Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Mwalimu, without CCM in the bandwagon hakuna mjadala. Kama watu wanataka mabadiliko ya Katiba ni lazima waanzie na CCM, ni jinsi gani tunaweza kuishawishi CCM kuwa mabadiliko ya Katiba yatakuwa for their own interests? Ukiweza kuja na hoja ya kuwashawishi CCM basi hatumuhitaji Mwinyi. Sasa hivi watu wakitaka kuzungumzia Katiba wanaruhusiwa na hata kufanya semina za "mabadiliko ya Katiba".

Lakini vyote hivyo havina nguvu kwani havijaonesha bado kwanini CCM ibadili Katiba na kutengeneza mazingira ya Chama hicho kuondolewa madarakani.
 
In fact baada ya tamko lile la serikali, you can't expect for any better opportunity to discuss our constitution; namshukuru sana mbunge Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa kuileta hii topic.

Sasa hivi ndio wakati wa kupiga kengele na makopo yote ili hata viziwi wasikie. Katiba yetu ina mapungufu mengi sana, na tangazo hili la serikali limeiharibu kabisa vacation yangu. Itabidi niisome tena ktiba hii kwa makini ingawa ni ndefu sana (page mia na ushee), ili niinyambue mapungufu nitakayoona, halafu nijiyapigie kelele. Nashauri kuwa wana JF wote tuiangalie katiba hii na tuitolee maoni yetu sasa hivi wakati bado kiti ni cha moto.
 
MKJJ,

Namwamini sana mzee Mwinyi katika kusukuma mabadiliko against the status quo bila kujali interest zake binafsi, kwa vile yeye ni mjumbe wa CC ya CCM na ni retired president, nadhani ana nafasi kubwa sana ya kutusaidia kubadilisha katiba hii - akiombwa kufanya hivyo na akakubali.
 
Hili la mjadala wa Katiba halitatokea kama CCM hawataki period. What CCM wants CCM gets, it doesn't want this so we won't get it. Ndio maana mimi naona kujaribu kubadilisha Katiba wakati hauna nguvu ya kufanya hivyo ni kutwanga maji kinuni. Hadi pale wapinzani wananguvu ya kulazimisha siyo kuomba kama wanavyofanya sasa.

Damn! I guess it won't be in our lifetime...
 
Nadhani umefika wakati sisi wananchi kuipigia kelele serikali yetu tusikae tu na kusema haiwezekani - inawezekana tukijaribu na kujitahidi, kila kizuri kina ughali wake na hakuna marefu yasiokuwa na mwisho. Maendeleo hayaji kwa kuyasubiri yanakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

Waagwana tusikate tamaa mapema hivo - CCM ina muda mrefu madarakani so tusidhani kuwa tutashinda kuyaondosha mabaya yake over night
 
Mabadiliko ya mfumo wa vyama vingi,soko huria nk. haya yote hayakusimamiwa na Mwinyi kwa ridhaa ya CCM bali shinikizo kutoka nje na wakati husika.Kesi ya ngedele huwezi kumpa nyani asimamie. Wapo watu mahiri na ambao hawana ukereketwa wa siasa zetu za ndani za vyama ambao wanaiweza sana kazi hiyo.
 
I support this wholeheartdeadly; this mzee is far more credible than many other CCM politicians. Hiyo kusema kuwa Mwinyi hakusaidi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa ni kukataa ukweli ulio uwazi. Tukumbuke huyu alikuwa Rais mwenye mamlaka kamili na angeweza kufanya kama alivyofanya Mugabe leo, tena kwa sisi wadanganyika ingekuwa balaa zaidi!
 
Petition: Tumwombe Rais Mwinyi Atuongoze Mjadala wa Kuboresha Katiba.

Ninashauri kuwa tumwombe mzee wetu Rais Ali Hassan Mwinyi atungoze katika kuendesha mjadala wa kuboresha katiba yetu. Alitungoza kwenye mabadiliko makubwa ya kutoka kwenye uchumi wa kijamaa na kutuingiza kwenye uchumi wa soko huria, halafu akatungoza kutoka mfumo wa chama kimoja kutuweka kwenye mfumo wa vyama vingi, mnaonaje akitusaidia hili dogo la kutuongoza kufanya mjadala wa kuboresha katiba yetu hasa kwa vile viongozi waliopo sasa hawataki kusikia neno katiba?

Wazo zuri lakini Mzee ruksa pamoja na kuvurunda kwake hana ushawishi na ubavu kwa hawa wezi vichwechwe. Kama unakumbuka vizuri alipewa fagio la chuma lililoishia kufagia anakojua mwenyewe.
 
I support this wholeheartdeadly; this mzee is far more credible than many other CCM politicians. Hiyo kusema kuwa Mwinyi hakusaidi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa ni kukataa ukweli ulio uwazi. Tukumbuke huyu alikuwa Rais mwenye mamlaka kamili na angeweza kufanya kama alivyofanya Mugabe leo, tena kwa sisi wadanganyika ingekuwa balaa zaidi!

Kitila acha bwana! Ruksa usimlinganishe na Mugabe kabisaa!Ni kweli alikuwa ni Rahisi (Rais)mwenye mamlaka kamili lakini alikuwa na ubavu huo wa kukataa kama Mugabe? Mtu ambaye ofisi 'takatifu' kama ile anaigeuza kijiwe cha wafanyabiashara na mashemeji anaweza kuwa na roho nya paka kama Mugabe? Sikatai anasifa za ziada kuliko wengi ndani ya CCM lakini kwenye suala hili NO.
 
Kitila do you seriously believe kwamba inner core ya CCM itakubaliana na hoja kama hiyo? Unajua kuwa true democracy Tanzania itaathiri sana maslahi ya wakubwa? Hakuna mtu atakayekubaliana na hilo. Ukweli uliopo ni kuwa kama issue hii inatakiwa kuwepo Tanzania waanze kubomoana wao kwa wao huko ndani, wengine ndio wa pick kutoka kwao.
 
Mwinyi...!!!???

Mimi naona bora tumtumie Salim A. Salim....sababu nitakuja nazo later.
 
Wakati Waziri anasema nilete maoni ya mabadiliko ya katiba kuhusu mfumo wa uchaguzi, tayari mnamo 31/5/2006 nilikuwa nimeandika barua kwa Rais kuhusu suala hili. Maoni gani tena yanatakiwa? nahisi serikali hii haina uratibu wa mambo yake. Barua hii ilichapishwa kama ilivyo na gazeti la Mtanzania. Wizara ya sheria na Katiba ilijibu barua yangu kuonesha wamepokea maoni yangu. Leo Waziri anasema nilete maoni tena.

Hata kama serikali haitaki, vuguvugu la wanannchi kuhusu katiba litachukua kasi. Serikali iachague tu, kufanya mabadiliko/kunadika katiba kwa hiari au kwa shinikizo.
 
Attachments

...tatizo la Tanzania ni umasikini na ubinafsi. watu wanajiunga na siasa kama njia ya kuondokana na umasikini na kutatua matatizo binafsi.

Hiyo katiba itakayoandikwa itakuwa na kitu gani kipya kurekebisha hali/mazingira niliyoeleza hapo juu?
 
Hili la mjadala wa Katiba halitatokea kama CCM hawataki period. What CCM wants CCM gets, it doesn't want this so we won't get it. Ndio maana mimi naona kujaribu kubadilisha Katiba wakati hauna nguvu ya kufanya hivyo ni kutwanga maji kinuni. Hadi pale wapinzani wananguvu ya kulazimisha siyo kuomba kama wanavyofanya sasa.

M.M
Mbona unakata tamaa mapema? CCM sio omnipotent/invincible. Sidhani kama wapinzani wanapoomba mabadiliko ya katiba, hawana alternative ya kulazimisha. Huko bungeni of course, hawana nguvu ya kulazimisha. Kuna maeneo mengine wana nguvu ya kutosha na ziada. Kitu pekee ninachohofia kutofanikisha hili la katiba mpya ni ubinafsi wa wapinzani.
 
Wakati Waziri anasema nilete maoni ya mabadiliko ya katiba kuhusu mfumo wa uchaguzi, tayari mnamo 31/5/2006 nilikuwa nimeandika barua kwa Rais kuhusu suala hili. Maoni gani tena yanatakiwa? nahisi serikali hii haina uratibu wa mambo yake. Barua hii ilichapishwa kama ilivyo na gazeti la Mtanzania. Wizara ya sheria na Katiba ilijibu barua yangu kuonesha wamepokea maoni yangu. Leo Waziri anasema nilete maoni tena.
Hata kama serikali haitaki, vuguvugu la wanannchi kuhusu katiba litachukua kasi. Serikali iachague tu, kufanya mabadiliko/kunadika katiba kwa hiari au kwa shinikizo.

Serikali ya CCM inafaidika na katiba iliyopo sasa, haioni umuhimu wowote wa kuibadilisha. Kwa nini iibadilishe katiba kama inafaidika nayo?

Hapa ndipo uongozi makini wa vyama vya ushindani unapotakiwa, kusimamia mageuzi haya ya katiba. Bila kuibadili hii katiba, demokrasi yetu itakuwa haijakamilika. Viongozi wa ushindani, acheni kuomba ruhusa. Ongozeni wananchi wachukue haki yao ya kuwa na katiba mpya. Mmekwishawaeleza wananchi kuwa hamtashiriki uchaguzi ujao bila ya kuwa na katiba mpya. Hiyo haitoshi, waambieni hapatakuwepo na uchaguzi 2010 bila ya katiba mpya. Wakati ni huu sasa hivi, kufanya mipango ya kuzuia uchaguzi huo.
 
Kalamu,

You r right man - ni wakati kwa vyama vya ushindani kutumia umma kuwashindikiza hawa jamaa (CCM)ni maandamano mtindo mmoja mpaka kieleweke
 
Mabadiliko ya katiba ni lazima - Mbowe

source:
http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/07/28/95288.html

"Mabadiliko ya katiba ni lazima - Mbowe"
Alisema, "mabadiliko ya katiba ya nchi ni ya lazima na kwamba hivi sasa vyama vya upinzani vipo katika mchakato wa kuandaa katiba mpya."

Vyama vya upinzani visituandalie katiba mpya. Vishughulikie kuishinikiza serikali ya CCM ikubali kubadili katiba. Utaratibu wa kuandaa katiba mpya ni wa wananchi kupitia katika wawakilishi na wataalamu mbalimbali watakaoteuliwa katika kamati mbalimbali zitakazohusika na uandaaji huo wa katiba.
 
Hiyo katiba mpya ya vyama vya ushindani itasaidia vipi kuishinikiza CCM ikubali kubadilisha Katiba?
 
Back
Top Bottom