#COVID19 Most Mutated COVID-19 Variant yet found in Tanzania travelers





Hatufuati kivipi? Unataka police wapite waanze kupiga watu? Usiamini kila kitu tafuta undani wake kwanza, haya hizo hapo instruction kutoka wizara ya afya
 
UMENENA VYEMA. WAKO WANATUTISHA KWA KUTUPAKAZIA PROPAGANDA ZA KORONA. HATUTISHIKI. TUKO IMARA JPM ALALE PEMA PEPONI. ULITUEPUSHA NA UTUMWA WA FIKRA ZA KUBUMBA ZA KORONA. ALISEMA TUSITISHANE. USIPOKUFA KWA KORONA UTAKUFA KWA UGONJWA MWINGINE. ZIDUMU FIKRA ZA MAGUFULI
 
Behaviourist unalipwa na kueneza hofu si bure kwa kukomalia propaganda za plandemic. Ushindwe n ulegee.
 
Azitaje? Do u by any chance, know of the UK & SA variants? Au nao walipuuzia kama sisi?
 
USA wnafuata hizo njia? Maambukizi yakoje?
 
UK wanafuata hizo njia? Maambukizi yako yakoje?
Kwa kawaida tu watu wengi wanakufa na cancer na TB achilia magonjwa ya watoto (maternal death) nchini Tanzania
Lakini UK wakitoa data ya haya magonjwa kwao, bado idadi itaonekana kubwa kulinganisha kwa nchi kama Tanzania ambapo hakuna mfumo wa ukusanyaji data, au serikali imeaamua kimabavu kutotoa data kwa wananchi wake.
UK na development world hawana yakuwaficha wananchi wao kwenye vitu vya umuhimu kama hivi.
 
UK wanafuata hizo njia za kisayansi? Maambukizi yao yakoje by percentage?
 
South Africa na UK wamezalisha mutation, nao hawapimi watu?
Umeelewa msingi wa habari kwamba mutation ya Tanzania imejiongeza kuliko zote zilizojulikana?

Unaelewa tofauti ya "mutated" na "most mutated" ?

Umeelewa msingi wa kupima sio kuzuia mutation bali kuziwahi ili kuzijua mapema na kuzidhibiti kwa chanjo mpya, kuzuia "mutated" zisije kuwa "most mutated"?
 
Jibu swali
 
Mimi mbona niko Marekani nimepiga chanjo mbili za Pfizer na sijafa?

Na kama issue ni kufa tu, kuna mtu ambaye hatakufa?

Unajua kujenga hoja kwa mantiki?

Yani mtu anakwambia, ukitaka kuvuka barabara, kwa usalama zaidi, kabla ya kuvuka barabara, angalia kulia, angalia kushoto, angalia kulia, hakikisha hakuna magari kote, vuka barabara.

Wewe unajibu, hata wanaoangalia magari hivyo wengine wanagongwa na kufa, sasa solution ni nini?

Unataka dunia iwe na vifo 0 vya watu waangalifu kugongwa na magari ndiyo ukubali kujihadhari na magari unapovuka barabara kunapunguza ajali na vifo barabarani?
 
Kuna jamaa mmoja hapa JF nilimwambia Tanzania inaweza kutoa mutation mpya ya kirusi, akawa anabisha saaana kwa ubishi wa kibongo wa ilimradi kubisha tu

Natamani niuone ule uzi nimuoneshe hii habari.

Na bado, tukiendelea hivi tutapigwa marufuku kusafiri kwani tunafanya hata hizi vaccines zisiwe na maana kwa ajili ya ujinga tu.
 
Jibu swali
Swali lako linawalinganisha wewe na babu yako mzaa baba yako mzazi kwamba wote mna miaka sawa, kwa sababu wote mna watoto.

Ukweli kwamba wewe una mtoto, na babu yako mzaa baba yako naye ana mtoto (ambaye ni baba yako mzazi) haukufanyi wewe uwe na umri sawa na babu yako mzaa baba yako mzazi.

Unapolinganisha vitu, linganisha vitu vinavyolingana.
 
Nionavyo kwa uchumi wetu sioni sababu ya kuhangaika na corona ambayo haina madhara kama marelia.


Kila siku mnatutisha tu tutakufa kama kuku na siku zinaenda tu sisi wa hali ya chini hatukidhi vigezo vya tahadhari ni kama wote twisha pata maambukizi tuna subiri kufa tu.

Msiba wa maalim kuna waliosema baada ya wiki tutaona watu wanavyo kufa sababu ya kukusanyika bila tahadhari sasa hivi tumehamia kwenye mkusanyika wa marehemu Jiwe.
 
Tatizo tunatofautiana katika kuthamini maisha ya mtu. Nchi imefiwa mpaka na rais wewe unaona jambo dogo tu hilo.

Kwa sababu wewe mbinafsi hujali wengine, ukiwa hai wewe tu unaona poa.

Hili tatizo ndilo linatufanya tuwe masikini, hatujaliani, kila mtu anajijali mwenyewe kwa kiasi kikubwa sana.

Wazee na watu wenye magonjwa makubwa wanakufa sana, lakini wewe inaonekana humo kwenye makundi yao, tena unaweza kusema ni sawa tu wafe.

Nikikwambia nikupige risasi ufe kwa sababu vifo vya risasi Tanzania si vingi kama vya Malaria utakubali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…