Moshi: Mfanyabiashara aua kwa bastola Himo

Moshi: Mfanyabiashara aua kwa bastola Himo

Wenda wote walikuwa under influence... Alcohol may be .

Too bad.
 
Samaleko wana jukwaaa! Ni habari iliyozua gumzo katika mji mdogo wa Himo mkaoni Kilimanjaro.

====
Ni mauaji yaliyotikisa mji wa kibiashara wa Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya mfanyabiashara mashuhuri katika mji huo, Kennedy Minja (47) kudaiwa kumfyatulia risasi na kumuua papo hapo, mkazi wa Kilema, Deogratius Lyimo.

Baada ya tukio hilo, inaelezwa mfanyabiashara huyo aliendesha gari lake umbali wa kilomita 27 kutoka mji wa Himo hadi Moshi mjini ambako inadaiwa alijisalimisha kituo kikuu cha Polisi na hadi leo ana siku 18 anashikiliwa polisi.

Ni tukio lilitikisa mji huo kutokana na umaarufu wa mfanyabiashara huyo wa mazao na namna mauaji hayo yanavyodaiwa kutokea, yakihusishwa na mzozo wa dakika chache baina yake na marehemu.

Wananchi wa mji huo hawaelewi kiini hasa cha mauaji, kama kweli ni baada ya tajiri huyo kuwakosakosa kuwagonga marehemu na ndugu yake waliokuwa na pikipiki au la.

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limethibitisha kumshikilia mfanyabiashara huyo pamoja na bastola anayodaiwa kuitumia katika mauaji hayo na huenda akafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia leo kwa tuhuma za mauaji.

Alipoulizwa jana kuhusu ni lini mfanyabiashara huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani, Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo alisema: "Jalada limeshapelekwa kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali, ila nafuatilia kujua ni lini atafikishwa mahakamani, huku kukiwa na taarifa huenda akafikishwa mahakamani kesho.

Awali Kamanda wa polisi mkoani hapa, Simon Maigwa alisema tukio hilo lilitokea saa 4:30 usiku wa kuamkia Mei 17, 2023 katika Barabara ya Himo-Marangu ambako mfanyabiashara huyo anadaiwa kumuua Lyimo.

Aliyeshuhudia afunguka
Richard Mahoo, aliyekuwa amempakia Deogratius, wakitokea Himo kuelekea Kilema alidai walipofika karibu na ofisi ya mbunge wa Vunjo, mfanyabiashara huyo aliingia barabarani bila tahadhari na kutaka kuwagonga na gari lake.

Mahoo alidai kitendo kile kilisababisha Deogratius kushuka kwenye pikipiki na kumfuata na kumuuliza kwa nini anataka kuwagonga, lakini mtuhumiwa alishuka kwenye gari na kutamka maneno kuwa, “nyie mlikuwa mnatakaje”. “Kauli ile ilimkera marehemu na kuanza kushikana na kuanza kupigana. Wakati huo mimi nilikuwa naegesha pikipiki vizuri ili niwafuate, kitendo cha mimi kushuka kwenye pikipiki nikasikia mlio wa bastola, nikachanganyikiwa na kukimbia,"alidai.

Aliongeza: "Nilikimbia kama hatua 200 ndipo nikasimama na kuangalia nini kinaendelea, huyo mwenye gari akapiga tena risasi nyingine kunielekezea mimi, lakini haikunipata, ndipo akawasha gari na kukimbia," alidai Mahoo.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, baada ya milio hiyo ya risasi watu walijitokeza na kumchukua marehemu na kumpeleka Hospitali ya Faraja Himo na walipomfikisha waliambiwa ameshafariki dunia.

Kwa upande wa baba mkubwa wa marehemu, Isaack Lyimo alisema kijana wake alitokea kwenye msiba wilayani Siha akiwa na rafiki yake na walipofika Himo, walichukua pikipiki ya huyo rafiki yake kwa ajili ya kuelekea nyumbani Kijiji cha Kyou, Kilema.

Mzazi huyo alidai walipofika jirani na ofisi ya mbunge wa Vunjo kulitokea kuzozana kati ya mfanyabiashara huyo na mtoto wake baada ya mfanyabiashara huyo kuingia barabarani bila tahadhari na kutaka kuwagonga.

Kulingana na maelezo aliyopewa, katika mabishano hayo walifikia hatua ya kutaka kupigana, ndipo mfanyabiashara huyo inadaiwa alikwenda kwenye gari na kuchukua bastola na kumfyatulia risasi mtoto wake na kumuua papo hapo.

Mwananchi
Msongamao wa mawazo ,afya ya akili..
 
Serikali inacheka na hawa wamiliki wa silaha, inatakiwa mtu kama huyu awe mfano! Adhalilishwe na kuhukumiwa kifo na habari iwe inakuwa reported kwa ukubwa ili kukomesha wamiliki wa silaha kuzitumia vibaya.

Wakati mwingine unatokea ugomvi mdogo tu tayari mtu anakimbilia silaha.
 
Ukiwa kwenye gari ,si arishuka akawafuta,busara ikikosekana kwa tajiri
Hutakiwi kukunjana na tajiri, hata ningekua Mimi nakufyatulia tu kiburi chako peleka kwenu maana wanasema mtu shujaa hupeleka Msiba nyumbani kwao, haya kajitia ushujaa anataka kupambana na mwenye kitu Cha Moto kala vyuma kafa
 
Sijawahi kusikia mtu yeyote anayemiliki silaha kihalali ameua majambazi au wezi.

Mara zote wanaua watu baki tu kwa mbaaali sana namuona Said Mwamwindi.
Kuja jamaa mikoa ya kusini alimuua polisi aliyetoroka Lindo na SMG kwenda kufanya uharifu,polisi alikuwa ni mtu wa Mara,aliliwa ya kichwa na ubongo ukamwagika,
 
Ukiwa na siraha muda wote unatamani ukorofishwe tuu hapo jamaa wa gari ndio alikua na makosa harafu tena yeye ndio kaua kwa sababu ana siraha na kukimbilia polisi hasira za Kijinga ni hasara wakati angewaomba msamaha tu hapo yangeisha kabisa na mambo ya kesi ya Serikali isingekuwepo tena...
 
Ukute Sasa hivi mfanya biashara anawaza kwani pale ningeomba samahani ningepungukiwa nini?

Sasa pesa za marejesho zinaenda kuendesha kesi, kuhonga familia na polisi.
 
Ukute Sasa hivi mfanya biashara anawaza kwani pale ningeomba samahani ningepungukiwa nini?

Sasa pesa za marejesho zinaenda kuendesha kesi, kuhonga familia na polisi.
Ogopa ugomvi ukiwa umelewa mbaya zaidi uwe na silaha, utajuta umeshafanya tukio.
 
Aisee! Kuna umuhimu wa kudhibiti hasira zetu. Maana huu mzozo ulikuwa unaepukika kabisa. Pia nina waswasi kama mtuhumiwa wa mauaji ndiye chanzo cha hiyo ajali.

Na hii inatokana na ukweli kwamba waendesha pikipiki wengi ndiyo wamekuwa na hii tabia ya kutochukua tahadhari, pale waingiapo barabara kuu.
Mtu ana ml 100 tu tena zipo Bank anaenda kunywa pombe na bastola. Hapo ukichunguza wote walikuwa kwenye state ya ulevi wa kupindukia
 
Sijawahi kusikia mtu yeyote anayemiliki silaha kihalali ameua majambazi au wezi.

Mara zote wanaua watu baki tu kwa mbaaali sana namuona Said Mwamwindi.
Wanasema kwamba kwenye ulimwengu wa crime, bunduki uliyoifanyia uhalifu kwa kukatisha uhai wa mtu hakikisha unaitupa au kuiharibu kwa namna yoyote ile.. sijawahi kufahamu kujua Nini main reason katika hili.. [emoji848]
 
Back
Top Bottom