Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

behewa la mwisho lilifuka moshi ilikua ha
Nimesema hivi, kama unaamini sababu za treni ya SGR kukwama ilikuwa ni ngedere na bundi, basi na wewe una akili ya kiwango cha ngedere na bundi. Na hata huyo anaesema hizo ndio zilikuwa sababu za treni kukwama, ana akili ya kiwango cha ngedere au bundi
 
Wakuu, nasikia tren ya SGR Dar-Dodoma imezima katika kituo cha kidete.

Pia soma: Serikali yasema treni ya SGR haitokuwa na tatizo la umeme

Milango imefunguliwa ili wapate hewa wakisubiri umeme urejee.

Mwenye taarifa zaidi atujuze.


==

UPDATE

Umeme ulirudi karibia saa saba za usiku na safari ikaendealea, hitilafu hiyo yasemwa kusababishwa na high voltage ya umeme wa TANESCO.

Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

UPDATE

HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE

Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.

Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk

MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO

View: https://www.instagram.com/p/C-FFUomC7o8/?igsh=cjJwYmNhOXQ2Y2Jz
 
1722413980584.png
 
Mama anaenda kuzindua 1 August yani kesho
Mama ajiandae na figisu nyingi mimi naona wazee wa spana wamepiga spana makusud ili mama wa watu kesho atoe maelezo mengi
 
Changamoto ni jambo la kawaida, iwe umeme au changamoto za train yenyewe.

Tusiwe wepesi kuponda au kuzodoa, hakuna kitu kimefanikiwa undwa kwa ufanisi wa 100%

Pole kwa abiria wote waliokwama.
Tatizo walisema treni lina backup ya umeme kukatika sasa wanyoshe maelezo mbona wanasema limesimama kwa itilafu ya umeme nje ya treni ....hapo ndipo utata unapo anza au backup za mafuta ya generator zake wahuni wa ccm wamesha gawana kwenye vidumu .
 
Back
Top Bottom