Moshi-Kilimanjaro: Kuna watu wana tabia ya kuchinja mbwa na kuuza supu

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Moris Makoi amesema kuna tabia ya baadhi ya watu kuchinja mbwa na kuuza nyama kwenye mabucha huku wengine wakichemsha supu ya mbwa na ndizi na kuwauzia watu wakidai ni supu ya nyama ya ng’ombe.

Akizungumza kuhusu tatizo hilo Makoi amewataka watumishi wa Idara ya Afya kuimarisha usimamizi wa utoaji wa vibali vya kusafirisha wanyama, kukagua na kusimamia mabucha kwani kuna wafanyabiashara wanaweka nyama ya ng’ombe yenye mihuri mbele ya mabucha huku ndani wakiweka vibudu.

Idara ya Afya katika halmashauri ya Wilaya ya Moshi imesema operesheni ya kukagua mabucha ya nyama ili kubaini wafanyabiashara wanaouza nyama ya mbwa tayari imeanza huku Mganga Mkuu wa Halmashauri, Alex Kazula akibainisha kuwa wameanza kufanya ukaguzi kwenye maeneo yanayodaiwa kuwa na tatizo hilo ikiwemo Kata ya Kibosho Kati, Okaoni na Kirima
 
Kuna siku nilikula mishikaki,wakati natafuna ile ladha yake nikasema mmh huyu atakuwa mbwa asee.

Jamaa muuzaji naye alikuwa makini sana kuniangalia wakati nakula ule mshikaki. Kuanzia siku hiyo Mimi nakula pweza na ngisi tu kwa sababu anaonekana alivyo. Mishkaki hapana kwa kweli.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kama hawajafa mbona poa tu..!!
 
Viongozi wetu wana hoja ndogo sana.
Sana. Kama vile mtu akila supu ya mbwa atapata covid. Anakomaa na wanaokula supu ya mbwa huku shule kadhaa kwenye hiyo halmashauri anayoongoza haina matundu ya vyoo. Anasubiri msaada wa USA
 
Imewadhuru? Wale tu. Ndiyo nyama waliyobarikiwa kwa kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia-nchi. Wasisahau kunywa mchuzi wake unaimarisha afya ya mwili na akili. Nyama inogile!
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Moris Makoi amesema kuna tabia ya baadhi ya watu kuchinja mbwa na kuuza nyama kwenye mabucha huku wengine wakichemsha supu ya mbwa na ndizi na kuwauzia watu wakidai ni supu ya nyama ya ng’ombe.

Akizungumza kuhusu tatizo hilo Makoi amewataka watumishi wa Idara ya Afya kuimarisha usimamizi wa utoaji wa vibali vya kusafirisha wanyama, kukagua na kusimamia mabucha kwani kuna wafanyabiashara wanaweka nyama ya ng’ombe yenye mihuri mbele ya mabucha huku ndani wakiweka vibudu.

Idara ya Afya katika halmashauri ya Wilaya ya Moshi imesema operesheni ya kukagua mabucha ya nyama ili kubaini wafanyabiashara wanaouza nyama ya mbwa tayari imeanza huku Mganga Mkuu wa Halmashauri, Alex Kazula akibainisha kuwa wameanza kufanya ukaguzi kwenye maeneo yanayodaiwa kuwa na tatizo hilo ikiwemo Kata ya Kibosho Kati, Okaoni na Kirima
Kiongozi kuropoka bila kufanya utafiti inaeza sababisha taharuki sana, its better wakajiridhisha kwa tafiti na kuja na data ndio iwe pubic!! mfano Mh. mwanasihasa hapo angesema wamebaini Mbwa kadhaa wameuzwa kwenye mabucha kadhaa maeneo kadhaa kwa kuyataja etc yaani a-apply (5W+H ) approach! (what, when, where, who, why na How)
 
Huo unaofanyika ni utapeli.

Kuna mahali tulikuwa na kazi fulani Vijijini huko, Sasa na Ugeni wetu asubuhi tukafika kwenye ki center tukaagiza mchemsho na Ndizi.

Sasa kwenye kula pamoja na kujaza pilipili za kutosha bado Ile nyama ilikuwa na utamu tamu hivi, nikamwomba Mzee Mmoja aonje Ile nyama na aniambie nyama ya Nini. Mzee akanambia Kijana wangu hii ni nyama ya Nyani.

Kuanzia siku Ile kama nina kazi za Site bora kubeba Biscuits kuliko kula kula nyama hazieleweki.
 
Wewe mnyalu nini mkuu?
Si suala la unyalu..!! Vitu vingi sana hamli kwa sababu tu mmekuta ipo hivyo, mkakaririshwa hivyo na wala hamna sababu za msingi..!! Haya, unaweza kunieleza kwa nini huli nyama ya mbwa? AU kwanini huli nyama ya punda? AU kwanini huli nyama ya ngedere? etc..!! Nyama zote nilizozitaja hapo juu kuna watu wanakula na hawajapata madhara
 
Huo unaofanyika ni utapeli.

Kuna mahali tulikuwa na kazi fulani Vijijini huko, Sasa na Ugeni wetu asubuhi tukafika kwenye ki center tukaagiza mchemsho na Ndizi...
Usiwe unabeba chochote mkuu hata biskuti acha, kamishina wa mihadarati jana kasema kuna biskuti pamoja na lamba lamba zinatengenezwa kwa kutumia malighafi za bhangi.

Usije ukaruka mkojo ukakanyaga kinyesi halisi.
 
Mkuu tutakufa njaa Sasa, labda kujihami tuwe tunanunua kwenye maduka local ya eneo husika.
 
Kuna siku nilikula mishikaki,wakati natafuna ile ladha yake nikasema mmh huyu atakuwa mbwa asee.

Jamaa muuzaji naye alikuwa makini sana kuniangalia wakati nakula ule mshikaki. Kuanzia siku hiyo Mimi nakula pweza na ngisi tu kwa sababu anaonekana alivyo. Mishkaki hapana kwa kweli.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Ulafi wabongo umewazidi unanunuaje mishikak sehemu isiyoeleweka
 
Mkuu tutakufa njaa Sasa, labda kujihami tuwe tunanunua kwenye maduka local ya eneo husika.
Kwani hayo mangada si ndo yamejazana sana huko kitaa..!!! Unakumbuka kule Zenji kuna muuza pweza alikuwa anaweka VIAGRA kwenye pweza wake?
 
Back
Top Bottom