Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Wakuu, nasikia tren ya SGR Dar-Dodoma imezima katika kituo cha kidete.

Milango imefunguliwa ili wapate hewa wakisubiri umeme urejee.

Mwenye taarifa zaidi atujuze.

==

UPDATE

Umeme ulirudi karibia saa saba za usiku na safari ikaendealea, hitilafu hiyo yasemwa kusababishwa na high voltage ya umeme wa TANESCO.

UPDATE

HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE

Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.

Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk

MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
View attachment 3057274
Bundi na ngedere walikata nyaya

View: https://www.instagram.com/p/C-Eyv2OKi6I/?igsh=cnFjbTVhbXU0YTZ6
 
Hiyo treni ndani nzuri sana hizo mambo kwa Tren za umeme kawaida tu cha msingi ipo salama na abiria wake..
Mimi sina shida na train ni nzuri sana, kuharibika pia sio ajabu, kuchelewa sio ajabu ila mashaka yananijia kwenye customer care, TRC walitakiwa usiku uleule kuelezea na kuomba radhi kuonesha kujali, kituoni tu hawakuweza kutoa taarifa kwenye display kama kuna delay hio ndio shida yangu.
 
Kuweni wavumilivu, Tanesco imeajiri vijana wakakamavu kitengo cha kukata umeme, sasa wanafanya majaribio, na hilo ni jaribio lakwanza. Kesho watakata line ya kizimkazi, msoga wajiandae keshokutwa.
Wanasingizia ngedere huko si wanajua ngedere haziwezi kujieleza
 
Tuwapongeze kwanza TRC kwa kuweza kuanza kwa safari za treni ya mwendokasi.

Hiyo ni changamoto ndogo sana, tena ni ya kawaida kabisa.

Tatizo watu wana negativity nyingi and are not optimistic.

By the way , mbona hamzungumzii matukio ya kukatika kwa umeme mara kadhaa na kukata kwa internet katika mashindano makubwa kabisa duniani ya michezo Olympics ufaransa ?

Watanzania tubadilike.
Sawa kabisa upo sahihi, tatizo letu sisi hatujifunzi mkuu tupo hapa hili litatokea zaidi na zaidi. Hicho tu ndicho kinachonisikitisha.
 
Hata nikitoa mapendekezo hawatoyafanyia kazi
Toa tu mimi nitafanyia.
IMG_20240731_091832.jpg
 
Wakuu, nasikia tren ya SGR Dar-Dodoma imezima katika kituo cha kidete.

Milango imefunguliwa ili wapate hewa wakisubiri umeme urejee.

Mwenye taarifa zaidi atujuze.

==

UPDATE

Umeme ulirudi karibia saa saba za usiku na safari ikaendealea, hitilafu hiyo yasemwa kusababishwa na high voltage ya umeme wa TANESCO.

UPDATE

HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE

Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.

Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk

MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
View attachment 3057274
 
Wakuu, nasikia tren ya SGR Dar-Dodoma imezima katika kituo cha kidete.

Milango imefunguliwa ili wapate hewa wakisubiri umeme urejee.

Mwenye taarifa zaidi atujuze.

==

UPDATE

Umeme ulirudi karibia saa saba za usiku na safari ikaendealea, hitilafu hiyo yasemwa kusababishwa na high voltage ya umeme wa TANESCO.

UPDATE

HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE

Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.

Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk

MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
View attachment 3057274
"Kumekuchaa"# kwa saut ya mzee majuto!!!
 
Hivi hizo nyaya hazina Insulation hadi ziharibiwe na Bundi, Ngedere?

Wataalamu mnifahamishe kuhusu hili
 
There is always a weakness point nothing works with an efficiency of 100% so ni mwanzo tuu jmn atleast nasisi nchini kwetu tunazoo hata kama zitakuwa zinazimazima
 
Back
Top Bottom