Moses Lijenje aliyetajwa kutupwa na Polisi kesi ya ugaidi ya Mbowe na wenzake ni nani?

Moses Lijenje aliyetajwa kutupwa na Polisi kesi ya ugaidi ya Mbowe na wenzake ni nani?

Hili la huyu Lijenje lina takiwa kupigiwa kelele sana na wapenda haki. Maana ina onekana polisi ndio walipoteza watu wetu wengi. Natamani kusikia Kingai na timu yake wako mahabusu kwa kesi za mauaji.
 
Lakini Moses hakuwahi kupelekwa mahabusu... Labda walitupa juu kwa juu!
Huyu kwenye maelezo ya Kingai ndiye alikuwa anatafutwa pamoja na wale washtakiwa kwa kijiwe baada ya kijiwe. Moshi na Bomang'ombe. walimtafuta hawakumpata.
 
Utesaji ni mbinu ya kizamani Sana na ya kijima Ili kupata taarifa toka kwa mtuhumiwa,japo watuhumiwa nao bila kipigo hawatoi ushirikiano.Waganga wa kienyeji wanayo elimu ya kuingia mwilini mwa mgonjwa kwa kutumia majini na kupata taarifa za mgonjwa thus ukienda kwa mganga ukuambia nikueleze matatizo yako au unieleze.

Ukimwambia nieleze atakueleza yote ambayo ni sahihi kwako.Uchawi ni sayansi ya mwafrika kwann police wasiombe msaada kwa waganga Ili wawasaidie kuyasoma mawazo ya watuhumiwa Ili kupata taarifa?

Hii torturing inawaletea ulemavu wengi hata wasio na hatia inakuja julikana ukweli mtu ashapata ulemavu wa kudumu.
 
Huyu komandoo wa pili anaonekana anayajua mengi hivyo tutajua mengi in advance kupitia kwake. Naona kaibua na linguine la shahidi wa jamhuri luteni mwenzao kuteswa kwanza kids kuibuka akiwa shahidi upande wa jamhuri. Mazingaombwe ya polisi yanaendelea kubainishwa.
Hapo ndio pamenishangaza urio kuteswa, hii itapelekea kina Kibatala watataka urio aletwe mahakamani
 
Urio ndio alikuwa awe Shahidi namba moja wa Jamhuri,lakini ghafla hajaletwa Mahakamani,kuna kitu sio bure.
Chakushangaza shahidi #2 anasema urio yupo tazara anateswa, wakati nilitarajia urio aje mahakamani kutoa ushahidi upande wa jamhuri

Hii nafikiri itapelekea kina Kibatara kuiomba mahakama imlete urio hapo ndio patakua patamu kweli kweli
 
Hii nchi ingekuwa nawatu conscious mitandaoni kote kungejaa swali
# SIRO YUKO WAPI LIJENJE??
 
Wakati shahidi namba mbili na mshitakiwa namba tatu Mohammed Abdilah Ling'wenya wa kesi ndogo katika kesi ya Ugaidi inayowakabili kina Mbowe alimtaja Mosses Lijenje kudaiwa kutupwa na polisi wakati akifanyiwa vitisho.

Mallya: Kitu gani Kiliendelea..?

Shahidi: Maaskari wakasema Mwenzenu Moses Lijenje tumeshamtupa, Ameshatangulia huku wakinigusa Kichwani na Kitu nilichokuwa nahisi kuwa ni Bastola, Ukileta Ujanja Ujanja na wewe tunakutupa
Hawa watu walizoea kupoteza watu ambazo hizi ni mbinu za kijinga na kizamani, kishamba na ulimbukeni. Leo hii wako wapi sukuma ngang likiongozwa na Bashite. Wako wapi kina Lengai ole Sabaya, wako wapi kina Dotto James na sauti zao. Ushauri wangu tuache kufukuwa makaburi, wale tunaohisi wametukosea tuwaite tuwaombe wafunguke. Tuwasamehe na kufungua ukurasa mpya kwa maslahi mapana ya taifa.

Likifanyika hilo: Mioyo ya hawa na familia yao itapona: Lissu, Alfred Mawazo, Gwanda, Lwijabe, Aquilina...........na wengine wengi ambao hatuwajui waliokutwa na mateso na huzuni kwa ujinga uliofanywa na wachache.

Hii nchi ni nzuri na imejengwa katika misingi ya utu. Tusameheane tusonge mbele. Tunapo tunishiana misuli tunazidi kurudi nyuma hatua nyingi bila kujua.

Nyuma ya pazia waigizaji ni wengi wananongonezana ndani ya CCM kuwa bora tukapitishwa kwenye tanuru la moto kila mtu akapita njia yake tukaibuka na mawazo mapya. Mawazo mapya ni kusameheana tukitunisha wote misuli hakuna atakaye ibuka mshindi wote tutapoteza.

Tuwape watu Uhuru wakusema sisi tutachukuwa mazuri na kuyakemea mabaya yao. Tukifanya hivyo hatutakosa usingizi hata kidogo. Lakini tukiwazibia pumzi watajamba na kutoa kijambo chenye sumu kinaconuka ambacho itatulegeza wengi. Tusiogopane tuangaliane kwa macho makavu na kukosoana bila kugombana hii misingi ya kujenga nchi nzuri.
 
Mbowe si alikuwa analilia kutaka Maridhiano ?
Sherehe za kitaifa zote anahudhuria hata bila kualikwa na kulilia mapatano.

Mwambieni hayo ndiyo majibu ya maombi yake ya kulilia maridhiano.
Najua mwisho wa siku atashinda kesi ili arudi kulilia mapatano.

Tumechoka na maigizo ya huyo
Gaidi wa Demokrasia.
Dicteta anaye ng'ang'ania madaraka katika zama za democrasia.
Na kuendesha siasa za maigizo na kuzuga wananchi.

Mpizani wa kweli nchi hii alikuwa Marehemu MTIKILA TU.
R.I.P. Shujaa wetu wa mageuzi
R.I.P. D.P. Party

Wangine wote ni janja janja tu.
Huyu Gaidi mwacheni alilie kupatanishwa na Chai ya Ikulu.
Utopolo 🖕
 
Hawa watu walizoea kupoteza watu ambazo hizi ni mbinu za kijinga na kizamani, kishamba na ulimbukeni. Leo hii wako wapi sukuma ngang likiongozwa na Bashite. Wako wapi kina Lengai ole Sabaya, wako wapi kina Dotto James na sauti zao. Ushauri wangu tuache kufukuwa makaburi, wale tunaohisi wametukosea tuwaite tuwaombe wafunguke. Tuwasamehe na kufungua ukurasa mpya kwa maslahi mapana ya taifa.
Lakini huwezi kutoa msamaha kwa mtu ambaye hajakiri kufanya maovu. Reconciliation inahitaji upande uliofanya makosa ukiri na kuomba kusamehewa.
 
Zaidi ya yote mtu unatakiwa kujiuliza kwa nini wanajeshi wametumika hapa na wamekamatwa na most of them ni Komando kwanini komando? kulikuwa na tishio gani la usalama kwa mbowe mpaka alindwe na komando au Komando wahusike kwenye chama cha siasa?
Tulio wengi humu huwa tunasoma kile tu kilichoandikwa humu, huwa hautuwezi kabisa kuchanganya na za kwetu!
 
Huyu Moses Lijenje ingekuwa ni mahakama huru kama zile za Kenya, Zambia, Malawi, Ghana, Nigeria, Sierra Leone au South Africa, ingeamuru aletwe awe shahidi ili aisaidie mahakama kubaini ukweli.

Lakini kwa bahati mbaya sana mahakama zetu zinafanya kazi chini ya usimamizi mkali wa serikali hasa katika vyesi hivi ambavyo serikali ina maslahi hivyo inaonekana ni kama ndoto kwa mahakama hii kuamuru hilo lifanyike kwani ni wazi kwamba ni kinyume na matakwa ya serikali hii.
 
Huyu kwenye maelezo ya kingai ndiye alikuwa anatafutwa pamoja na wale washtakiwa kwa kijiwe baada ya kijiwe. Moshi na Bomang'ombe. walimtafuta hawakumpata.
Hiyo "hawakuwahi kumpata" pengine ni hitimisho la ushiriki wa Moses kwenye tamthilia ya Kingai na Mahita.
Swali la kujiuliza hapa... Kwanini jamaa wa 92KJ wapo wengi kule Tazara?
 
Mbowe si alikuwa analilia kutaka Maridhiano ?
Sherehe za kitaifa zote anahudhuria hata bila kualikwa na kulilia mapatano.

Mwambieni hayo ndiyo majibu ya maombi yake ya kulilia maridhiano.
Najua mwisho wa siku atashinda kesi ili arudi kulilia mapatano.

Tumechoka na maigizo ya huyo
Gaidi wa Demokrasia.
Dicteta anaye ng'ang'ania madaraka katika zama za democrasia.
Na kuendesha siasa za maigizo na kuzuga wananchi.

Mpizani wa kweli nchi hii alikuwa Marehemu MTIKILA TU.
R.I.P. Shujaa wetu wa mageuzi
R.I.P. D.P. Party

Wangine wote ni janja janja tu.
Huyu Gaidi mwacheni alilie kupatanishwa na Chai ya Ikulu.
wewe mpumbavu unachangia mada gani?
 
Kuna watu wengi sana wameuawa pale, natumaini siku moja yaliyopo gizani yatamulikwa.[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827]
Kwanza mungejiuliza Wakati Ben Saanane anapotea miaka hiyo nani alikuwa mkuu wa kituo Tazara na nani alikuwa mkuu wa kituo Mbweeni labda inaweza saidia kuunganisha na kujua Ben alipoteaje
 
Back
Top Bottom