emanuel goa
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 522
- 585
Mbona habari yenyewe unaandika unaichanganyachanganya huenda ww ndio ulisababisha mtuhumiwa aachiwe kama ulikiwa mmoja wa mashahidiTukio hili la kusikitisha lilotokea mwezi uliopita katika Kata ya Machame Narumu huko wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro limeleta sintofahamu katika familia ya kijana huyo ya watuhumiwa kuachiwa huru hata kabla ya upelelezi na kesi kufikishwa Mahakamani.
Wanafamilia wa kijana huyo wamesikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi Kituo kikuu cha Bomang'ombe kuwaachia huru vijana hao ilihali ripoti ya Daktari inaonyesha kuwa ni kweli kuwa kijana huyo kaingiliwa na pia kijana huyo kukiri na kuwatambua watuhumiwa wote waliohusika kumfanyia kitendo hicho.
Baadhi wakazi wa kata hiyo pamoja na wanafamilia wa kijana huyo wamesikitishwa na kitendo hicho na kusema kuwa wamekosa Imani na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa vijana hao kutoa rushwa Polisi na hivyo kuachiwa huru.