Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Labda kama ana kosa lingine, lakini kama ni hilo la kumlaumu Mungu itakuwa ni ujinga huu.

Sijaiona hiyo clip ya kulaumu lakini nimekutana na malalamiko kadhaa kwamba kakosea blah blah.

Kama angekashifu dini/imani ya Mwingine sawa maana hapo kosa ni kumuudhi mwingine...lakini Mungu huyu wetu sote kama Mtu ataamua kutukana kadri anavyojisikia sioni kama kama kuna mwenye mamlaka ya kumuadhibu mwingine, sana sana ni kumsihi asifanye hivyo mbele yako maana hupendi kusikia.
 
Hii kesi nashauri wai-forward kwa Askofu, Mchungaji, au kwa Baba Paroko
 
Mimi ni Mkristo, Ukristo unaamini sana katika TOBA, Yesu anasema, "amin amin nawaambieni, atakae mkufuru Baba au mwana atasamehewa, lakini yeye atakae mkufuru Roho mtakatifu hatasamehewa" Afande Sele ni kweli alikufuru, hakatai kwamba alikufuru ( anoather credit kwa Mungu ) but kaomba RADHI kwa Mungu wake aliyemkufuru na kwa wote aliowakwaza; sasa najiuliza; jamuhuri itamshtaki kwa kosa lipi? Yaani nani anae mlalamikia afande Sele?
Binafsi ninaamini kabisa (kwa matamshi yake ) huyo Mungu aliyemkashfu kisha msamehe, kwasasa Seleman Msindi kaomba msamaha kwake
 
Ndio maana ukiingia kuswali msikitini, na kusali makanisani kuna muda upo, unaomba, kuongea, kutukanana wewe na Mungu wako kimya kimya kama una bifu naye unajua mwenyewe. Ukiliweka hadharani ni kashfa kwa wasio na bifu na Miungu yao.
 
Hilo jina ni kubwa, tena la Nabii wa Mwenyezi Mungu, Hakustahili kuitwa hilo (Suleiman) badala yake wangemuita John n.k
John Bado mtume wa Mungu badala yake wangemuita afande nguchiro
 
Kama haina dini basi iruhusu watu kukashifu imani ya wengine?
Kakashifu imani ya nani? Mimi nilisikiliza ile clip. Haamini uwepo wa Mungu. Hili ni jambo la mtu binafsi. Alisema ataabudu hata jua. Huwezi kumlazimisha mtu kuamini na polisi wamefanya kosa kubwa sana. Acha Mungu ajitetee mwenyewe. Kwanza hili kwa Mungu siyo issue kubwa kama binadamu mnafiki anavyotaka ionekana. Mbona wapo watu kama kina Paulo walimhujumu Mungu lakini baada wakaja badalika?
 
Bora ashughulikiwe na serikali
Mungu mwenyewe akimshughulikia hata SEKUNDE NYINGI.
Anakauka.
Unafikiri Mungu ana akili mbovu namna hiyo? Wanafiki wakubwa nyie wanadamu. Mtu kama yule sheikh papuchi anabanjua kama hana akili nzuri halafu leo anakuja ''kumwamurisha'' Mungu aue kiumbe chake! Kwani Mungu yeye haoni? Au mnafikiri Mungu ni kama serikali inayoogopa kuhojiwa?
 
Mungu nae ana HASIRA.
Akichukia inawezekana tusiamke kesho.
Acha Afundishwe.
Kuwa hii dunia na pumzi si Yetu.
Mtu anatukaniwa BABA yake anachukia sembuse kutukaniwa Mungu?.
 
Mungu nae ana HASIRA.
Akichukia inawezekana tusiamke kesho.
Acha Afundishwe.
Kuwa hii dunia na pumzi si Yetu.
Mtu anatukaniwa BABA yake anachukia sembuse kutukaniwa Mungu?.
Hivi unajua duniani kuna mamilioni ya watu ambao hawaamini kuwa kuna Mungu na Mungu hata siku moja hajawahi kuwaadhibu? Kwa nini mnataka kumfundisha Mungu kazi?
 
Kama haina dini basi iruhusu watu kukashifu imani ya wengine?

Hujaelewa kitu, kiazi! Inawezaje kuruhusu kukashifu wakati kutoa kashfa au dhihaka ni kosa?? Wakisema haina dini hawana maana mtu aseme chochote juu ya imani ya mtu mwingine. Ina maana maamuzi yake hayataathiriwa na imani moja na si nyingine katika kushughulikia mambo ya kisheria. Kama ukiua mtu, huwezi ukasema mahakama ikuachie huru kwa sababu ulikuwa unamtoa mtu huyo kama dhabihu kwa mungu wako!!

Inabidi tutoe na mifano ili vilaza waelewe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…