Morogoro: Watu 21 mbaroni kwa tuhuma za wizi Mtandaoni

Morogoro: Watu 21 mbaroni kwa tuhuma za wizi Mtandaoni

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewakamata watu 21 kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli na wizi wa kimtandao maarufu ‘halo halo’, katika operesheni maalumu iliyofanyika kati ya Julai 2 hadi 11, 2025.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Alex Mkama Julai 14, 2015, amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa maeneo mbalimbali ikiwamo Ifakara (Wilaya ya Kilombero), Msowelo na Rudewa (Kilosa) na Turiani (Mvomeno)

“Kati ya watuhumiwa hao, 13 wamekamatwa Ifakara,
watano Msowelo na Rudewa, na watatu Tuniani,” amesema Kamanda Mkama

Amesema watuhumiwa wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwamo kusajili laini nyingi za simu kwa majina ya watu wengine kupitia mawakala (freelancer), pamoja na kujifanya maofisa wa mitandao ya simu, waganga wa kienyeji, wafanyabiashara wa mbolea na wa chakula cha mifugo

Kamanda Mkama ametoa wito kwa wananchi kufanya kazi za halali na kuacha kufikiria utajiri wa muda mfupi usiohusisha kazi yenye kueleweka



Chanzo: ITV
 
Halo halo halo vijana wakazi ifakara ukipoteza simu au line nduguzako wataambiwa umepata ajari mikumi huwezi kuongea
 
Wezi wa mtandao wanapatikana.. Ila watekaji bado mtihani..

Mnategemea tuwaze nini?

Anyway hongereni jeshi la polisi..
 
Back
Top Bottom