Kwa upande wa washitakiwa ambaye ni Profesa Kasanga na Linael Makundi wanatetewa wa wakili Asifiwe Alinanuswe ambaye alipotakiwa kuzungumzia shitaka hilo alisema hajapewa maelekezo ya kuzungumzia kesi hiyo kutoka kwa mteja wake.

"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine, wateja wangu hawajanipa maelekezo ya kuzungumza nanyi," alisema.

Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
Men, by nature, are polygamous ....
 
Back
Top Bottom