Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Kwani uongo?! Watafute zao kweli. Hata wakiendelea kuuwa wazazi ndio itasaidia?! Ni uvivu tamaa kukosa mbinu akili duni ndio inawafanya wawe majinga kutokutafuta zao. Na wafanyayo haya wafie jela au wafe kwa kamba tu
Ndio watafute za kwao kwa kutumia hizo za kwako wewe mzazi. Tatizo lipo wapi hapo?
 
Mzazi wako aligawiwa au alitafuta kwa jasho lake......???
Sasa yeye kutafuta hizo mali kwa jasho ndio atake na mwanae nae ataabike kama yeye? Huo basi uzazi wa kukomoana na wakijinga.
Wewe kama mzazi unapaswa kumrahisishia maisha mwanao kama kutumia malinulizo nazo kutasaidia katika hilo, basi ni vyema ukamshirikisha mwanao kwa manufaa ya familia kwa ujumla.
 
Kuna watu ni majasiri au mashetani, unaua mtu,unamfukia na unaendelea na maisha kawaida tuuu ???????
Moyo wa mtu kichaka, hata wewe una mengi umeyazika moyoni japo si makubwa kama haya na yanakusumbua akili unapokuwa peke yako, ni vile tu hatuwezi kuona yaliyo mioyoni mwa watu. Watu wanateseka sana katika nafsi zao kwa mizigo ya mawazo mkuu.
 
hakuna shortcut kwa maisha tuko nayo.
Tatizo La vijana kupenda mserereko. Huyu na yule wa Arusha lazima wanautindio, hizo mali kwani angeshirikiana na mama yake kuziendekeza mwisho wa siku si zingekua zake.

Ila ,wakati mwingine wanasema " Ukiishi kwa Upanga Utakufa kwa Upanga" huenda na hao mama zao nao hizo mali walizipata kwa njia hiyo hiyo.
 
Sasa yeye kutafuta hizo mali kwa jasho ndio atake na mwanae nae ataabike kama yeye? Huo basi uzazi wa kukomoana na wakijinga.
Wewe kama mzazi unapaswa kumrahisishia maisha mwanao kama kutumia malinulizo nazo kutasaidia katika hilo, basi ni vyema ukamshirikisha mwanao kwa manufaa ya familia kwa ujumla.
Lakini Hilo ni jambo la khiyari kwa mzazi.....kama amekusomesha kwa gharama basi ni wajibu wako kumalizia alipoishia......uwekezaji wa fedha zako amewekeza kwenye elimu yako....
 
Kuna magonjwa ya akili pia, watu wengi ni vichaa kichwani na mara nyingi ni ya kurithi unakuta Wazazi ni vichaa pia, Babu na Bibi na kuendelea.
Mental illness is a tragedy. We are in for premium tears!
 
Lakini Hilo ni jambo la khiyari kwa mzazi.....kama amekusomesha kwa gharama basi ni wajibu wako kumalizia alipoishia......uwekezaji wa fedha zako amewekeza kwenye elimu yako....
Kumpa mtoto elimi ni jambo la muhimu. Zamani wakati bado tupo smal smal population hiyo elimu waa a guarantee kupata job. Mambo sasa yamebadilika kabisa.

Wasomi wapo mtaani wanahangaika....kama mtoto kaumiza kichwa na kaja na wazo zuri ambalo linahitaji usaidizi toka kwako mzazi basi ni vyema ukamsaidia.

Kama mzazi hupendi kuona mwanao anataambika...ni ule upendo wa asili wa mzazi. Hivyo basi tumia mali zako katika kumsaidia mwanao kupata mali zake.

Kama mtoto umemlea vizuri sidhani kwamba kumwambia mwanangu hizi mali zote nizochuma ni za kwetu sote hivyo nataka wewe uzitumie kuendeleza utajiri wa familia kutamfanya abweteke but rather itamfanya atambue kuwa ana jukumu kubwa na kwamba mzazi wake anamtegemea na kuthamini uwepo wake katika familia.
 
Inawezekana kua ni kweli lakini kwa jicho la kibinadamu lawama lazima ziende kwa binti. Lakini je
Huyo mama alikua na mtoto mmoja tuu kiasi cha kufanya tukio na asijulikane?
Uhusiano wake na majirani upo je?

Maswali ni mengi sana

Mwaka mzima watu hawajastuka
 
Yesu alipouawa alikuwa na msala gani hadi laana ya kuuliwa ikamfuata?

Seems wewe pia utakuwa unammind mzazi wako kwa kukufanyia unoko na sasa unamfanyia timing ili laana yake naye imfuate

Wewe jua laana inatafun vizazi

Kwahiyo kama unacholopoa mimbaza watu huko hospitalini ujue UTALIPA
 
Kumpa mtoto elimi ni jambo la muhimu. Zamani wakati bado tupo smal smal population hiyo elimu waa a guarantee kupata job. Mambo sasa yamebadilika kabisa. Wasomi wapo mtaani wanahangaika...
Bado ipo kwenye khiyari ya mzazi.....na khiyari hiyo ya mzazi itasukumwa na utashi na mwenendo wako kijana.

Vijana wengi wanaoshikwa mikono wanawaangusha wazazi wao kwa kwnda kinyume na matarajio.

Kama wewe ni Simba wa vita na unaonyesha weledi kwenye mambo yako basi wewe ni hazina kwa wazazi wako na lazima wawe nyuma yako kwa Hali na mali.
 
Wastaafu wengi wanapangiwa kuuwawa na watoto wao,sema tu ni chance inakosa matukio yangekuwa mengi zaidi
 
Hawa polisi wetu ukute wamemuingizia sana chupa za mirinda na bia huyo binti huwa najiuliza Kwan hakunaga mbinu zingine za kugundua ushahidi wa haya matukio ukiacha hii ya kutesa
 
Back
Top Bottom