Moshi: Mlinzi aliyehukumiwa kifo kwa Mauaji ya Mwanafunzi wa Sekondari ya Scolastica aachiwa huru

Moshi: Mlinzi aliyehukumiwa kifo kwa Mauaji ya Mwanafunzi wa Sekondari ya Scolastica aachiwa huru

Binafsi ningeenda tafuta uchawi mkali Sana[emoji15][emoji15]

NB; mtoto anauma sana, ma bachelor hamuwezielewa


Kesi Kama hii Imani yako ndio mchawi mkali.


Kama wewe ndio mzazi na kweli hapa uhai wa mtoto wako umedhulumiwa basi Imani yako ya dhati juu ya kile unachotaka kufanya kwa kulipa kisasa ndio nguzo yako.

Namaanisha Imani sio Dini.
 
Kwanini wamtupe? Maamuzi mengine ya kijinga sana.

Na hapa kumtupa ndipo kosa lenyewe lilipo.


Ina maana hao Judges wote watatu wameshindwa kutambua nia ovu ya kuficha mwili na kuficha chanzo cha kifo hapo awali?

Kama waliwafunga wale waliokubaliana na kushirikiana kuficha mwili huyu mlinzi ambae ni chanzo cha mauti anakosaje?

Hata Kama ni mauaji ya bahati mbaya, ndio maana sheria zikawepo ili kutoa funzo kwa wengine Kama yeye wanaopenda ku act at an impulse badala ya patience and logic.

Halafu hilo pigo moja la ubapa wa panga lilikua na force kubwa kiasi gani na lilipigwa maeneo gani? Mpaka pigo moja kupelekea maut?

Kimo cha huyo mlinzi na huyo marehemu vilikua na utofauti ama ulinganifu kiasi gani?

Kama marehemu aliruka ukuta yawezekana sio Mara yake/yao ya kwanza, which means mlinzi alikua familiar na ujinga huo kutoka kwa wanafunzi, sasa katika hili tukio lililozaa mauti mlinzi hakujua kwamba ni wanafunzi pia? Kimo cha aliyeruka hakikumuonyesha kwamba ni mdogo/mfupi?


Maybe alikufa kwa mshtuko baada ya kubamizwa na ubapa wa panga na ukizingatia adrenaline ilikua juu muda huo (?) Report ya postmortem ilisemaje?


Sipingi maamuzi ya Mahakama ila yamenishangaza.

Marehemu aendelee kupumzika kwa amani mahali pema, wazazi poleni sana.
 
Hapana. Mahakama haina kosa. Japo siwezi kusema imetenda haki. Wenye kosa ni waliofungua mashtaka ya kuua kwa kukusudia ilhali uhalisia ni mauaji ya bila kukusudia. Kwa maoni yangu ilitakiwa hati ya mashtaka iwe ya kuua bila kukusudia.

Upande mmoja uko sahihi.


Lakini kwenye rufaa ndio maana kuna jopo la watu watatu, kwa maana zaidi ya makaratasi basi uelewa, maarifa baina yao, ujuzi wao kwa pamoja, vyote hivi vinatumika.

Sasa inakuwaje wote wameshindwa kung’amua humanity kwenye sheria zao?

Kwamba hawajaona non recovery loss iliyopata family ya huyo mtoto?

Kwamba hawakufikiria kutoa funzo kwa Taasisi zozote zenye mamlaka ya kutoa huduma kwa jamii Kama hizi shule za private zenye maatukio Kama haya?

Kama hati ndio tatizo basi wangeagiza kesi ifutwe na kuanza upya kwa kuagiza hati mpya ya mashtaka?

Tukubali kwamba maslahi ya kifedha yameshinda maslahi ya kibinaadam nyakati hizi?
 
Walichokifanya ni kibaya kutupa mwili wangejitetea kuwa walidhani ni kibaka green acres ya mbezi kwa wasichana mie domitory aliingia mtu na kisu akamkita mtu aliyeagiziwa
 
Ukiwa mzazi ukisoma taarifa kama hizi, na una mtoto anayesoma shule za kulala, unasisimka.

Mungu wewe ndiye hakimu wa haki.

Hakika mkuu, nakazia tena mtoto anauma yaani akiumwa homa unahaha sembuse kuuawa!!!

Tazama hata mnyama anavyopagawa dhidi ya mtoto wake akihisi anadhurika!😳😳

NB: mtoto anauma sana hasa akiwa mdogo, ma bachelor hamuwezi nielewa hata nikiwaelewesha 😳
 
Na huyu OCS Juma alibaki salama kwenye utumishi wa umma??

"Mlinzi alishauri mtu yule asiyefahamika awahishwe hospitali kwani anaweza akawa bado yuko hai lakini Mkuu wa Shule, kwa kuhofia usumbufu ambao ungejitokeza, akashauri mtu yule atupwe kwenye Mto Ghona ulio umbali wa mita zaidi ya 300 kutoka ilipo shule ya Scolastica. Mwalimu Labani, akishirikiana na mlinzi, wakatekeleza ushauri ule huku mwenye shule akiwaambia mambo mengine yote wamwachie yeye."

"Mwenye shule akawasiliana na Inspekta Idd Juma ambaye alikuwa ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Himo. Haikujulikana walichowasiliana lakini mnamo Novemba 10, 2017, polisi wa Himo, wakiwa na mkuu wao wa kituo, walienda mto Ghona na kuuopoa mwili ule na kuupeleka Hospitali ya Mawenzi. Kwenye miamala ilionekana Mzee Shayo alimtumia kiasi cha Sh500,000 Mkuu wa Kituo cha Himo."

Fortunatus Buyobe, mwandishi wa habari za uchunguzi
 
Back
Top Bottom