#COVID19 Most Mutated COVID-19 Variant yet found in Tanzania travelers

US na UK pia wanaweza kutoa mutations zao. Sayansi ina safari mrefu sana kumaliza hili tatizo
Sawa. Angalau wenzetu wanapima na kuwapa wananchi wao chanjo. Mutationnikitokea wanaiona mapema, wanaiwahi kuitafutia dawa na chanjo.

Sisi hatupimi, hatu isolate, hatuwapi watu chanjo, mutation kuonekana mpaka Watanzania wasafiri wapimwe nje huko!
 
Hiyo COVIDO imejaribiwa wapi na lini katika kutibu Corona?Ilionyesha mafanikio ya asilimia ngapi?
 
mafitna haya mkuu yani maisha yako mazuri huku Tanzania kuliko mnavyoaminishwa huko na mabeberu alafu wewe ni learned brother sikutegemea kama utayumbishwa na propaganda
Kwanza kabisa usitegemee chochote kutoka kwangu kwa fikra zako kwamba mimi ni "learned brother". Naomba unitoe katika hiyo list yako, kwa sababu siku yoyote nina uwezo mkubwa wa kukushangaza kwa kuandika kitu ambacho hujategemea halafu ukasema "huyu learned brother kasemaje hivi"?

Naomba uniachie uhuru wangu kwa kunitoa katika list hiyo.

Kwenye hoja zako.

Magufuli naye alisema hivyo hivyo kwamba ugonjwa huu unapazwa kwa propaganda. Kafyekelewa mbali.

Wewe unaweza kutamba hivyo kwa sababu labda ni kijana na huna magonjwa kama hayo ya moyo, kisukari etc. Ukiwa mzee na una magonjwa hayo Covid-19 inaua sana.

Kama hujali maisha yako, jali maisha ya watu wanaokuzunguka ambao wanaweza kuwa na matatizo ya afya.

Dr. Mahiga kafariki, Maalim Seif kafariki, Balozi Kijazi kafariki, Magufuli kafariki, hao viongozi wakubwa tu wanaojulikana. Bado wewe unasema huu ugonjwa ni propaganda?

Sasa wewe ama ni mjinga hujui hilo, ama ni mbinafsi hujali.

Yote mawili ni majanga.
 
Corona huwa ni mzaa mzaa hivi hivi mpaka siku unasikia uzito kifuani hewa haiingii wala kutoka ndo unaelewa kuwa hili dubwasha ni hatari.
 
Corona huwa ni mzaa mzaa hivi hivi mpaka siku unasikia uzito kifuani hewa haiingii wala kutoka ndo unaelewa kuwa hili dubwasha ni hatari.
We mpaka Tingatinga limekutana na meli ya sumu mfereji wa Suez limeishindwa unafikiri mchezo?

Magufuli tumemzika kama utani.
 
eti leo corona ya kutoka tanzania imejipanga zaidi[emoji16][emoji16][emoji16].

kama matoleo ya tecno vile,wakati unatumia ukisikilizia utamu wake kesho kuna nyinyine inatangazwa.
Eti sisi tuna toleo Kali zaidi la corona lenye prosesa yenye nguvu Mara kumi zaidi ya ile ya china.
Utasikia astra zaneca wana chanjo yake muda si mrefu.
 
Sawa. Angalau wenzetu wanapima na kuwapa wananchi wao chanjo. Mutationnikitokea wanaiona mapema, wanaiwahi kuitafutia dawa na chanjo.

Sisi hatupimi, hatu isolate, hatuwapi watu chanjo, mutation kuonekana mpaka Watanzania wasafiri wapimwe nje huko!

We need to start emphasising the importance of taking precautions.
Haya mengine kama mutations ya virus ni ngumu sana kusema lolote kwa sasa.
Terrible, Brazil imepigwa kweli kweli na Corona. I hope hawaendeshi mambo kama tunavyofanya
 

Let discuss this scientifically, je hata tungefuata WHO instructions kusingetokea virus mutation?
 
Hakuna mahalo ilipoandikwa kuwa hii covid mutant eti ina nguvu mara kumi. Hakuna research iliyosema hivyo.
Pia hakuna research iliyosema variant hii ipo resistant kwa vaccine.

Subirini, it can be less harmful or even not harmful. Not saying that it won't be harmful.

Watanzania kwa ujumla tupo nyuma sana kisayansi. Tupende tusipende, kwa sababu tupo nyuma sana kisanaa.
 
Hata Kama hazitumiki what if zingekuwa zinatumika je zingefaa akati unaambiwa kirus kimefanya mutation
Kirusi kimefanya mutations 10, kwa sababu kimeachiwa tu kitapakae, nchi haipimi watu, hai isolate watu, hai chanji watu.

Nchi ingekuwa inapima watu, ina isolate watu na inchnja watu, kirusi kingekuwa controled, na hata mutations zingeonekana na kukabiliwa mapema si kutegemea watu wanaosafiri na kupimwa nje ya Tanzania.

Tumekumbatia ujinga.
 
Let discuss this scientifically, je hata tungefuata WHO instructions kusingetokea virus mutation?
Virus wa Corona huwa wanafanya mutations muda wowote ule na popote pale lakini huwa wanapata wasaa pamoja na uwanja mpana zaidi wa kufanya mutations kama wakiachwa huru bila ya kupigwa vita.Hii maana yake ni kwamba kama hapa Tanzania tungewapiga vita kama vile kupiga watu chanjo na kuwapiga vita katika kutumia njia nyingine za kuzuia wasienee kwa wingi pia mutations ingekuwepo ila siyo hiyo kubwa ya mara kumi,ingekuwepo mutation ndogo mfano ya mara mbili,tatu au nne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…