Kwanini wamtupe? Maamuzi mengine ya kijinga sana.
Na hapa kumtupa ndipo kosa lenyewe lilipo.
Ina maana hao Judges wote watatu wameshindwa kutambua nia ovu ya kuficha mwili na kuficha chanzo cha kifo hapo awali?
Kama waliwafunga wale waliokubaliana na kushirikiana kuficha mwili huyu mlinzi ambae ni chanzo cha mauti anakosaje?
Hata Kama ni mauaji ya bahati mbaya, ndio maana sheria zikawepo ili kutoa funzo kwa wengine Kama yeye wanaopenda ku act at an impulse badala ya patience and logic.
Halafu hilo pigo moja la ubapa wa panga lilikua na force kubwa kiasi gani na lilipigwa maeneo gani? Mpaka pigo moja kupelekea maut?
Kimo cha huyo mlinzi na huyo marehemu vilikua na utofauti ama ulinganifu kiasi gani?
Kama marehemu aliruka ukuta yawezekana sio Mara yake/yao ya kwanza, which means mlinzi alikua familiar na ujinga huo kutoka kwa wanafunzi, sasa katika hili tukio lililozaa mauti mlinzi hakujua kwamba ni wanafunzi pia? Kimo cha aliyeruka hakikumuonyesha kwamba ni mdogo/mfupi?
Maybe alikufa kwa mshtuko baada ya kubamizwa na ubapa wa panga na ukizingatia adrenaline ilikua juu muda huo (?) Report ya postmortem ilisemaje?
Sipingi maamuzi ya Mahakama ila yamenishangaza.
Marehemu aendelee kupumzika kwa amani mahali pema, wazazi poleni sana.