Moses Lijenje aliyetajwa kutupwa na Polisi kesi ya ugaidi ya Mbowe na wenzake ni nani?

Moses Lijenje aliyetajwa kutupwa na Polisi kesi ya ugaidi ya Mbowe na wenzake ni nani?

Hii kesi badala ya kuleta amani uraiani kwa kuwafungia gaidi mbowe na wenzake inakoelekea italeta machafuko nchini, kwa sababu hii kesi inaeleweka ni ya kisiasa, sasa haya mambo ya jeshi la polisi kuanza kuonekana linaua watu litawaletea shida hawa askari huku vituoni kwao mitaani.

huyu mama wa kizanzibar nimeishasema afute hii kesi, haya mambo ya askari kuua watu yalikuwa awamu ya tano huko, sasa hawa kina kingai wanataka kuanza kuyaambatanisha na awamu ya sita.
Mama ameacha mahakama iamue, kitu ambacho naona amefanya vema. Muhimu ni mahakama itende haki.
 
Wakati shahidi namba mbili na mshitakiwa namba tatu Mohammed Abdilah Ling'wenya wa kesi ndogo katika kesi ya Ugaidi inayowakabili kina Mbowe alimtaja Mosses Lijenje kudaiwa kutupwa na polisi wakati akifanyiwa vitisho.

Mallya: Kitu gani Kiliendelea..?

Hawa mashahidi ni criminal defendants, sio independent witnesses. Ushahidi wao sio wa kulalia mlango wazi.
 
Hana wizi shoga angu ilikuwa jambo linaeleweka kabisa ila wao wakaiba.....kaguzi zote wanazofanya kwa watu pale inapohitajika huwa ni kwa sababu ya wizi? Kina mbowe walipokwenda kukaguliwa kwao mbowe huwa ni mwizi au wanatafutia watu sababu
Usiumize kichwa chako na huyo empty set kichwani
 
hii kesi itavurumua mengi.... ndugu wa Moses Lijenje wakisikia haya litakuwa jambo lingine jipya.
Wamemtupa jamaa yetu simple tu ,inaumiza sana

IMG-20210928-WA0068.jpg
 
Sawa Jumanne, ila siku ukiwa unaulilia uhai wako siku izrael akikufikia utatamani kuyakana haya japo nafasi hutakuwa nayo tena. Mwenzako aliyekuwa anawatuma alikuwa na jeuri ya hii hii ila Muulize aliko kama ile nafasi ya kuongoza malaika aliikuta bado iko wazi.
Huyo ndiyo ID ya gaidi jumanne kweli au umeotea tu?
 
Hawa police wanawezaje kuwatesa wanajeshi Hadi wengine kuwafanya kama Moses Lijenje? Wanajeshi wenzao wanajisikiaje tunapotangaza maandamano wao wanaamua kutangaza kufanya usafi?
Kwa hapa itabidi wajitafakari sana ,hasa kikosi cha KJ 92 hapo Ngerengere
 
Lile sio jeshi la polisi, ni kundi la wauaji wakiongozwa na lile gaidi roho mbaya Siro, ila shujaa Hamza alikataa kuonewa kifala na aliwapa za uso kabla hawajamzidi nguvu...RIP Hamza
 
Moses katajwa tena asubuhi hii... shuuli ni pevu sana hii.

Nashon: ni Kweli Kwamba Wakati Mkiwa mnaelekea Mbweni walikwambia watakupoteza.?

Shahidi: Afande Goodluck aliniambia Tutakupoteza Kama Moses Lijenje
Huyu Goodluck awekwe wazi tumjue
 
Kwanza, unamuomba rais kuingilia mahakama. Kama Mbowe na wenzake hawana hatia, ni kazi ya mahakamas kuamuwa kuwa hawana hatia. Je, kumshauri raisi aingilkie huo ni utawala bora. Kwani wewe una wasiwasi gani? Kama Mbowe hakutenda kosa la ugaidi, ataachiwa.
Zaidi ya yote mtu unatakiwa kujiuliza kwa nini wanajeshi wametumika hapa na wamekamatwa na most of them ni Komando kwanini komando? kulikuwa na tishio gani la usalama kwa mbowe mpaka alindwe na komando au Komando wahusike kwenye chama cha siasa?
 
Duh 🙄 hii kesi nadhani inaweza kutupeleka kusiko tarajiwa.
Na matarajio yetu yalikuwa ni zaidi ya 'mitano', tena; pengine ingekuwa 25 au zaidi kama kule kwa M7 na Kagame!

Hapana, hiyo mifano niliyotoa hapo ingekuwa ni nafuu sana.

Tanzania ingekuwa ni nchi ya kipekee kabisa.

Ukiulizwa utoe faida moja tu ya Corona, pamoja na ubaya wake wote; kweli utashindwa kujibu swali hilo rahisi vile?
 
Luteni Urio mmemficha wapi? Kwanini asiletwe Mahakamani kama bado yuko hai? CCM ndio magaidi wa nchi hii.

..Lt.Urio naye ataitwa mahakamani.

..Maana madai yao ni kwamba Urio alipigiwa simu ili atafute makomandoo wa kufanya ugaidi.
 
Mbowe si alikuwa analilia kutaka Maridhiano ? Sherehe za kitaifa zote anahudhuria hata bila kualikwa na kulilia mapatano.

Mwambieni hayo ndiyo majibu ya maombi yake ya kulilia maridhiano. Najua mwisho wa siku atashinda kesi ili arudi kulilia mapatano.

Tumechoka na maigizo ya huyo
Gaidi wa Demokrasia.
Dicteta anaye ng'ang'ania madaraka katika zama za democrasia.
Na kuendesha siasa za maigizo na kuzuga wananchi.

Mpizani wa kweli nchi hii alikuwa Marehemu MTIKILA TU.
R.I.P. Shujaa wetu wa mageuzi
R.I.P. D.P. Party

Wangine wote ni janja janja tu.
Huyu Gaidi mwacheni alilie kupatanishwa na Chai ya Ikulu.
 
Halafu jaji kashausoma mchezo, hivyo hataki kabisa kumtaja huyo Lijenje maana anajua itakuwa dhahama. Hawa vyombo vya dola kwani ndio hasa waliokuwa wanajiita watu wasiojulikana. Na kundi hili liliasisiwa kipindi cha JK, na lilikuja kupewa nguvu kubwa sana na Magufuli.
Kinachoendelea ni kuwa polisi wanafanya operesheni ya kuwafyeka makomandoo wanaoshiriki mission za kimataifa!
Sijuhi wanaogopa nini!
 
Back
Top Bottom