Moshi: International School of UWCEA yasitisha masomo Baada ya Wanafunzi 2 kupatwa na Corona

That is it! shule ndio imeshafungwa milele, tungoje ni watu wangapi watakamatwa kwa hujuma mbali mbali kuanzia kutolipa kodi hadi kutokuwana vibali halali vya kuishi na kufanya kazi nchini.
Na hii ndio dawa yao hao mbwa wanaotaka kufanya kazi ya wizara ya afya, nani kawapa ruhusa ya kusitisha utoaji elimu? Masharti ya leseni yao ndio yanasema hivyo, kwamba wafunge tu shule kadri wanavyojisikia bila kushirikisha mamlaka husika? Nyang’anya leseni hao mbwa haraka sana!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] eti takwimu zinatolewa kwenye makoti, pole kwa kuugua mkuu
Mkuu ahsante nimeshapoa hiyo kitu ilikuwa inanipa machungu wenzangu wanasherekea mdudu kaondoka, halafu kiutani utani nilikuwa naona jahazi linaelekea kuzama. Nakumbuka sana waheshimiwa walivyokuwa wanatoa vikaratasi kwenye koti wanasema wagonjwa wamebaki wachache sana kwenye vituo vya kuwahudumia na hivyo ugonjwa ndio unaondoka.
 
Mkuu ukipata muda embu share strategies ulitumia walau tuwe equipped in case of anything

Natanguliza shukrani
Niliwahi kuandika njia niliyotumia hapo nyuma baada ya kupata nafuu:
  • Kunywa mara tatu mpaka tano kwa siku mchanganyiko wa limao+tangawizi+pili pili kichaa -> Kupunguza kikohozi.
  • Kusukutua koo na mchangayiko wa maji ya uvuguvugu na chumvi -> Kupunguza maumivu ya vindonda kooni.
  • Kutafuna karafuu na tangawizi mbichi - kurudisha ladha ya chakula, na kutuliza maumivu ya vidonda kooni.
  • Kujifukiza kwa majani ya mkaratusi, tangawizi na viks kingo ya mafuta ->Kufungua pua na kurudisha pumzi.
  • Panadol -> Kupunguza maumivu ya kichwa na kutuliza homa.
Inategemea na mwili wa mtu lakini, sijui kama ni formula ambayo itatibu 100% kila mtu. Hii ishu ya kwenda kupima wakati unaumwa ni kutafuta "stress" nilifanyiwa IgM antibody test 2 tofauti baadaye na kupimwa mapafu walinikuta nina viashiria kuwa nilipata maambukizi, mapafu yalipungua uwezo wake nikashauriwa na huyo daktari nifanye mazoezi mepesi kwanza maana nilikuwa nimepona ila naona kama mwili umebadilika na sio wangu, ila kwa sasa naona nipo imara kwa asilimia 99% kama sio 100%.

Hao watu walipima na kupata majibu kuwa ni corona au ndio kipimo ni dalili tu za corona?
Mfano wa karibu kabisa kuna jamaa nafahamiana naye kabisa alikuwa anataka kwenda South Africa kikazi December, alipimwa hiyo kitu ili apate cheti asafiri akakutwa positive alikuwa analalamika anakosa hela ya January. Alikuwa na mafua na kichwa kuumwa kwa mbali na tulikuwa wote bar tunabadilishana mawazo ndio akafunguka hilo jambo, alikuwa na mafua tu kwa mbali na uchovu kidogo, nadhani niliwahi kuandika humu. Ukitaka kupata stress ni uanze kupima watu wengi na utangaze idadi ya walioathirika, mbona tutakimbiana. Ni bora tu maisha yaendelee, ukiona hali si hali njia mbadala za kukabiliana nazo zinajulikana, wewe mwenyewe chukua tahadhari pale inapobidi tuendelee kutafuta maisha.
 
Kwahiyo wakikupima na kukukuta positive wanakuacha tu uingie mtaani kama kawaida ukajiuguze mwenyewe
 
Hakuna sababu ya kumuweka mtu hospitali kama hana dalili kali, hata kwa nchi za walioendelea wanafanya hivyo. Tofauti ni kwamba wao wanahimiza watu wajitenge, na hutoa adhabu kali kama ukikutwa unazunguka mtaani. Huku kwetu ni ngumu mtu kujitenga njia pekee kama tungetaka kutenga watu ni kuwafungia wale ambao wapo positive quarantine, na yenyewe haitekelezeki ukisema uweke kila mtu aliye positive unaweza ukajaza kiwanja cha mpira na kutumia gharama kubwa. Corona ingekuwa ni ugonjwa unaoua kama Ebola au zaidi tungekuwa tunaongea mengine, ni ugonjwa hatari lakini ni asilimia chache ndio hufariki pale wanapoupata.
 
Shule ya kimataifa ya UWCEA Kampasi ya Moshi, Kaskazini mwa #Tanzania imesitisha mafunzo ya ana kwa ana kwa Wanafunzi kwa madai ya mmoja wa Wanafunzi kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya Corona.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya Shule hiyo, Januari 18 Mwanafunzi huyo alithibitishwa kuwa na Corona na jana Jumanne, Mwanafunzi mwingine ameonesha dalili za maambukizi ya virusi hivyo.

=====

A UWCEA day student in the M4 class in Moshi Campus tested positive for Covid-19 on 18th January. On 19th January a second student is displaying symptoms that may indicate Covid-19 although this has not yet been tested. As a result, the Moshi Campus has temporarily stopped all face-to-face teaching and has moved all learning online until 1st February.

Details are given in the Director’s letter of 19th January, as well as in her earlier email of 18th January. Information on the Distance Learning Program can be found at the Distance Learning Update.
Arusha Campus is continuing face-to-face teaching with additional precautions.

Anecdotal evidence suggested that the incidence of the virus in Tanzania was relatively low for much of 2020, but the current situation is unfortunately less clear.

Tanzanian authorities do not publish details of coronavirus cases in the country and there is no information about any tracking of the epidemic. Official figures have not been released since April 2020 (and the figures given on most data collection sites are those from that date).

There are no mandated rules for slowing the spread of the virus although social distancing and hand washing were advised. At present most people do not wear masks. In December a Ministry of Health spokesman indicated that there were no plans to import any Covid-19 vaccines to the country.

Hataree. Twifwaaaaa
 
Kuna jilani/ndugu yako kafa kwa corona mbona mnataka kusimamisha shughuri za watu aise, gvt imetunyima ajila tumeamua kujiajili we unataka tufungiwe ndani

Watanzania bana saijui tunataka nini, wacha tupige kazi aise
Alishasema hakuna cha lockdown wala shangazi yake na lockdown.
 
Shule ya kimataifa ya UWCEA Kampasi ya Moshi, Kaskazini mwa #Tanzania imesitisha mafunzo ya ana kwa ana kwa Wanafunzi kwa madai ya mmoja wa Wanafunzi kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya Corona.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya Shule hiyo, Januari 18 Mwanafunzi huyo alithibitishwa kuwa na Corona na jana Jumanne, Mwanafunzi mwingine ameonesha dalili za maambukizi ya virusi hivyo.

=====

A UWCEA day student in the M4 class in Moshi Campus tested positive for Covid-19 on 18th January. On 19th January a second student is displaying symptoms that may indicate Covid-19 although this has not yet been tested. As a result, the Moshi Campus has temporarily stopped all face-to-face teaching and has moved all learning online until 1st February.

Details are given in the Director’s letter of 19th January, as well as in her earlier email of 18th January. Information on the Distance Learning Program can be found at the Distance Learning Update.
Arusha Campus is continuing face-to-face teaching with additional precautions.

Anecdotal evidence suggested that the incidence of the virus in Tanzania was relatively low for much of 2020, but the current situation is unfortunately less clear.

Tanzanian authorities do not publish details of coronavirus cases in the country and there is no information about any tracking of the epidemic. Official figures have not been released since April 2020 (and the figures given on most data collection sites are those from that date).

There are no mandated rules for slowing the spread of the virus although social distancing and hand washing were advised. At present most people do not wear masks. In December a Ministry of Health spokesman indicated that there were no plans to import any Covid-19 vaccines to the country.

Kwa hiyo umeandika na kiingereza ili bwana zenu wajue au unataka kuonyesha unajua kiingeleza?
Kiswahili ulichoandika umeona watanzania hawajaelewa ila kiingereza ndo watajua na bibi zako huko mtwara?
 
Tatizo hakuna ukweli kwenye jambo hili, takwimu hamna, ila uai si mali ya serikali, jikinge!
 
Hakuna sababu ya kumuweka mtu hospitali kama hana dalili kali, hata kwa nchi za walioendelea wanafanya hivyo. Tofauti ni kwamba wao wanahimiza watu wajitenge, na hutoa adhabu kali kama ukikutwa unazunguka mtaani. Huku kwetu ni ngumu mtu kujitenga njia pekee kama tungetaka kutenga watu ni kuwafungia wale ambao wapo positive quarantine, na yenyewe haitekelezeki ukisema uweke kila mtu aliye positive unaweza ukajaza kiwanja cha mpira na kutumia gharama kubwa. Corona ingekuwa ni ugonjwa unaoua kama Ebola au zaidi tungekuwa tunaongea mengine, ni ugonjwa hatari lakini ni asilimia chache ndio hufariki pale wanapoupata.
Mkuu jinsi watu wanavyoichukulia corona unadhani ni sawa uhalisia wa corona yenyewe?
Dunia nzima inazungumzia corona na kusema ni ugonjwa na mambo mengi yamevurugika kwa sababu ya corona,lakini wakati huo huo tunaambiwa wanaopata huu ugonjwa na kupona ni wengi kuliko wanaokufa kwa maana vifo vya corona ni vichache tofauti na ugonjwa kama Ebola. Na pengine ndio sababu insyofanya watanzania kuamini hakuna corona Tz kwa sababu laiti corona ingekuwa inapukutisha watu basi kusingekuwa na huku kuamini kwamba hakuna corona.

Je, unafikiri kwanini sasa corona imekuwa ikionekana ni ugonjwa hatari sana?
 
Unaposema vifo vya kutatanisha una maana gani? kwamba kuna vifo ambavyo wataalamu hawajavielewa kwa hiyo vinahitaj uchunguzi?
Ndio maama yake,kuishia kusema matatizo ya kupumua haitoshi!Tungebiwa hayo matatizo ya kupumua yametokana na nini?
 
Back
Top Bottom