MotoGP, WRC, SuperBike and other Motorsports

MotoGP, WRC, SuperBike and other Motorsports

Walianza hivi; 1Pedrosa, 2Lorenzo 3MM 4Rossi, baada ya race kuanza tu kama kawa Lorenzo ni mzuri sana kwenye kuanza, kaongoza kama lap 2 hivi nyuma yake akiwa the doctor, the doctor kapita na anaongoza nyuma yake mchuano mkali kati ya MM na Lorenzo.

Huko garage watu wanaandaa bikes nyingine kwa sababu ya mvua inayotegemewa kunyesha muda wowote

Haya Lorenzo yuko nafasi ya nne, Pedrosa-3, MM-2, the doctor anawaburuza
 
Doh, hii ilikua race ya kiume, Marc Marques ni habari nyingine aisee itabidi umkubali tu, Pedrosa anaonekana karudi, good race from him na the doctor anautumia uzoefu vizuri. Jamaa yangu Lorenzo hakua na pafu la kushindana na hawa jamaa.
 
Catalunya 2014

 

Attachments

  • rossi1.jpg
    rossi1.jpg
    99.8 KB · Views: 43
  • rossi2.jpg
    rossi2.jpg
    91.3 KB · Views: 62
Doh, hii ilikua race ya kiume, Marc Marques ni habari nyingine aisee itabidi umkubali tu, Pedrosa anaonekana karudi, good race from him na the doctor anautumia uzoefu vizuri....

Marquez-Rossi-Pedrosa-590x393.jpg
Rossi zaidi ya uzoefu ameweza kuimprove katika braking distance na kuweza kutumia mfumo mpya wa clutch less - downshift, ambao bado ni mpya kwa Team Yamaha. Kwao Honda mfumo huu walianza kuutumia zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Kwa Lorenzo mfumo huu unahitaji uwezo wa juu katika braking, kitu ambacho sio mazoea yake kwani ana speed kubwa kwenye kuingia kwenye kona. Hata hivyo kuingia kwa matairi ya Bridgestone, setting ya downshift clutchless na braking kumemfanya Lorenzo astruggle sana kwa baadhi ya mbio ukiacha ile tu ya Mugello, ambayo aliweza kupata kombination nzuri ya setting.
 
TT Assen GP

Qualification:-

1. Aleix Espargaro - Forward Yamaha

2. Marc Marquez - Honda

3. Dani Pedrosa - Honda

4. Andrea Iannone - Ducati


9. Jorge Lorenzo - Yamaha

12. Valentino Rossi - Yamaha.

Note:
Mashindano haya yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 28/06/14, saa 9 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki. Ni mashindano pekee katika kalenda ya MotoGP kufanyika siku ya Jumamosi.
 
TT Assen GP

Qualification:-

1. Aleix Espargaro - Forward Yamaha

2. Marc Marquez - Honda

3. Dani Pedrosa - Honda

4. Andrea Iannone - Ducati


9. Jorge Lorenzo - Yamaha

12. Valentino Rossi - Yamaha.

Note:
Mashindano haya yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 28/06/14, saa 9 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki. Ni mashindano pekee katika kalenda ya MotoGP kufanyika siku ya Jumamosi.

Ahsante kwa taarifa Mkuu, imebidi nibadilishe channel baada ya kusoma uzi huu nakutana na Moto2, 16 laps to go
 
Ahsante kwa taarifa Mkuu, imebidi nibadilishe channel baada ya kusoma uzi huu nakutana na Moto2, 16 laps to go
Moto2, inanipita leo... Hapa nafanya fasta shughuli fulani ili niwahi kucheck overtake za The Doctor...
 
Moto2, inanipita leo... Hapa nafanya fasta shughuli fulani ili niwahi kucheck overtake za The Doctor...

Track ilikua wet kwa muda mrefu ila inaendelea kukauka kwa hiyo nategemea tutaona race nzuri sana ya The Doctor and co.

So far West anaongoza mbele ya Maverick Vinales na Kallio, 4 laps to go
 
The Doctor anakwenda Ujerumani weekend hii akiwa na smile tele, ni baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na Yamaha....
 
Back
Top Bottom