Ninja assasin
JF-Expert Member
- Jul 2, 2018
- 2,512
- 5,848
mpwayungu village kweny one and two tupe muongozo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawaelewi Kwa kua hawajitambui ila inaumiza hata Mimi ni mzazi ukiniumizia mwanangu lazima tupambane aseeehhh!!!Wakikuelewa nahama nchi
Ahsante kiukweli uko sahihiHongera ni vizuri kuipenda kazi yako. Hamzeekagi
Kwanini niibie siri iliyopo kati ya ualimu na kutokuzeeka.
Sijui kila shule iwe na askari wa kuwalinda wanafunzi dhidi ya ukatili wa waalimu?Utata umeibuka kuhusu kifo cha mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari iliyoko Pasua, Manispaa ya Moshi, Walter Ebenezer, anayedaiwa kushambuliwa kwa mateke kwenye mbavu na mwalimu wake kisha kupewa adhabu ya kupiga ‘push up’.
Kutokana na kifo hicho, ndugu wa mwanafunzi huyo wamejitokeza hadharani wakiliomba Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kufanya uchunguzi wa kitabibu kubaini sababu za kifo hicho.
Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo kabla ya kupoteza maisha Februari 19 mwaka huu kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru) alikokuwa anapatiwa matibabu, alikuwa mwanafunzi wa bweni wa shule hiyo.
Akizungumzia tukio hilo jana, mama mdogo wa marehemu, Mkazi wa Sakina-Arusha, aliyejitambulisha kwa jina moja la Neema, alidai kuwa kabla mwanafunzi huyo hajafariki dunia, aliwaambia kwamba alipigwa na mwalimu wake mateke kwenye mbavu na aliambiwa apige push up kutokana na kosa ambalo hakuliweka wazi.
"Baba mzazi wa marehemu, alipigiwa simu akaambiwa akamchukue mtoto maana anaumwa sana. Alipokwenda shuleni kumchukua mtoto, alimleta Mount Meru kwa ajili ya matibabu.
Alipofikishwa Mount Meru, alipatiwa matibabu na aliwekewa oksijeni. Baadaye mtoto alipoteza maisha. Lakini tulikwenda kufuatilia polisi. Tulianzia Central Arusha (Kituo Kikuu cha Polisi) na baadaye tukaelekezwa twende Central ya Moshi mahali ambako tukio ndiko lilitokea.
"Tulimwelezea OCD Moshi (Mkuu wa Polisi wa Wilaya) tukio zima na akachukua gari na askari na wakaenda shuleni, hawakumpata mwalimu, wakaambiwa warudi siku iliyofuata.
"Niliwauliza polisi kama tunaruhusiwa kuuzika mwili, nikaambiwa 'hapana!', tunatakiwa kusubiri mpaka wafanye uchunguzi wao," alidai.
Hata hivyo, mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliendelea kudai kuwa walipokwenda Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, waliambiwa wanatakiwa wauzike mwili huo.
"Tunashangaa tutazikaje wakati Central Moshi wametuzuia na ndio ambako tukio limetokea? Tunazikaje huo mwili, mbona wanafamilia tunachanganywa? Tunazikaje wakati hatujajua mwafaka wa ndugu yetu amekufakufaje? Tunahitaji haki, uchunguzi ufanyike," alisisitiza.
Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi (ACP) Simon Maigwa, alikiri jeshi hilo linamshikilia mmoja wa walimu wa shule hiyo (hakumtaja jina) kwa ajili ya uchunguzi.
"Tumefungua jalada la uchunguzi. Kwa sababu ni malalamiko, ni jukumu letu kumshikilia ili tujiridhishe. Timu yangu ya makachero imekwenda kufanya postmortem (uchunguzi wa kitabibu) ili tujiridhishe kwamba ni kweli aliuawa au alikuwa anaumwa?
"Tunachunguza lakini hatuwezi kusema moja kwa moja. Sasa kumshikilia ni jukumu letu, kwa sababu kuna malalamiko juu yake. Tunasubiri madaktari, watuambie kwamba chanzo cha kifo chake ni nini.
"Makachero wetu wamekwenda huko (Hospitali ya Mount Meru) kujiridhisha kwanza na hiyo taarifa, kama kweli ipo na kama ipo, basi washirikiane na ndugu ili 'ku-clear' (kumaliza) hiyo doubt (shaka). Bado uchunguzi unaendelea, tunamshikilia kwa ajili ya uchunguzi na sio kwa sababu ya mauaji," alisema.
Chanzo: Nipashe
Ukiwaambia wanasema unawanangaWalimu jiwekezeni kwenye harakati za kutetea maslahi yenu ikiwemo posho achana na toto la mtu,
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]mwambaa huyu hapaaMwalimu kama ndio kaniulia mtoto lazma nimvizie nimtie kichapo hadi akate moto nayeye. Undava undava tu
Nani kakufuata PM we mgogo[emoji16][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Tukiswasema Wanatufata PM
Walimu badala wapambane,wawabane serikaliWalimu wenyewe wa siku hizi wanakaa vijiweni wakivuta bangi na wanafunzi wao heshima ya mwalimu shuleni itatoka wapi?
Siku hizi hakuna kufukuza shule ila Sio sababu ya kupiga mangumiMtoto kakosea nini hadi umpige mateke ya mbavu. Kama umemuonya hasikii mfukuze shule
[emoji3][emoji3][emoji3] kucheka na watoto mda wote ni dawa sanaKwanini niibie siri iliyopo kati ya ualimu na kutokuzeeka.
Kama ni hilo tu nitajitahidi kucheka nao[emoji3][emoji3][emoji3] kucheka na watoto mda wote ni dawa sana
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mi nadeal na wazazi wao nna no za simu za wazazi au walezi wao,nahakikisha na wao wa no yangu pia so mwanafunzi hajasahihisha nampigia simu mzazi wake ,kagua daftari za kijana wako haiwezekani maths asisahihishiwe siku 3 zoteee,wakifeli nawapa adhabu za kujenga wanapanda bustani,kulima n.k nikichapa wanashangaa[emoji4][emoji4][emoji4][emoji1][emoji1][emoji1]!!! mnoooooooMimi nna jamaa yangu mwalimu akitoa exercise darasani akija kesho yake akiulizia daftari zikusanywe hata zikikusanywa daftari 2 hao wengine 38 wawe hawajakusanya hana hata habari nao yanini kujitafutia matatizo umpge mtoto wa mtu umuue upoteze kazi yako na jela juu yy ata komaa na 2 tu wanaopenda kusoma.
[emoji3][emoji3][emoji4][emoji4]Cheka na watoto utafurahia mnoooKama ni hilo tu nitajitahidi kucheka nao
Sawa madam reymage nitalifanyia kazi[emoji3][emoji3][emoji4][emoji4]Cheka na watoto utafurahia mnooo
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Afisaelimu sekondari huko moshi manispaa ni mtumishi mzembe katika historia asipoondolewa haraka kuna maafa mengi mtayasikia.Utata umeibuka kuhusu kifo cha mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari iliyoko Pasua, Manispaa ya Moshi, Walter Ebenezer, anayedaiwa kushambuliwa kwa mateke kwenye mbavu na mwalimu wake kisha kupewa adhabu ya kupiga ‘push up’...