Moshi: Mlinzi aliyehukumiwa kifo kwa Mauaji ya Mwanafunzi wa Sekondari ya Scolastica aachiwa huru

Dogo alitoroka Shule akaenda anakokujua mwenyewe. Aliporudi aliruka ukuta ili aende bwenini kulala, Mazingira yalikuwa ya giza lakini pia sheria ni kuwa lazima uwe na uniform ya shule muda wote uwapo nje ya shule- Mwizi ana alama! Askari alikuwa anajiami kwani alikuwa anamshambulia mtu asiyejulikana alieruka ukuta wa shule usiku na kwenye giza nene.Marehemu alitakiwa ajitambulishe na pengine ata kumwita mlinzi kwa jina lake ingesaidia kutoshambuliwa zaidi mpaka ikapeleka kifo chake. (HAYA NI MAWAZO YANGU SIO UKWELI WOWOTE NISINUKULIWE VIBAYA)
 
Nadhani mwanafunzi alikuwa anaenda disco ( adolescence / Nyege). Mlinzi hakuwa na nia ya kuua bali alitaka kukamata aliyemdhani ni jambazi au mbakaji labda, ndio maana hakutumia bunduki (kama alikuwa nayo).
Dogo alitakiwa ajitambulishe na ata kumwita jina Kamanda! Uenda angepigwa ubapa mmoja tu na angeishia suspension na angerudi shule.
 
Dogo alitakiwa ajitambulishe na ata kumwita jina Kamanda! Uenda angepigwa ubapa mmoja tu na angeishia suspension na angerudi shule.
Yeah, ila adhabu ya miaka minne kwa manslaughter ni ndogo, walau mitano
 
Mtu kukufia ghafla sio rahisi jamani,we unavyosikia mtu mpaka anamchoma kwa gunia mbili za mkaa mchezo,mara mwingine anabomoa sakafu anazika ndani na mwingine anaenda kutupa huko mtoni,kifo cha ghafla acha kabisa.
Mungu amrehemu aendelee kuwafariji wazazi wake na waloua bila kukusudia awasamehe kwakweli
 
Title ya uzi na uzi husika ni vitu viwili tofauti.

Sio kwamba imemuachia huru, hapana ni kuwa rufaa yake imekubaliwa nusu ila wakamrudisha kwenye kosa la kuua bila kukusudia, kisha kwenye adhabu wazee wakajikuta imeshakamilika.

Sasa swali la msingi ni je, Mahakama ya rufaa inaweza kuwa mahakama ya kusikiliza kesi mpya? trial court jibu la awali kabisa ni hapana, sasa swali ni je, kilichofanyika ni marejeo, mapitio au kusikilizwa kesi trial?

Huu mjadala niishie hapa, ntaend kusoma zaidi na zaidi
 
Oya kwa yoyote humu aliyekuria / kuishi mazingira Yale ya Himo na anaepaelewa kule mto Ghona hadi kule nyuki hd kipande cha mieresini tujuane, binafc kitambo sana pande zile [emoji3] karibu na Shule ya scolastica kuna hospitali ya Dokta wangu pendwa Dkt. Lazaro I wish km mpk Leo Bado yupo site ile aisee

Naona Himo panaitwa mji siku hz haha,
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]msipeleke watoto wenu scolastica
Watauawa halafu kunakuwa hamna kesi
Msijesema hatujawaambia[emoji1787][emoji1787]
Haya[emoji108][emoji108][emoji848]
Bwana Shayo pesa anazo bhn
 
Kwanini wamtupe? Maamuzi mengine ya kijinga sana.
Kule kumtupa ndiko kulikowafunga wenzake adhabu ndogo.

Pia katika hukumu huangaliwa zaidi kiini cha kosa na kuthibitisha bila shaka utendwaji wake.

Kukimbia, kuficha ushahidi huwa haviangaliwi sana kwa sababu kutapatapa kukwepa mikono ya sheria ni jambo linalofahamika na linaloweza kufanywa na mtu yeyote.
 
Nadhani mantiki (logic) imefanya kazi yake. Maana kesi mpya ya ‘kuua bila kukusudia’ ikisikilizwa, there can be only one outcome, regardless ya hukumu, ni kwamba the guy walks free. Akishindwa kesi na kuhukumiwa adhabu stahiki (miaka 4) basi atakuwa amashamaliza adhanu yake (time served), hivyo he walks. Akishinda kesi, he walks.

Ila hapa kuna swali la kujiuliza, miaka mi4 ni adhabu tosha kwa kosa kubwa kama hilo? Hivi si ilibidi apigwe miaka kama 20 hivi au? Sheria inasemaje?
 

Hio kesi rushwa imetumika sana.

Huyo Shayo sio mwenye shule.
shule bi ya huyo mama anaitwa Scolastica.

Scolastica ni mpango wa kando wa wa mzee shayo. Maana shayo ana mke kabisa wa ndoa.

Hiyo shule chini ya mwl mkuu Michael Chapombe (mkenya) na huyo mwal Laban (mkenya) nadhani ni mwl wa nidhamu, ina kesi lukuki kupiga na kuumiza wanafunzi kituo cha polisi cha himo. Kimsingi kupiga wanafunzi na kuumiza ni kawaida yao hado ilipotokea huyo mwanafunzi aliekufa. Thanks kwa mzazi wa mtoto (makundi) alikuwa na msuli, vinginevyo ilishakuwa imepangwa kuwa mtoto ametoroka shule na uongozi wa shule hawajui alipo.

Kimsingi alietakiwa kuwa ndani ni huyo mama sio shayo. Huyo mama anaishi hapo hapo shule na mwanae kiongozi wa shule. Anaishi mira chache karibu na geti, na shayo mara nyingi huishi kwny hotel zake. Na mama ndiyo final say, kwahiyo kama kuna maamuzi ya kuufukia mwili, basi yalitoka kwa mama sio shayo. Nadhani pesa aliyotumia mama kuzima hiyo kesi na kupindisha, ndiyo ilifanya Shayo akalale ndani badala yake.
 
Naona na maji ya Kilimanjaro mkononi, hawa jamaa wa mkoa huu ni wabaguzi sana, huwezi kuta uhai maisha wala afya katika mkoa huu
 
Kama tukitumia mantiki, Mahakama ya Rufaa haina mamlaka au uwezo wakusikiliza trial uwezo wake ni kisikiliza Rufaa, kufanya marejeo na mapitio pia.

Kama ni kesi kuanza kusikilizwa upya wanatoa amri ya kesi ikasikilizwe upya retrial hivyo ndivyo sheria inataka wafanye.

Hiyo ni sheria Mkuu, kama ni wakili utaelewa ninachojaribu kukiwaza ila kama si wakili, basi Mkuu sheria huwa inatasiriwa sio kuja na dhana iliyo nje ya hiyo sheria.
 
Wakati tunamuuliza kicheche kwanini aliua kuku bila hatia ........swali ni kwanini pia kuku Allenda kwenye mitaa ya kicheche bila sababu
 
Logic na common sense ya kufanya trial mpya huku outcome ikiwa ile ile (walks free) regardless ya verdict (guilty/ innocent) itakayotolewa ni ipi?

Hapo nimesema imetumika mantiki (logic).
 
Logic na common sense ya kufanya trial mpya huku outcome ikiwa ile ile (walks free) regardless ya verdict (guilty/ innocent) itakayotolewa ni ipi?

Hapo nimesema imetumika mantiki (logic).
Sheria haipo hivyo Mkuu, ukipata muda kaisome. Walitakiwa kuelekeza na kuishia hapo sio kuwa trial court hawana hayo mamlaka.

Kuendelea mbwle bila kuwa na mamlaka ni kutwngeneza sheria mbaya hasa kwa Mahakama ya juu.

Kama ni layman ni ngumu sana kuelewa hili ila ndio lilivyo. Logic hata kama ikiwa ina logic kiasi gani kama sio utaratibu ni ubatili tu.
 
Mahakama imetumia mantiki (Logic). Elewa basi, sheria huwa inatoa mwanya kwa Logic kutumika, na imetumika.

Assume hilo unalosema ni sheria linefanyika, ukiacha kupoteza muda na pesa, kuna utofauti gani na kama halikufanyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…