Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,734
- 140,476
Kocha nguli wa soka duniani, José Mourinho, amebatiza mchezo wa ushindi wa mabao 3-2 wa Argentina dhidi ya Misri kuwa ni "filamu iliyoandaliwa matokeo tangu mwanzo," akilalamikia vikli maamuzi ya marefa na chumba cha VAR yaliyowaumiza Farao hao wa Misri. Mourinho amefunguka kwa hisia kali akidai kuwa mchezo huo haukuwa wa haki na kwamba Misri haikupoteza kwa sababu ya soka, bali kwa sababu ya "script" (maandishi) ya mashindano hayo yanayobeba upendeleo kwa upande mmoja.
Katika uchambuzi wake, Mourinho alifafanua jinsi maamuzi kadhaa ya utata yalivyopindua mchezo huo ambao Misri iliongoza kwa mabao 2-0 mapema, akitolea mfano pale nahodha Mohamed Salah aliponyimwa faida ya kufunga goli, huku beki Cristian Romero akifanya madhambi mabaya yaliyotaka "kuuvunja mguu wa Salah vipande viwili" bila kupewa kadi yoyote. Zaidi ya hayo, alilalamikia VAR kurudisha nyuma mchezo "hadi zama za mawe" ili tu kutafuta kisingizio chochote cha kufuta goli la Misri, sambamba na kunyimwa penati ya wazi ya dakika ya 93 baada ya Salah kuangushwa ndani ya boksi.
Tukio hilo la mwisho lilitoa mwanya kwa Argentina kufanya shambulizi la kushtukiza lililomwezesha Enzo Fernández kufunga bao la ushindi, jambo lililomfanya Mourinho kuhitimisha kwa hasira: "Unapocheza dhidi ya hii timu ya Argentina, kuwa mbele kwa mabao 2-0 haitoshi, kwa sababu haujaribu tu kuwafunga wanaume 11 uwanjani. Unajaribu kuishinda filimbi. Unajaribu kuishinda chumba cha VAR. Unajaribu kushinda 'script' nzima ya mashindano. Huu sio mpira wa miguu tena. Ni filamu, na mwisho wake umeshapangwa kabla hata wachezaji hawajatoka kwenye koridoro kuelekea uwanjani."