Mkuu jinsi watu wanavyoichukulia corona unadhani ni sawa uhalisia wa corona yenyewe?
Dunia nzima inazungumzia corona na kusema ni ugonjwa na mambo mengi yamevurugika kwa sababu ya corona,lakini wakati huo huo tunaambiwa wanaopata huu ugonjwa na kupona ni wengi kuliko wanaokufa kwa maana vifo vya corona ni vichache tofauti na ugonjwa kama Ebola. Na pengine ndio sababu insyofanya watanzania kuamini hakuna corona Tz kwa sababu laiti corona ingekuwa inapukutisha watu basi kusingekuwa na huku kuamini kwamba hakuna corona.
Je, unafikiri kwanini sasa corona imekuwa ikionekana ni ugonjwa hatari sana?
Hayo mataifa ya Ulaya, Asia na Marekani wanavyoichukulia Corona ni sawa kwa maana husumbuliwa sana na magonjwa ya aina hiyo kama influenza, inawezekana ni biolojia ya miili yao na hali ya hewa.
Corona imeonekana ni ugonjwa hatari kwa sababu
1. Kutokana na nchi ulizoanzia, kwa kua wao ndio wenye vyombo vya habari vikubwa na kuendesha uchumi wa dunia, kama ungeanzia Afrika ungetangazwa kwenye habari zao mara moja moja tena kwa habari fupi tu na ingewezekana wangetutenga kabisa, hamna mtu kwenda kwao wala wao kuingia huku hovyo hovyo.
2. Corona haiui kila mtu anayeupata ila inasamabazwa kiurahisi kwa watu wengi ndani ya muda mfupi kuliko magonjwa kama Ebola na hata yale mafua ya ndege (H5N1), hii ni kwa sababu hata mtu asiyekuwa na dalili anaweza kuueneza kwa njia ya hewa bila kujia wakati hayo magonjwa mengine huenezwa pale ambapo virusi vinakuwa vimeushambulia sana mwili na mara nyingi mgonjwa huwa mahututi na hawezi kuzunguka na kuusambaza kwa urahisi.
Afrika ni nchi chache zinazoweza kukabiliana na Corona kwa uhakika kutokana na hali duni ya kiuchumi, kwa mfano Kenya tangu wanapambana na Corona wameripoti vifo 1736 , hiyo ni karibu mwaka sasa, na ndani ya mwaka huo huo wana wastani ya vifo
10,700 vinavyotokana na Maralia, jiulize bado magonjwa mengine kama TB, homa ya ini. Inawezekana nguvu kubwa ingewekwa kwenye haya magonjwa yetu ingeokoa uhai wa watu wengi zaidi kuliko tu kuhangaika na ugonjwa mmoja.
Jiulize kwa nini ukienda kukaa huko Ulaya watakuambia uonyeshe kama una chanjo mara ya Yellow Fever, upimwe TB na mengineyo lakini kamwe hawakuambii uonyeshe ama upewe chanjo ya Influenza zinazowasumbua, wakati wao kila mwaka wanapeana chanjo za influenza ili kujilinda na wala hawajali kama tutazibeba hizo influenza na kuzileta kwetu ila hawataki haya magonjwa yetu makali yawafikie kwa namna yoyote maana walishayadhibiti siku nyingi.
Ni ngumu kuamini kwamba corona haipo kabisa Tanzania kutokana na muingiliano tulionao na mataifa yenye maambukizi makubwa ya Corona, hakuna haja ya kuanza kuweka watu lockdown ama quarantine na kufanya mass testing, hiyo muda wake umeshapita na gharama ni kubwa ila ni bora tu tungeambiwa ukweli ugonjwa upo na kukumbushana kuchukua tahadhari, ikiwapo hata mtu ukijiona hali si nzuri ni bora ajitenge mwenyewe kwa muda, apige dawa zetu asili ili usiusambaze kwa wengine. Sasa hivi kuna watu wanaona aibu hata kuvaa barakoa na wanazo ndani huku wana matatizo lukuki ya presha, sukari n.k. ambayo yanaweza kuwa hatarishi endapo watapata maambukizi.