Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

mambo za kawaida za wapi/nchi gani? Mwendo kasi mlisema hivi hivi!
Brother haya mambo yanatokea tena mnapewa taarifa Canada jamaa iliwahi kutokea ila sio muda mrefu hapo kwa Kaburu Gauteng walivyokua na tatizo la umeme iliwahi kutokea pia mambo ya kiufundi kuharibika ni kawaida sana labda mtu asijue hizi mambo sema ni vile imetokea Tanzania tunaona ni kama Wazembe.
Magari Toyota,Ford na BMw yanarudishwa kiwandani kwa sababu ya fault tena yaliyouzwa kabisa yapo mtaani kitu gani cha ajabu hapo..
 
1722418358453.png
 
Wakuu, nasikia tren ya SGR Dar-Dodoma imezima katika kituo cha kidete.

Pia soma: Serikali yasema treni ya SGR haitokuwa na tatizo la umeme

Milango imefunguliwa ili wapate hewa wakisubiri umeme urejee.

Mwenye taarifa zaidi atujuze.

==

UPDATE

Umeme ulirudi karibia saa saba za usiku na safari ikaendealea, hitilafu hiyo yasemwa kusababishwa na high voltage ya umeme wa TANESCO.

Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

UPDATE

HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE

Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.

Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk

MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
"hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system)"! Sababu hii si ya kweli, sijaona sehemu yoyote ya reli ambayo kuna waya zimetandazwa juu yake, waya zilizopo zipo kwenye nguzo labda watueleze kwanini hawakufikiria kuweka vizuwizi vya kuzuia wadudu na wanyama wasiweze kuzifikia waya.
 
Tayari, mkurugenzi mkuu wa shirika la Reli Tanzania TRC Bw Masanja Kungu Kadogoso majibu tafadhali !

WAZIRI MAKAME MBARAWA : RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA SGR DAR - DODOMA 1/08/2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=SsyA-E2wR1A

Enzi zile siku kama hii mkandamizaji ingembidi aende amejinoa. Kutojua idadi ya bundi na ngedere porini kungeweza kugeuka fedheha
 
Kuweni wavumilivu, Tanesco imeajiri vijana wakakamavu kitengo cha kukata umeme, sasa wanafanya majaribio, na hilo ni jaribio lakwanza. Kesho watakata line ya kizimkazi, msoga wajiandae keshokutwa.
Hzo line za kizimkazi,msoga wana jenereta automatic hata huwa hawajui kama kuna matatizo ya umeme nchi hii
 
Hii habari itawafurahisha wengi sana.

HATERS.
Watu inabidi wafurahie kukatika kwa umeme maana wamechukia muda mrefu sana. Ni uhuzinike kisa umeme umekatika? 😁😁😁😁.
Yule anakuja kuzindua treni ya umeme ili sijui iweje. Huo ni ufujaji wa hela na kukosa kazi. Treni inafanya kazi basi inatosha
 
Tatizo walisema treni lina backup ya umeme kukatika sasa wanyoshe maelezo mbona wanasema limesimama kwa itilafu ya umeme nje ya treni ....hapo ndipo utata unapo anza au backup za mafuta ya generator zake wahuni wa ccm wamesha gawana kwenye vidumu .
Kwa taarifa za ndani nilizopata nikuwa wakati inaingia katika eneo la Kidete kwa maana na power inakuwa switched kutoka station moja kwenda nyingine taa za charge hazikuwaka sababu umeme ulikuwa umapata short hata hivyo kwa sababu ya power back up ilitembea muda kidogo kabla ya kusimama kitu kizuri mafundi waliweza kurudishia mfumo mimi nadhani tuchukulie jambo la kawaida tu hata ndege huwa zinapata changamoto tumeona majuzi kukatika kwa IT tu ndege kibao zikashindwa kuruka, ma Bank yakafungwa hata magari yanapata changamoto na Train sababu umeme ndio nishati kuu ya kuendesha tuchukulie kawaida. Tusilifanye kisiasa sababu tu wengine wana chuki na kijani.
 
Brother haya mambo yanatokea tena mnapewa taarifa Canada jamaa iliwahi kutokea ila sio muda mrefu hapo kwa Kaburu Gauteng walivyokua na tatizo la umeme iliwahi kutokea pia mambo ya kiufundi kuharibika ni kawaida sana labda mtu asijue hizi mambo sema ni vile imetokea Tanzania tunaona ni kama Wazembe.
Magari Toyota,Ford na BMw yanarudishwa kiwandani kwa sababu ya fault tena yaliyouzwa kabisa yapo mtaani kitu gani cha ajabu hapo..
tuna historia ya failure in every aspect!
 
tuna historia ya failure in every aspect!
Ni kweli mkuu ila kujaribu vitu vizuri kama tunaweza wacha wajaribu maana vikiwepo wapo watakaokuja kufanya maajabu humo humo najua hilo ila naona tunaenda vizuri kama tutatulia...
 
Hiyo route akodishe shibibi, tuone kama haijaleta matunda.

Usikute hapo Behewa la kuendesha hiyo treni limekwisha kufa kwa kusukumiwa umeme mkubwa, bonge la hasara ya mabilioni.

Na uzembe wa umeme hauihusu mikataba ya "warranty".

Kadogosa wajibika.
 
Ameshasema ni bundi na ngedere ndio wameleta fedheha sasa ulitaka aende na gobole kuwawinda? Kazi ya askari wa wanyama pori .Hao wawajibike kutowatunza wanyama wao.
 
Ameshasema ni bundi na ngedere ndio wameleta fedheha sasa ulitaka aende na gobole kuwawinda? Kazi ya askari wa wanyama pori .Hao wawajibike kutowatunza wanyama wao.
Hizo sababu zinawezekana lakini ni za kijinga kabisa.

WQao wenye dhamana ya usalama wa reli walikuwa wapi mpaka ngedere na nyani wanakwea zilipo waya?

Katika elimu ya mawasiliano, na siku hizi imekuwa sana kuna vitu vinaitwa "telemetry". Dunia ya biashara kwa sasa mehama katika mawasiliano ya mtu kwa mtu na sasa ipo katika mawasiliano ya vitu kwa vitu na vitu kwa watu.

Sensors kidogo sana tena z gfharama nafuu sana na vijidude vya kuwatisha hao ndegere kwa sauti wasizozipenda wala hazihitaji mtu kuwepo line nzima hiyo.

Ni ujinga tu umetujaa, hakuna zaidi. Utengeneze reli ya matrilioni ushindwe kuweka vi sensoe vichache na mfumo wa kuweza kuilinda na kuiona line nzima mwanzo mpaka mwisho?

Kama si ujinga ni nini hiko?

Nafahamu kwa Watanzania wengi ambayo siyo fanyi yenu hiyo ya mawasiliano mnaweza kuona naongea vitu vya kiajabu, lakini ni vitu very simple.

usilolijuwa ni usiku wa kiza.

Hakuna ujinga zaidi ya sababu hizo kuisimamisha treni ya kibiashara maporini.
 
siyo hiko ni hicho
 
eti milango ilifunguliwa ili watu wapumue 😀 😀...kuna boya mmoja anasikika akisema umeme ukikatika abiria hatojua...mara oooh umeme ukikatika treni inatunza umeme wake inaweza tembea kilomita 100 (mia moja) bila umeme wa nje.Hivi huyu boya si achukue ustaarabu ajiudhuru atoke kwenye ofisi ya umma,??...yaani utudanganye uongo wa muda mfupi Mungu akuanike mapema hivi bado ung'ang'anie kukaa ofisi za umma. Wanatutia aibu hawa jamanii!!!...wameharibu ratiba za watu...na nibora ...waruhusu watu kubeba vyakula waingie navyo ndani, na shangazi kaja ziruhusiwe watu waingie nazo....wasitupangie maujinga yao🙁🙁
 
Brother haya mambo yanatokea tena mnapewa taarifa Canada jamaa iliwahi kutokea ila sio muda mrefu hapo kwa Kaburu Gauteng walivyokua na tatizo la umeme iliwahi kutokea pia mambo ya kiufundi kuharibika ni kawaida sana labda mtu asijue hizi mambo sema ni vile imetokea Tanzania tunaona ni kama Wazembe.
Magari Toyota,Ford na BMw yanarudishwa kiwandani kwa sababu ya fault tena yaliyouzwa kabisa yapo mtaani kitu gani cha ajabu hapo..
Umejitahidi kutetea ila haisaidii! Kwa wenzetu ni tofauti kabisa!

Na kwa nini walidanganya kuwa umeme ukilete hitilafu, diesel itakuwa standby na abiria hawatagundua kama kuna tatizo!

Shukrani zetu ziende kwa bundi na ngedere kwa kufichua hujuma hizi!
 
Back
Top Bottom