Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sheby na Abu 😂😂😂🔥
Ukiamini kwamba tatizo lilisababishwa na bundi na ngedere, basi na wewe una akili kama za bundi na ngedere, kama hao waliosema ni bundi na ngedere walisababisha tatizoWashukiwa ni Hawa hapa ,Wanajulikana Kwa picha na Majina , washughulikiwe 👇👇
heheheheheLabda wakiwa wametoroka kambi wanachepuka au kwenda kukojoa
Nimesema hivi, kama unaamini sababu za treni ya SGR kukwama ilikuwa ni ngedere na bundi, basi na wewe una akili ya kiwango cha ngedere na bundi. Na hata huyo anaesema hizo ndio zilikuwa sababu za treni kukwama, ana akili ya kiwango cha ngedere au bundibehewa la mwisho lilifuka moshi ilikua ha
Washukiwa ni Hawa hapa ,Wanajulikana Kwa picha na Majina , washughulikiwe 👇👇
View: https://www.instagram.com/p/C-E9RKFI80Y/?igsh=bjc1NTNkdWtiOHY=
View attachment 3057377View attachment 3057378
Mara bundi mara ngedere mara high volatage, semeni ukweli kama ni mikono ya waarabu mnaogopa nini kuwa wawazi?Umeme ulirudi karibia saa saba za usiku na safari ikaendealea, hitilafu hiyo yasemwa kusababishwa na high voltage ya umeme wa TANESCO.
Wakuu, nasikia tren ya SGR Dar-Dodoma imezima katika kituo cha kidete.
Pia soma: Serikali yasema treni ya SGR haitokuwa na tatizo la umeme
Milango imefunguliwa ili wapate hewa wakisubiri umeme urejee.
Mwenye taarifa zaidi atujuze.
==
UPDATE
Umeme ulirudi karibia saa saba za usiku na safari ikaendealea, hitilafu hiyo yasemwa kusababishwa na high voltage ya umeme wa TANESCO.
Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete
UPDATE
HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE
Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.
Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.
Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Jamila Mbarouk
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
Watakwambia sababu Magufuli hayupo 😂😂👇👇Ukiiga kunya kwa tembo utapasuka msamba, Tanzania ilipaswa iimarishe tu treni iliyopo ya single gauge kuliko kung'ang'ana na vitu wasivyo viweza wakati bado nchi haina umeme wa uhakika.
Kibongobongo.Lakini kitaalam tests zote anticipations na recovery strategies zilitakiwa kuwa zimefanyika kabla. Suala la ngedere hatukujua reli inapita porini kwenye nyaniz!!Mambo ya kawaida mwanzoni.
Tatizo walisema treni lina backup ya umeme kukatika sasa wanyoshe maelezo mbona wanasema limesimama kwa itilafu ya umeme nje ya treni ....hapo ndipo utata unapo anza au backup za mafuta ya generator zake wahuni wa ccm wamesha gawana kwenye vidumu .Changamoto ni jambo la kawaida, iwe umeme au changamoto za train yenyewe.
Tusiwe wepesi kuponda au kuzodoa, hakuna kitu kimefanikiwa undwa kwa ufanisi wa 100%
Pole kwa abiria wote waliokwama.
Jana kuna jamaa yangu alipanda hiyo treni,na abiria waliambiwa kuna umeme high voltage tanesco,walishindwa kubalance umeme,hyo ngedere sjui bundi ni siasa maneno tuLuku imeisha Au?