Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Wagombea wa CHADEMA Moshi wakataliwa kupokelewa fomu zao na Mkurugenzi.
======

Mkurugenzi amegoma kupokea fomu baada ya tuhuma za awali kwamba sio halisi na kutaka kabla wahusika hawajazirudisha wakathibitishe polisi kama ni halisi ama La.

Baada ya katibu wa CHADEMA kuhoji iwapo vyama vyote vinaenda polisi kuthibitisha, amejibu yeye aliemtuhumu na wote waliomtuhumu ndio wanatakiwa kwenda polisi kuzithibitisha kabla hawajazileta kwake.

Pia katibu wa CHADEMA alilalamikia kuwa na risiti za aina mbili kwa wagombea wa CCM na CHADEMA ambapo risiti za CHADEMA zimekuwa printed kwenye computer ilhali za CCM ni stakabadhi ya halmashauri.

Kuhusu hilo mkurugenzi, amemtaka kuwasilisha kwa maandishi malalamiko yao na yeye atakaa na wataalam kuangalia kipi ni kipi lakini amesema uko utata, zipo ambazo ni stakabadhi kama za mahakama, nyingine za mfumo na nzuri ni ya stakabadhi lakini wakitaka majibu wawasilishe malalamiko yao.

Pia mwenyekiti amelalamika suala la risiti ya mgombea ubunge kuandikwa ni ya mgombea udiwani, mkurugenzi ametaka wayawasilishe wamalizane.


=====

Kwa upande wake mkurugenzi amesema ametoa fomu halali na CHADEMA wakaandika barua na kumpelekea wakimtuhumu amewapa fomu zisizo halisi na baadae kwenda polisi. Ikabidi awaandikie kwamba hilo suala halina shida lakini kwa kuwa wameenda polisi, yeye hana uweza wa kutambua kitu 'fake' hivyo watafute mamlaka yenye weledi wa kutambua hivyo asingeweza kuzipokea.




Huyu sio aliyeleta maafa kwa the late Acquilina? Au ni pacha wake?
 
Lililopo..

Nimekupa fomu kisha ukasema ni feki.

Kisha ukaijaza na kuirudisha...so far does it make sense to you sir?

Mimi kama fomu niliyopewa ingekuwa feki ningeirudisha bila kuijaza na kudai iliyo halali maana kama naijua feki basi iliyohalali naijua vema.

Ukinirudishia fomu uliyoijaza huku uliita feki kuna mengi...kwanza ulikurupuka kunichafua. Pili, je nitajibu nini kama fomu uliyoirudisha kweli ni feki na ni mtego, niliyokupatia ilikuwa halali hivyo ulifanya mchezo wa kuset minds za watu kwamba nimekupq feki ilihali ilikuwa halali...sasa wakati wa kurudisha unarudisha feki.
Una akili zaidi ya kuku mkuu
 
Wakurugenzi wanatengeneza cv kwa ajili ya awamu ijayo.
 
mi nadhani wapinzani wajitoe tu wabaki CCM peke yao si ndio wanachotaka
 
Sijui viongozi wa chadema wote akili zao zinafanana yani amepewa fomu akasema ni feki Sasa hiyo feki unarudishaje wakati haijathibitishwa??
Nyumbu wanatengeneza matatizo halafu wake kulialia humu jukwaani. Kama walipewa fomu wakasema feki wanaenda polisi kulalamika Sasa Leo wanarudishaje bila uthibitisho wa polisi? Na hapo zitathibitishwa keshoooo!

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
kutokana na wimbi la wagombea wa upinzani kuwindwa na shetani kama swala ili watekwe au wauliwe huku viongozi wa dini na tume wakikaa kimya sababu wagombea wa ccm hawatekwi ni jukumu lao sasa wagombea wa upinzani kujihami binafsi na kurekodi matukio yote live watumie kofia,miwani,earphone, nguo zenye camera 360 degree warekodi kila kitu huku wakitembea na watu waliofully armed ili kujilinda endapo watafamiwa waweze kutoa fundisho ili wakamsimulie shetani aliyewatuma na sio kulalamika mnatekwa tekwa hovyo hovyo kirahisi tu kumbukeni mpo mawindoni sababu wanajua awatoboi kwenye sanduku.Toeni funzo kama wananchi wa Ukara tembeeni hata na asidi atakaekugusa tu anayo ndo njia pekee ya kujihami,hatutaki watu wa kulialia safari hii.Rekodini matukio yote mrudishapo formu kama ushahidi na kuyarusha live watz wayaone. Pia tembeeni na kopi za fomu kwenye bahasha ifananoyo na ya nec ili kuwaadaa waporaji wakija wapore hizo kopi huku halisi mkiwa mmezificha mnapopajua wenyewe. Tumieni kanuni namba 9 ya shetani mtu akikufanyia ushenzi mfanyie mara kumi yake mpaka ajiulize huyu ni mtu au.Endeleeni kuwa wajinga mtatekwa hadi mchakae
 
kama mkurugenzi huwezi tambua fomu feki na halali hali we ndo unazitoa ufai kuwa ofisini,tuwaambie tu wakurugenzi wao ndo wanataka kuvunja amani yetu nalaana ya damu zetu hazitowaacha salama
 
Hebu mtaalam tusaidie kwanini wagombea wa ccm wamepewa risiti ya halmashauri na wengine wasipewe wapewe ya tofauti?

Kwanini risiti za wagombea ubunge zimeandikwa za wagombea udiwani?

Acheni kujifanya mna akili sana kuliko wengine
Muda mwingine ficheni upumbavu
Kwani chadema hamjui kusoma? Wewe unapewa fomu ili ugombee ubunge halafu fomu imeandikwa ya kugombea udiwani nawe unaijaza ukiulizwa mbona ni fomu ya udiwani si ubunge unasema unaonewa!

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Bila hawa wakurugenzi uchwara kushikishwa adabu ,hawatajifunza.
 
Utawasikia wanasema TUNATEKELEZA
Ahahahahh. Waoga na wepesi sana hawa jamaa I see. Sikuwahi kuwaza kwamba Sisiemu ni wepesi namna hii. Tangu lini polisi wakawa dio wathibitishaji wa fomu zawagombea?
 
Bottom line, kwa nini Chadema wanapenda kurejesha fomu siku ya deadline? Walisubiri nini siku zote hizo?
 
Kivipi? Mgombea anaenda kuchukua fomu katika sehemu iliyopangwa kutoa fomu husika. Mgombea hajui fomu zinafananaje ili kutofautisha kati ya fomu halali na fake. Sasa iweje tena Chadema wajitengenezee matatizo!? 😳

Matatizo mengine Chadema wanajitengezea wenyewe.
 
Back
Top Bottom