Mourinho asema Barcelona na Real Madrid zingekua England maisha yao yangekua magumu

Mourinho asema Barcelona na Real Madrid zingekua England maisha yao yangekua magumu

hivi wewe una akili ?
lini barcelona au madrid kamaliza unbeaten kwenye ligi yao ?
kwanini wasifungwe ??
hawa madrid wakacheze kila wiki mikiki mikiki ya epl msimu mmoja wataomba poo
yaani ucheze wiki hii na everton wiki ijayo na crystal wiki ijayo na stoke wiki inayofuata na Arsenal kisha man u kisha unasubiri man cty chelsea liverpool spurs ndio wasifungwe ??
kufungwa kunatokana na kuchoka kwa wachezaji sio kiwango kibovu upo hapo ?

Kwa uelewa wangu mdogo hizi ligi zote zina timu 20 na zina mechi 38 ila tu Laliga inaanza wiki moja kabla ya EPL sasa hii habari ya kila wiki nadhani iko kote.
 
Jamani ligi ya EPL wanatumia NGUVU kubwa sana sana kuitangaza lakini hamna kitu,angalia vitu Vichache tuu,Tangu wewe unaesoma ujumbe huu upate akili nani kutoka EPL amewahi Kuwa Mchezaji Bora wa Dunia au hata Ulaya? Wote wanatoka Spain na Italy,mpira wa Spain unakupa nafasi ya kuweza kuonyesha kipaji chako,England ni Mbio tuuu mwanzo mwisho,uki jaribu kupunguza wawili watatu either utatolewa Nje Kuwa unawachelewesha wenzako "kukimbia"Mbele,kwa Uchache Johan Kruff,Frank Rijkaad,George weah Opong,Rivaldo,Ronaldo de Lima,Fabiola Canavaro,Jurgen klinsman,Ruud voller,Zinedine Zidane,Ronaldinho,Pele Maradona,Zico,Lionel Mess na Christiano Ronaldo!wao Waingereza ni kupiga Kelele tuu kwenye Vyombo Vya habari!hata UEFA champions league,Madrid 10 times,AC Milan 7 times,ndo wanakuja Liverpool (EPL) 5 nk.timu za Taifa hivyo hivyo sasa Tuangalie wapi tena?,uje hata Makocha bora na wengi(kwa Utaifa wao)ni Waitaliano na Spain.Sijui Tuangalie wapi tena!
Italy ndo Ana uwezo wa kumsimamisha Spain!

duhh kumbe ronaldo 2008 alikua madrid ??
 
Stoke City, Swansea, Manchester United, Arsenal na wengine wote ni timu mbovu period. Kwahiyo wagonjwa wakikutana we unategemea nini? Hizo timu nilizozitaja hapo juu, achana na Real Madrid, Barca, Atleti au Valencia, hakuna hata moja inayoweza kusimama na Malaga, sasa hizi kelele za Uingereza tumeshazizoea. Ushauri kwa Morinho, anatakiwa afundishe mpira kunyanyua kiwango cha soka la England, maneno maneno hawaachie kina Khadija Kopa wao ndio wanaolipwa kwa kazi hiyo.
 
Siyo kila mwaka mkuu, labda kama umeanza kutazama mashindano hayo hivi karibuni! Chelsea ilimfunga barca kwao na ikamwondoa kwenye mashindano! Na mwaka ule chelsea walibeba ndoo ya UEFA!

Hivi karibuni lini?
 
Du! mansakankanmusa una umri gani mkuu? Unajua Newcastle walichukua lini ubingwa wa England? 1927! Liverpool nao mwisho kuona ndoo ilikuwa msimu wa 1989-1990. Ina maana toka EPL ianze mwaka 1992, Newcastle na Liverpool hawajawahi kutwaa ubingwa wa England.
 
Last edited by a moderator:
Ndo maana kuna mashindano ya kukutanisha teams za league zote, yaani wababe wa league zote Ulaya wanakutana katika league inayoitwa UEFA CHAMPIONS LEAGUE, hapo mnasemaje wadau?

Ujue kuna tofauti kubwa sana ya kucheza mechi 14 ambazo huchezwa kila baada ya wiki moja na zile 38 zinazochezwa kila wikend ambazo sometimes huchezwa hadi katikati ya wiki.
 
Ujue kuna tofauti kubwa sana ya kucheza mechi 14 ambazo huchezwa kila baada ya wiki moja na zile 38 zinazochezwa kila wikend ambazo sometimes huchezwa hadi katikati ya wiki.

Fafanua mkuu uko upande gani unaouamini wa epl ligi bora au la liga maana hzo mech 38 hata spain hivohvo pia kucheza katkat ni hata spain hvohvo
 
hebu nielewe mkuu nikikwambia barca ni hvi ishamfunga city barca ikamfunga chelsea barca ikamfunga arsenal barca pia imemfunga man u sasa ukintajia oooh city wap na wap mara chelsea ambaye mechi ya mwisho na madrid kala 3-0.sasa nazani umebielewa nitajie timu moja ya england ambayo imeshawahi kuifunga barca atletico na madrid ili nihamie NASUBIRIA JIBU

Unajitoa ufahamu au? ARSENAL KAWANYOSHA WOTE HAO.
 
Fafanua mkuu uko upande gani unaouamini wa epl ligi bora au la liga maana hzo mech 38 hata spain hivohvo pia kucheza katkat ni hata spain hvohvo

Kaka ligi ya uingereza ngumu kinachotokea sasa hata Spain kishawahi kuwakuta kutoingiza timu hata moja robo fainali.
 
Kaka ligi ya uingereza ngumu kinachotokea sasa hata Spain kishawahi kuwakuta kutoingiza timu hata moja robo fainali.

mara ya mwisho spain kutoingiza hata timu moja robo fainal ni mwaka gani mkuu maana mie sikumbuki
 
Mkuu huo ndo ukweli,timu iliyofungwa na r,madrid gori9, ndo iliyofungwa barc gori8,wachezaji wake hawajalipwa mishahala yao km miezi5 hivi,epl ulishasikia timu imeshindwa kulipa wachezaji?

Unakijua kilichoishusha Portsmouth daraja?
 
nafikili kama sikosei ilikatagwa pointi 10 kwa kutowalipa wachexaji wake mishahara

Ndio hivyo mkuu, hizo kitu huwa zinatokeaga tu kila sehemu, Monaco kumfunga Arsenal haimaanishi ligi ya France ni bora kuliko EPL, wala Juve kumtoa Madrid pia sio ishu sana. Ebu kwa mfano kombe la UCL akichukua Juve, ndio tuseme kuwa Seria A ni bora kuliko ligi zote ulaya? Anyway mimi naona alichokizungumzia Morinho hapo juu ni ushindani, na hilo halipingiki ligi ya EPL ina ushindani mkubwa kuliko La liga.
 
Ref. 1976/1977.

kaaaaaaah kwanza pole sana mkuu kwa kuangaika kugoogle yani kipindi hiko mama yangu alikuwa ndio.kwanza anasoma tena shule ya msingi yani mm.hata mpango wa kuzaliwa sina
 
Ndio hivyo mkuu, hizo kitu huwa zinatokeaga tu kila sehemu, Monaco kumfunga Arsenal haimaanishi ligi ya France ni bora kuliko EPL, wala Juve kumtoa Madrid pia sio ishu sana. Ebu kwa mfano kombe la UCL akichukua Juve, ndio tuseme kuwa Seria A ni bora kuliko ligi zote ulaya? Anyway mimi naona alichokizungumzia Morinho hapo juu ni ushindani, na hilo halipingiki ligi ya EPL ina ushindani mkubwa kuliko La liga.

kiupande wangu binafs naona epl ni ligi maarufu sababu inakuzwa na vyombo vya habari ila spain ni ligi bora na ndio mana miaka yote inafanya vizur hvyo ni ishara tosha kuwa sio ligi ya kubahatshabahatsha
 
Back
Top Bottom