Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 8,797
- 15,762
FAKE NEWSView attachment 3624817
Kocha nguli wa soka duniani, José Mourinho, amebatiza mchezo wa ushindi wa mabao 3-2 wa Argentina dhidi ya Misri kuwa ni "filamu iliyoandaliwa matokeo tangu mwanzo," akilalamikia vikli maamuzi ya marefa na chumba cha VAR yaliyowaumiza Farao hao wa Misri. Mourinho amefunguka kwa hisia kali akidai kuwa mchezo huo haukuwa wa haki na kwamba Misri haikupoteza kwa sababu ya soka, bali kwa sababu ya "script" (maandishi) ya mashindano hayo yanayobeba upendeleo kwa upande mmoja.
Katika uchambuzi wake, Mourinho alifafanua jinsi maamuzi kadhaa ya utata yalivyopindua mchezo huo ambao Misri iliongoza kwa mabao 2-0 mapema, akitolea mfano pale nahodha Mohamed Salah aliponyimwa faida ya kufunga goli, huku beki Cristian Romero akifanya madhambi mabaya yaliyotaka "kuuvunja mguu wa Salah vipande viwili" bila kupewa kadi yoyote. Zaidi ya hayo, alilalamikia VAR kurudisha nyuma mchezo "hadi zama za mawe" ili tu kutafuta kisingizio chochote cha kufuta goli la Misri, sambamba na kunyimwa penati ya wazi ya dakika ya 93 baada ya Salah kuangushwa ndani ya boksi.
Tukio hilo la mwisho lilitoa mwanya kwa Argentina kufanya shambulizi la kushtukiza lililomwezesha Enzo Fernández kufunga bao la ushindi, jambo lililomfanya Mourinho kuhitimisha kwa hasira: "Unapocheza dhidi ya hii timu ya Argentina, kuwa mbele kwa mabao 2-0 haitoshi, kwa sababu haujaribu tu kuwafunga wanaume 11 uwanjani. Unajaribu kuishinda filimbi. Unajaribu kuishinda chumba cha VAR. Unajaribu kushinda 'script' nzima ya mashindano. Huu sio mpira wa miguu tena. Ni filamu, na mwisho wake umeshapangwa kabla hata wachezaji hawajatoka kwenye koridoro kuelekea uwanjani."
Huyo kocha wa Misri inabidi tumuonyeshe chumba cha kwenda kutoa machozi yake😂Vipi kuhusu Portugal ya Cr7 wao sio wa muhimu kwa FIFA kwenye World Cup marketing?
Argentina imeshinda kwa
1. Huruma ya referee / kubebwa/mbeleko/figisu = 85
2. Uzembe wa Misri = 15
Pia na wao gemu ya coreshia walibebwa , mpira wa aina hii ni w hovyo mno bwasheeVipi kuhusu Portugal ya Cr7 wao sio wa muhimu kwa FIFA kwenye World Cup marketing?
Kabisa 📌🤣Mou ni mreno, tunatambua maumivu Yao!
😄😄😄Ukiona unabebwa ujue una kitu.
Ukibebwa bebeka
Messi ni GOAT.
cristiano ni goti (la mguu).
Mzee kuamia sana kuona ureno hata robo hawajafika 🤣😅😅 Mou anachukia na Leo toka kitamboo
Huyu kapagawa 😂😂😂Umeandika kishabiki sana hapa.
Faulu gani ya Romero iliyotaka kumvunja Salah mguu vipande viwili?!
Nyie mashabiki wa Ronaldo mmechanganyikiwa, Misri wametolewa kwa uzembe wao wenyewe.
Romero kachukua mpira kaanzisha shambulizi wakaenda kufunga goli la tatu, huku huyo Salah akijiangusha kama kawaida yake.
😄😄 Kufika hatua ya mtoano tu Kuna goli la Colombia lilikataliwa na goli la Croatia piaVipi kuhusu Portugal ya Cr7 wao sio wa muhimu kwa FIFA kwenye World Cup marketing?
Punguza kusema ukweliPia na wao gemu ya coreshia walibebwa , mpira wa aina hii ni w hovyo mno bwashee
Kabebwa ,kwanzia fauli nyepesi aliyochezewa martinezi goli likafungwa VAR wapitia bila hata malalamiko ya wachezaji wa Argentina, fauli hiyo nyepesi kachezewa salah na ikazaa movement ya goli na refa akagoma hata kutazama VAR tuPunguza kusema ukweli
Ila Argentina Jana haijabebwa ni uzembe wa Egypt wenyewe ndio umewaponza
Tunaomba source ya taarifa yako I don't think Mourinho anaweza kuongea maneno kama hayo
Wala sio kweli salah hapakuwa na faulo pale Mzee tuweke mahaba kando ukweli usemwe na ile ya Martinez mbona ilikuwa ni faulo ya wazi kabisa two against one na akakanyagwa mguuKabebwa ,kwanzia fauli nyepesi aliyochezewa martinezi goli likafungwa VAR wapitia bila hata malalamiko ya wachezaji wa Argentina, fauli hiyo nyepesi kachezewa salah na ikazaa movement ya goli na refa akagoma hata kutazama VAR tuView attachment 3624885
Mguu ulikwatuliwa kabla ya kuugusa mpiraWala sio kweli salah hapakuwa na faulo pale Mzee tuweke mahaba kando ukweli usemwe na ile ya Martinez mbona ilikuwa ni faulo ya wazi kabisa two against one na akakanyagwa mguu
Naona uko kinyume na walimwengu wengine.Punguza kusema ukweli
Ila Argentina Jana haijabebwa ni uzembe wa Egypt wenyewe ndio umewaponza