Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Mie nineoa huko tena ukoo wa kawaida tu Ila nawaona mashemeji usipowapa hata lift au kuwapa support wakati wa sikukuu sababu pia kuna Bibi wa watoto wangu nao wanahitaji kuwa nae wakati wa likizo nyingine, wengine wanakuja mwaka mpya tu Ila wakizipata Wana tabia ya kishenzi sana wanakusahau uliyemsaidia tena especially sisi tunaotoka mikoa mingine
Mkuu ukitajirika unauliwa ili hao jamaa dada Yao awape Mali yako ili wadunde.
Jitahidi uwawezeshe iyo lazima uchagani Kama umeoa.
Mana huwezi kuwa na Mali na ndugu wa mke wanateseka watakakumaliza upumzike kwa amani
 
Daaaaah binti anaonekana Wife Material kabsa ukikutana nae road unaapa viapo vyote kua lazima awe wako na kujuta majuto yote hadi kujikana nafsi endapo hutamweka kwenye himaya yako, moyo wa mtu ni kichaka na maisha yana siri nyingi sana [emoji846][emoji846][emoji846][emoji846]
 
Hivi Kuna unyama mkubwa zaidi ya kuua?
Ukikua siku moja utakutana na matukio ya kinyama zaidi ya kuua, dunia kila siku ina mambo mapya yapo ambayo unaweza ukafa bila kuyasikia lakin yanafanyika ila tatzo la ubinadam ni unafki mchawi ataua na atakula nyama ya binadam lakin atajidai anasikitika kuona mtu alieua akazika
 
WACHAGA NA AMBAO WAMEJAA CHADEMA NA WANATAKA TUWAPE NCHI.
JamiiForums1232863076.jpg
 
MOSHI: BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI ILI ARITHI MALI, MWILI WAGUNDULIWA BAADA YA MWAKA MMOJA

• Meya Juma Raibu ashindwa kujizua amwaga machozi na kulaani vikali, awaasa vijana kuacha tamaa na starehe
•Meya Raibu ampongeza Rpc Kilimanjaro ACP Simon Maigwa na timu Yake Kuendelea Kusikiliza Na Kutatua Jinai Mbali Mbali


Ikiwa zimepita siku kadhaa toka litokee tukio la kijana mmoja jijini Arusha kumuua mama yake mzazi Kwa tamaa ya Mali, Limegundulika tukio lingine la kinyama mkoani Kilimanjaro katika Manispaa ya Moshi ambapo binti mmoja aliejulikana Kwa jina Moja la Wendy amemuua Mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambae ni Nesi mstaafu wa Hospital ya KCMC.

Jeshi la Polisi limeufukua Mwili huo leo tarehe 09-01-2022 katika kata ya Rau baada ya kumhoji binti huyo Kwa zaidi ya wiki mbili sasa Kisha kukiri kumchinja mama yake Kwa panga na kumfukia nyumbani hapo.

Ni takribani Mwaka sasa ndugu na majirani walipokuwa wamuulizia mama huyo walipatiwa majibu na binti huyo kuwa amesafiri Kwa matibabu nje ya nchi.

Akizingumza Kwa uchungu huku akilengwalengwa na machozi Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ndg Juma Raibu ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho na amelaani vikali tabia ya vijana kuendekeza tamaa na kukosa uvumilivu wa utafutaji Mali Kisha wanaishia kufanya matendo ya kinyama.
Namnukuu

"Kiukweli hili ni tukio la kutisha, nitoe pole Kwa familia ndugu na majirani wote mliofika hapa, nimepata huzuni sana kuona jinsi gani ya taamaa Mali imetufikisha hapa, nalaani na ninatoa wito Kwa vijana wenzangu wote nchini kuacha kupaparikia Mali na starehe mwisho wake tunageuka kuwa wanyama kiasi hiki, yaani unamuua mama mzazi? hivi unakuwa huoogopi laana na adhabu ya mola? nalipongeza Jeshi letu la Polisi Kwa hatua hii nawatia Moyo mwendelee na kazi hii njema ya kufichua na kudhibiti wahalifu wa namna hii na wanaoshirikiana nao"
mwisho wa kunukuu.

Tayari madaktari wameanza kufanyia uchunguzi wa postmortem Mwili huo kwajili ya hatua zinazofuata.

#MoshiBlog UpdatesView attachment 2075108View attachment 2075109
Duh hii hatari
 
Ndio hataki na pesa yake, tafuta zako
Sasa atakataaje tena wakati mie ndio mtoto wake? Haoni kuwa hiyo ni rroho mbaya tuu? Yaani mtoto ateseke huko wakati mie ninauwezo wakumsaidia as long as haendi kufanya kitu kinyume na sheria za nchi....hapo sasa sioni faida ya kuwa mzazina mtoto nae hataona faida ya kuwa na mzazi mwenye uwezo kiuchumi.
 
Kila siku tunasema ......wachaga sio wa kuoa ........mnakua wabishi

Ona Sasa wameanza kuwahishana wao kwa wao

Anyway huu ni unyama mkubwa
Kila mtu ana ushetani wake, s wachaga tu. Mbona kuna wachaga wametulia hawana tamaa za kishetani, na je yule aliyemuuza Yesu n mchaga[emoji2955].



Ifke mahali hyo mitazamo potofu mlio nayo juu ya wachaga muache...
 
Back
Top Bottom