Moses Lijenje aliyetajwa kutupwa na Polisi kesi ya ugaidi ya Mbowe na wenzake ni nani?

Moses Lijenje aliyetajwa kutupwa na Polisi kesi ya ugaidi ya Mbowe na wenzake ni nani?

Kila jina la Mahita linapotajwa, namkumbuka yule IGP mstaafu mwenye roho mbaya aliyemkana mwanaye baada ya dai la kuzaa na mfanya kazi wake wa ndani kuanikwa na kulipa jeshi la polisi jina ngunguli akipambana na CUF ngangari. Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka...hatimaye jeshi la wasiojulikana laweza kujulikana!
 
Ukifuatilia toka mwanzo Adamo alisema wanapobadilishwa vituo hulazimishwa na kupewa majina tofauti na majina yao halisi so unaweza kukuta huyo Moses lijenje ni katika mlolongo huo
What if kama lengo ni kutaka kupoteza uwezekano wa kupata taarifa sahihi za mtu endapo atapatiwa mateso na kuzidiwa au hata kupelekea kifo chake.

Fikiria mtu anabadilishiwa jina, mahaki alipokamatiwa pamoja na kesi kusomeka tofauti.
 
Ukifuatilia toka mwanzo Adamo alisema wanapobadilishwa vituo hulazimishwa na kupewa majina tofauti na majina yao halisi so unaweza kukuta huyo Moses lijenje ni katika mlolongo huo
Lakini Moses hakuwahi kupelekwa mahabusu... Labda walitupa juu kwa juu!
 
Duh 🙄 hii kesi nadhani inaweza kutupeleka kusiko tarajiwa.
Hii itapelekea mageuzi makubwa kwenye muundo na uendeshajo wa polisi na hatimae uonevu utakoma na hata katiba mpya itapatikana.
 
Wakati shahidi namba mbili na mshitakiwa namba tatu Mohammed Abdilah Ling'wenya wa kesi ndogo katika kesi ya Ugaidi inayowakabili kina Mbowe alimtaja Mosses Lijenje kudaiwa kutupwa na polisi wakati akifanyiwa vitisho.

Mallya: Kitu gani Kiliendelea..?

Shahidi: Maaskari wakasema Mwenzenu Moses Lijenje tumeshamtupa, Ameshatangulia huku wakinigusa Kichwani na Kitu nilichokuwa nahisi kuwa ni Bastola, Ukileta Ujanja Ujanja na wewe tunakutupa

Mallya: Maneno haya ulikuwa unaambiwa wakati gani wakati wa Safari au baada ya Kufika


Huyu Moses Lijenje ni nani?

Je yupo wapi?

Je yupo hai?

Je anahusika vipi na hawa makomando?

Je anahusika vipi na hii kesi ya Mbowe?

Shahidi anaposema polisi kudai wameshamtupa wanamaanisha nini?

Hili limeniacha na maswali mengi sana ya kutafakari.
Killers are disorganized. Hod has revealed.
 
Hivi hatuwezi kuwabana hawa Mahita na Kingai wakatuonesha Ben Saanane alipo.Hisia zina tuma kuwa jamaaa wanajua kila kitu
Hawa jamaa wana nguvu kubwa kwenye magenge hayo. Watu wenye uwdzo wa kumficha mtu kwenye magereza( bila kufata utaratibu wa kuhifadhi watuhumiwa) na wasiulizwe tena katika magereza tofauti tofauti ni watu wa hatari sana.
 
Good observation. I asked my self the same questions...Tusubiri wenye insights kama wapo.
Inawezekana hakutupwa vilevile Ila kutupwa ikawa ilikua sehemu yakutishia wengine wakili ubunifu wakipolisi dhidi ugaidi wambowe
 
Hii kesi isikilizwe kijeshi tu.raia wasiwepo.
Ingawa hao makomando baada ya kutoka jeshini.

..huwezi kuisikiliza kijeshi.

..wanaoshtakiwa ktk mahakama za kijeshi ni askari ambao wako ktk utumishi wa jeshi.

..Na baadhi ya watuhumiwa ktk kesi ya ugaidi ambao inasemekana waliachiswa kazi kwa makosa ya kinidhamu, maana yake ni kwamba walishtakiwa ktk mahakama za kijeshi na kukutwa na hatia.
 
Kwanza, unamuomba rais kuingilia mahakama. Kama Mbowe na wenzake hawana hatia, ni kazi ya mahakamas kuamuwa kuwa hawana hatia. Je, kumshauri raisi aingilkie huo ni utawala bora. Kwani wewe una wasiwasi gani? Kama Mbowe hakutenda kosa la ugaidi, ataachiwa.
Kesi siyo ya mahakama; mwenye kesi ni serikali, yaani Rais. Kazi ya mahakama ni kupokea kesi na kuisikiloza. Wakati wowote mwenye kesi, yani serikali akiamua hataki kuendelea anaiarifu mahakama kesi inafutwa.
 
Hawa police wanawezaje kuwatesa wanajeshi Hadi wengine kuwafanya kama Moses Lijenje? Wanajeshi wenzao wanajisikiaje tunapotangaza maandamano wao wanaamua kutangaza kufanya usafi?
 
Back
Top Bottom