Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Historia hujirudia. Watu wangu wanakufa kwa kukosa maarifa na hivyo kudaganywa na wajanja. Alikuwepo Kibwetere akawaponza wafuasi wake yeye haifahamiki vizuri yuko wapi. Bulldozer baada ya kusababisha dhahama hiyo ndo kwanza anapanda ndege kurudi zake Dar badala ya kuongoza ibada ya mazishi ya hao waliokufa!
Umeongea point ya muhimu sana. Ilibidi awe mmoja wa waokoaji wa mstari wa mbele na kuliwza wafiwa
 
Mtasema serikali inaingilia uhuru wa kuabudu
Jukumu la msingi la serikali ni kuhakikisha usalama wa watu wake.
Hakuna uhalali wowote ule wa ibada hatarishi hasa hizo za sanamu za matapeli.
 
Halafu utakuta mchungaji anaendelea na ujinga wake na serikali itakaa kimya tu kwa mauwaji hayo
Huyu ilikuwa awe ndani saa hizi kujibu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Sijapata kuona watu wajinga zaid kama wafuas wa....... yani unalikuta jitu lina ma digirii lkn kichwan pumbav kabisa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilichojifunza, hakuna kitu chenye thamani kama damu ya Yesu, sasa hayo mafuta ya upako sijui na vitu gani vingine sijavielewa vizuri..
 
Mkuu labda utuambie wewe hili tukio unalionaje, kwamba ni tukio la kawaida tu na watu hawatakiwi kusema kitu?
Kwahiyo kama halijawahi kutokea tena, basi tusiongee tukae kimya?
Wewe huoni kama kuna uzembe uliofanyika kwa upande wa waandaaji (akiwepo mchungaji) uliopelekea watu 20 kufa?
Na je unachukuliaje kitendo cha mchungaji kuondoka zake baada ya watu 20 kufariki as if nothing happened, akaishia airport?
Wakati wanakanyaga mafuta wala hakuwepo alishaondoka akaacha watu wanasukumana!! Nafikiri hata hizo taarifa kazipata akiwa Dar tayari!
 
Uchagani wajinga ni wengi sana....... Wewe huoni wanavyoburuzwa na Chadema!
Usijumuishe kiujulma kwamba ni uchagani,Moshi Mjini wanaishi makabila yote na wasio na kabila.Kubagua ni kufanya sana hata Mwalimu Nyerere alilisemea hili.
 
Polisi wanasema wanamsaka,wakati lamaa leo nasikia yupo Kawe anapiga neno..
 
Mauaji ya kimbari Rwanda yaliongozwa na mapadri na maaskofu wa kanisa katoliki ambao wote walikuwa na digrii za theolojia.Kagame hajielewi.Yeye mwenyewe huwa anaenda kusali Nigeria kwa TB Joshua ambaye hajawahi somea uchungaji maisha Yale yote
Kagame hajawahi kusali SCOAN kwa TB Joshua...leta evidence hapa kwa usemayo ni kweli. He is way far too smart for this kind of shit. He understands the way of the world which is 'survival of the fittest' mind you He will do anything absolutely anything to ensure that he survives and stays in power. Pia mauaji ya kimbari hayakuongozwa na mapadre wala maaskofu... Hawakuongoza elewa maana ya neno kuongoza bali walishiriki na kuchochea maana wengi wao walikua wahutu na hatred kwa watutsi ilikua ishaenea nchi nzima..this kind of hatred transcended religion...had you been there...ungekua mtu wa huko ungenielewa vizur..War is war my friend. Never wish for something called War..let alone tribal/civil war...madhara yake ni makubwa..makovu yake huwa hayafutiki milele. To date ukiachilia mkono wa chuma wa Kagame wahutu na watutsi hawapendani...its a matter of time before what happen in 1994 will happen again. Najua huwez nielewa maana hivi vitu wengi mmevisoma kwenye vitabu na mitandao but had you lived in Rwanda and eastern Congo from 1990 to early 2000s you would understand what i mean
 
Sijakuelewa mkuu! Yaani wamekanyagana wakigombea kukanyaga mafuta au wakigombea kuchukua hayo mafuta?

Mungu tuhurumie Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
...Mkuu, nadhani ana maana ya kwamba Huyo Mtume aliyamwaga mafuta hayo sehemu kisha akadai kuwa watakaokanyaga sehemu hiyo watapata baraka na ndio mijitu ikakanyagana ikigombea kukanyanga sehemu hiyo!
Nimefarijika kwamba idadi ya watoto waliopoteza maisha in ndogo ukilinganisha na idadi ya hao watu wazima ambao wanapaswa akili za kuambiwa wachanganye na zao....!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom