Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Kama siamini vile sababu ya watu kukanyagana kiasi cha kufikia kuuana!
Poleni wafiwa. Ngoja nisubiri maelezo ya kina.
 
We ndo zuzu kweli toka lini Mungu akafanya jambo kwa bahati mbaya. Yaani Mungu aruhusu watu wafe wakiwa kwenye eneo takatifu tena kwa nabii na mtume wake? Huyo ni nabii wa uongo na tapeli.

Mungu mwenyew anasema", Njooni nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha". Kwahiyo hapo ndo kawapumzisha au? Pigo la Mungu huja siku usioizani na siku yake ndo leo. Huko nyuma Mungu alimwacha pengine ili atubu,bahati mbaya akawa jeuri na hayo ndio matunda yake. Bulldozer ni tapeli,na mchawi km ilivyo kwa TB Joshua,Mzee wa upako, Gwajima,Prophet Bushir na Geodavie.
Nilicho gundua watu walio wengi humu Jf mnapenda kuongelea vitu kimihemko sana na porojo za kuchangamsha akili kuliko kuongelea uhalisia ambao una ukweli wa kutosha ambao haupendwi wala kusikilizwa na watu wengi wajinga,
Mara nyingi Mwamposa amkekuwa akiandaa makongamano ya kukanyaga mafuta Dsm na watu wengi kuponywa na kokote aliko enda halijawahi tokea tatizo lolote iweje Moshi wakati wa kukanyaga mafuta bahati mbaya wengi wakadondoka na kukanyagana, mtu anatokea aliko toka anakwambia "wajinga ndio waliwao" mnamkosea sana Mungu,
Jifunzeni kufanya research vya kutosha kabla ya kutenda wala kuongea lolote, kuna mtu ame-reply eti mafuta ya upako ni kama hirizi tu, na yametajwa hadi kwenye biblia na matumizi yake ila kwakuwa wengi wanapenda mihemko na porojo kuliko ukweli basi ni tatizo kwenye jamii,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:

Watu 20 (watu wazima 18 na watoto 2) wamepoteza maisha mjini Moshi Kilimanjaro jioni ya leo, baada ya kutokea kukanyagana kwenye kusanyiko la kidini, wakati umati wa watu ukigombea kukanyaga eneo yalipomwagwa mafuta yaliyosemwa kuwa ya upako toka kwa Mhubiri Boniface Mwamposa.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.

Chanzo: Mwananchi
Kumbe wachagga mbumbumbu namna hii

Nabii kawapiga, ujinga Huu.... Hakuna, hakuambiwa na wasaidizi asitishe watu wanakanyagana, hana ushers? Mie ningekuwa na mamlaka naanza msweka ndani yeye!
 
Nilicho gundua watu walio wengi humu Jf mnapenda kuongelea vitu kimihemko sana na porojo za kuchangamsha akili kuliko kuongelea uhalisia ambao una ukweli wa kutosha ambao haupendwi wala kusikilizwa na watu wengi wajinga,
Mara nyingi Mwamposa amekuwa akiandaa makongamano ya kukanyaga mafuta Dsm na watu wengi kuponywa na kokote aliko enda halijawahi tokea tatizo lolote iweje Moshi wakati wa kukanyaga mafuta bahati mbaya wengi wakadondoka na kukanyagana, mtu anatokea aliko toka eti "wajinga ndio waliwao" mnamkosea sana Mungu,
Jifunzeni kufanya research vya kutosha kabla ya kutenda wala kuongea lolote, kuna mtu ame-reply eti mafuta ya upako ni kama hirizi tu, na yametajwa hadi kwenye biblia na matumizi yake, Muogopeni Mungu,
Kama siyo mmoja wa wanufaika basi acha kushabikia ushirikina na utapeli wa baadhi ya hao wanaojiita manabii na mitume wajasiriamali kupitia mgongo wa dini.
 
Nilicho gundua watu walio wengi humu Jf mnapenda kuongelea vitu kimihemko sana na porojo za kuchangamsha akili kuliko kuongelea uhalisia ambao una ukweli wa kutosha ambao haupendwi wala kusikilizwa na watu wengi wajinga,
Mara nyingi Mwamposa amekuwa akiandaa makongamano ya kukanyaga mafuta Dsm na watu wengi kuponywa na kokote aliko enda halijawahi tokea tatizo lolote iweje Moshi wakati wa kukanyaga mafuta bahati mbaya wengi wakadondoka na kukanyagana, mtu anatokea aliko toka eti "wajinga ndio waliwao" mnamkosea sana Mungu,
Jifunzeni kufanya research vya kutosha kabla ya kutenda wala kuongea lolote, kuna mtu ame-reply eti mafuta ya upako ni kama hirizi tu, na yametajwa hadi kwenye biblia na matumizi yake, Muogopeni Mungu,
@I am Bless: Usiseme kwamba watu wengi wanakurupuka bali jiulize na fanya kuushirikisha vyema ubongo wako.

Iweje mahosptilani wagonjwa ni wengi na kama hawa wanaojiita manabii wanauwezo wa kutibu kwa nini watu waende hospitali badala ya kwenda kwenye haya makanisa?.

Kwa nini watu wahangaike kufanya kazi ilihali wakienda kwa hao mitume wanafanikiwa kupata mkate na kuendeleza familia zao?

Kwa nini watu wahangaike na matatizo ambayo wakipakwa mafuta au maji hayakomi ila inakuwa ni utumwa wa kila leo unataka upate mafuta hayo au maji hayo?

Kwa nini hamtaki kukubali ukweli kwamba hawa sio manabii wa ukweli wameweka mbele maslahi ya wao kuwa na miujiza ambayo ukiifikiria kwa undani zaidi haieleweki?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ndo zuzu kweli toka lini Mungu akafanya jambo kwa bahati mbaya. Yaani Mungu aruhusu watu wafe wakiwa kwenye eneo takatifu tena kwa nabii na mtume wake? Huyo ni nabii wa uongo na tapeli.

Mungu mwenyew anasema", Njooni nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha". Kwahiyo hapo ndo kawapumzisha au? Pigo la Mungu huja siku usioizani na siku yake ndo leo. Huko nyuma Mungu alimwacha pengine ili atubu,bahati mbaya akawa jeuri na hayo ndio matunda yake. Bulldozer ni tapeli,na mchawi km ilivyo kwa TB Joshua,Mzee wa upako, Gwajima,Prophet Bushir na Geodavie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe nawe ni kipofu, hujui hata kuchambua kati ya pumba na mchele. Mungu akurehemu bure.
 
Back
Top Bottom