Mourinho: Mechi ya Misri na Argentina ilikuwa filamu

Mourinho: Mechi ya Misri na Argentina ilikuwa filamu

View attachment 3624817

Kocha nguli wa soka duniani, José Mourinho, amebatiza mchezo wa ushindi wa mabao 3-2 wa Argentina dhidi ya Misri kuwa ni "filamu iliyoandaliwa matokeo tangu mwanzo," akilalamikia vikli maamuzi ya marefa na chumba cha VAR yaliyowaumiza Farao hao wa Misri. Mourinho amefunguka kwa hisia kali akidai kuwa mchezo huo haukuwa wa haki na kwamba Misri haikupoteza kwa sababu ya soka, bali kwa sababu ya "script" (maandishi) ya mashindano hayo yanayobeba upendeleo kwa upande mmoja.

Katika uchambuzi wake, Mourinho alifafanua jinsi maamuzi kadhaa ya utata yalivyopindua mchezo huo ambao Misri iliongoza kwa mabao 2-0 mapema, akitolea mfano pale nahodha Mohamed Salah aliponyimwa faida ya kufunga goli, huku beki Cristian Romero akifanya madhambi mabaya yaliyotaka "kuuvunja mguu wa Salah vipande viwili" bila kupewa kadi yoyote. Zaidi ya hayo, alilalamikia VAR kurudisha nyuma mchezo "hadi zama za mawe" ili tu kutafuta kisingizio chochote cha kufuta goli la Misri, sambamba na kunyimwa penati ya wazi ya dakika ya 93 baada ya Salah kuangushwa ndani ya boksi.

Tukio hilo la mwisho lilitoa mwanya kwa Argentina kufanya shambulizi la kushtukiza lililomwezesha Enzo Fernández kufunga bao la ushindi, jambo lililomfanya Mourinho kuhitimisha kwa hasira: "Unapocheza dhidi ya hii timu ya Argentina, kuwa mbele kwa mabao 2-0 haitoshi, kwa sababu haujaribu tu kuwafunga wanaume 11 uwanjani. Unajaribu kuishinda filimbi. Unajaribu kuishinda chumba cha VAR. Unajaribu kushinda 'script' nzima ya mashindano. Huu sio mpira wa miguu tena. Ni filamu, na mwisho wake umeshapangwa kabla hata wachezaji hawajatoka kwenye koridoro kuelekea uwanjani."
FAKE NEWS
 
Mourinho anaongea kwa code utadhani hakuna asiyejua nani aliyekuwa incharge kwenye chumba cha VAR
FB_IMG_1783451610172.jpg
 
Umeandika kishabiki sana hapa.

Faulu gani ya Romero iliyotaka kumvunja Salah mguu vipande viwili?!

Nyie mashabiki wa Ronaldo mmechanganyikiwa, Misri wametolewa kwa uzembe wao wenyewe.

Romero kachukua mpira kaanzisha shambulizi wakaenda kufunga goli la tatu, huku huyo Salah akijiangusha kama kawaida yake.
Huyu kapagawa 😂😂😂

Eti ile Salah alivyojiangusha ndio faulo iliyotaka kumvunja Salah miguu what a joke
 
Punguza kusema ukweli

Ila Argentina Jana haijabebwa ni uzembe wa Egypt wenyewe ndio umewaponza
Kabebwa ,kwanzia fauli nyepesi aliyochezewa martinezi goli likafungwa VAR wapitia bila hata malalamiko ya wachezaji wa Argentina, fauli hiyo nyepesi kachezewa salah na ikazaa movement ya goli na refa akagoma hata kutazama VAR tu
Screenshot_2026-07-08_095925.jpg
 
Tunaomba source ya taarifa yako I don't think Mourinho anaweza kuongea maneno kama hayo

José Mourinho slammed the controversial refereeing in Argentina's 3-2 victory over Egypt in the FIFA World Cup 2026 Round of 16 as "daylight robbery".
He strongly criticized the inconsistent VAR decisions, claiming the tournament felt like a "script" decided before the games were even played.Mourinho specifically pointed out several major grievances during the match
😀isallowed Egyptian Goal: He questioned why the referee waited to allow play to continue and a goal to be scored before going back to the VAR room to cancel it for a questionable foul.Missed Penalties and Fouls
: He argued that a clear foul on Mohamed Salah in the box was ignored, allowing Argentina to quickly counter and score the winning goal, while aggressive tackles by Argentina players went unpunished.VAR Favoritism:
Mourinho demanded to know why every incident favoring Argentina was scrutinized while Egypt did not seem to receive the same treatment
 
Kabebwa ,kwanzia fauli nyepesi aliyochezewa martinezi goli likafungwa VAR wapitia bila hata malalamiko ya wachezaji wa Argentina, fauli hiyo nyepesi kachezewa salah na ikazaa movement ya goli na refa akagoma hata kutazama VAR tuView attachment 3624885
Wala sio kweli salah hapakuwa na faulo pale Mzee tuweke mahaba kando ukweli usemwe na ile ya Martinez mbona ilikuwa ni faulo ya wazi kabisa two against one na akakanyagwa mguu
 
Wala sio kweli salah hapakuwa na faulo pale Mzee tuweke mahaba kando ukweli usemwe na ile ya Martinez mbona ilikuwa ni faulo ya wazi kabisa two against one na akakanyagwa mguu
Mguu ulikwatuliwa kabla ya kuugusa mpira
Screenshot_2026-07-08_095944.jpg
 
Punguza kusema ukweli

Ila Argentina Jana haijabebwa ni uzembe wa Egypt wenyewe ndio umewaponza
Naona uko kinyume na walimwengu wengine.
👇👇Just to connect you into discussion.

 

Attachments

  • Screenshot_2026-07-08-11-01-47-59.jpg
    Screenshot_2026-07-08-11-01-47-59.jpg
    127.8 KB · Views: 15
Back
Top Bottom